Nimegeuka adui wa mzazi dhidi ya wanangu

Nimegeuka adui wa mzazi dhidi ya wanangu

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Wakuu sijui ni upendo ama nini maana wazazi wananigeukia balaa.

Mfano ;

Mwanangu akikosea nikimuadhibu mzazi wangu anakua mkali mno ananishambulia mpaka naona aibu,

Nifanyaje maana watoto ni wangu ila wazazi wangu wamewamiliki.
 
Wewe kwanini unaka kwa wazazi wako, na unapiga watoto wako baada ya kulewa, acha pombe mkuu.
 
Hama kwenu
Kaanzr maisha wewe na wanao.

Hasara za kuzalia home ni kufanywa mtoto
 
Aise ktk kipindi fimbo zitembezwe kwa watoto ni kipindi hiki. Tandika Hadi wakuone soro Hawa wazazi wako wasingekutandika Leo hi ungekuwa kibaka
 
Wakuu sijui ni upendo ama nini maana wazazi wananigeukia balaa.

Mfano ;

Mwanangu akikosea nikimuadhibu mzazi wangu anakua mkali mno ananishambulia mpaka naona aibu,

Nifanyaje maana watoto ni wangu ila wazazi wangu wamewamiliki.
Na wewe ni mtoto ndio maana.... mtoto kumpiga mtoto mwenzie nia kosa.lazima afokewe hata kufinya ikilazimika .
 
Aise ktk kipindi fimbo zitembezwe kwa watoto ni kipindi hiki. Tandika Hadi wakuone soro Hawa wazazi wako wasingekutandika Leo hi ungekuwa kibaka
Huyu bibi nae kwakweli simuelewi.

Ukigusa tu anakua mkali mno.

Niko njia panda maana bi mkubwa hataki niwaseme wajukuu wake.
 
Wewe kwanini unaka kwa wazazi wako, na unapiga watoto wako baada ya kulewa, acha pombe mkuu.
Kitu gani kimefanya uamini kwamba jamaa anaishi kwa wazazi wake?na hujui hata wewe hapo kuna namna ilibidi wazazi wako wakuadhibu ili uje kuwa na akili kama unazoona unazo leo?

So kila anaempa adhabu mtoto wake anakuwa amelewa pombe?
 
U

Una umri wa miaka mingapi?
Je wazazi wako mtoto wao wa mwisho ana umri gani?
Wastani wa umri wa wazazi wako ni miaka mingapi?
Watu wanavyomwambia akapange aondoke hapo nyumbn mnaweza msiish pamoja Ila ukimchapa mtoto anakimbilia kwa wazazii..... Humu watu sjui wanalewaga asubuhi

Nii kawaida wazazi kukataa kuchapa watoto lkn watoto wapigwe kisawasawa kwa fimbo sio mateke Wala ngumi no.....

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ndio baba yao.

Ila wazazi wangu hawataki niwaadhibu au hata kuwasema tu wanangu.

Jamani, dogo akikosea nikimsema bibi yake a awake utadhani nimeua??
Shukuru MUNGU una wazazi wanawajali wanao! Shukuru MUNGU!
Usipige watoto please
 
Kitu gani kimefanya uamini kwamba jamaa ana kwa wazazi wake?na hujui hata wewe hapo kuna namna ilibidi wazazi wako wakuadhibu ili uje kuwa na akili kama unazoona unazo leo?

So kila anaempa adhabu mtoto wake anakuwa amelewa pombe?
At least umeelewa wengine umu wanajibu tuu ilimradi, Hama apo..... Mara una hasira, sjui kulewa

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Mleta mada hiyo ni hali ya kawaida kwa wazazi wetu,wamesahau mtoto bila fimbo hakui ktk misingi iliyo bora kama walivyokuwa wanafanya kwetu.

Mimi nikiwa namwadhibu mwanangu kama bibi yake yupo nampeleka chemba namtia adabu mama akitetea namwambia mama tulia wewe nafasi yako umeshaimaliza niache nifanye yangu.
 
Saasa Role yangu kama mzazi ni ipi maana jamaa hawataki hata useme lolote.
Simama kama baba mtoto halelewi na bibi au babu bro,mimi mama yangu wakati wa udogo wangu kunilaza njaa kama adhabu ilikuwa kwake kitu simple tu,tena nikishalala njaa asubuhi naamka naenda shule bila kugusa chochote.

Leo mwanangu akengeuke nimwadhibu aseme niache?huyo wa kwangu ana tofauti gani na mimi nilipokuwa mdogo,siku hiyo mama amenitembelea kakuta mtoto ana mafua ananihimiza eti mpeleke hospital wakati mimi sikumbuki ni lini nilipata mafua yeye akanipeleka hospital.

Kumbukumbu zangu za utoto nikikumbuka siku niliyoenda hospital ni siku niliyoenda kutairiwa tu lakini mjukuu mafua kidogo anapiga kelele mtoto atapata shida zaidi muwahisheni hospital,wewe ndiye baba kazia malezi ya wanao kama yote unayoyafanya wazee wako walikufanyia elewa hukosei wao ndiyo wanaoona huruma kwa sababu mtoto akiharibika siyo wao watakaoumia ni wewe utakaeumia.
 
Back
Top Bottom