Nimegoma Kuwa Mnyonge Mbele ya Polisi

Nimegoma Kuwa Mnyonge Mbele ya Polisi

Pole sana mkuu.Binadamu ni mtu mbaya sana.

Na siku zote mpole na mkorofi hawakai sehemu moja.ila sumu ya mpole inapopata na kuwa jua hata yule mkorofi atamkimbia.

Rudi kwa mkuu wake umwambie maana ikitokea chochote atakuwa na la kuzungumzia.

Mi mwenyewe sipendi uonevu pasipokuwa na kosa.ukinifanyia mi naweza kukuchinja mchana kweupe.nikishindwa nitawamaliza hata watoto wako ,napenda kuishi kwa amani na kuwaheshimu watu wote,maana nikipandisha hasira nakuwa kama tembo
Mkuu,ile issue yako ya kukojoa kitandani uliisolve?
 
Traffic mwenye akili hawezi kukomalia kukomoa wananchi, maana rushwa kila siku wanachukua na kinyume na sheria, anashindwaje kusamehe?

unakutana na polisi kwa matatizo tu wala sio starehe au biashara.akikwambia utaona anakukumbusha uhusiano wenu mshindi wa mwisho ni yeye.siku itafika utatamani apokee rushwa halafu jamaa atakataa kabisa ili haki itendeke.

kwani ukishindana na polisi unapata faida gani zaidi ya kupoteza heshima yako???
 
Kangi Lugola kipindi akiwa waziri mambo ya ndani alikua hapendi ujinga wa hawa Wakuda alikua anawachana live hasa tabia ya kurusha JINI yani una-over speed Mlandizi picha inatumwa Chalinze.

Dawa nyingine ya hawa Wakuda wakikusimamisha ukuijua huna kosa tembea usisimame ndomana Kinana kawatoa nishai wana njaa kali sana.
Utajuaje kama huna kosa bila kuwasikiliza..ukiamsha si wanaanzia kukifukuzia wanajua huenda una kitu ambacho hakipo SAwa...Cha muhimu ninkusimama na kuwasikiliza pengine wanafanya ukaguzi ambao kisheria wanaruhusiwa
 
Nawasalimu! Tarehe 25/7/2022 nikiwa mizungukoni nilisimamishwa na Askari wa usalama barabarani wakaniomba leseni nikatoa kisha wakaikagua gari na kubaini sina dosari kisha nikaruhusiwa kuendelea na safari zangu.

Kesho yake tarehe 26/7/2022 nikiwa na familia yangu yaani mke na watoto wawili mahali fulani nilikutana na askari wa usalama barabarani wapatao 7, Wakanitaka niweke gari pembeni nikatii , Wakaitaka leseni nikawapa, Mmoja akaizunguka gari kisha akaja dirishani na kuniambia tairi moja imeisha hivyo nishuke garini ili waipeleke kituoni.

Shida ikaanza nilipomwambia mkuu mbona jana tu nilionekana sina tatizo lakini leo tayari tairi imeisha? Akanijibu vibaya kidogo nikaona niwe mpole, Nikamuomba niifikishe familia kisha nitaenda mwenyewe kituoni akagoma akawa mkali, Nikamuomba anipe muda mfupi ili nilifanyie kazi tatizo Akakataa na Kulazisha tushuke garini ili ipelekwe kituoni.

Kama baba Mbele ya Mke na Watoto sikuiubali Unyonge kwani Wazi Niliona Sitendewi haki, Nilishindwa kujizuwia nikamwambia Afande kusema Ukweli hakuna mtu yeyote atakayeshuka kwenye gari na Wewe au mwingine yeyote hapa hataendesha gari yangu.

Hali ikawa tete, Askari wawili wakapandisha Mori lakini kwa hakika Nilivurugwa kidogo kisaikolojia kwa wakati ule Nikawaambia wakati wowote kuanzia sasa endapo yeyote atanigusa au kufanya tofauti na maelezo yangu Hakika jambo baya sana litaenda kutokea. Mimi ni Mhehe original na kwa wakati ule nilijiona naenda kuacha historia mbaya muda wowote. Kwa Ufupi nilidhamiria kufanya jambo baya sana.

Wife anajua kuwa mimi sio mkorofi lakini nikifika kwenye point of no return huwa nakua mnyama, hivyo alishuka akawasihi wanitreat kwa tahadhari, nadhani kuna mmoja aliniangalia akajua sitanii na baada ya kujumuisha maneno ya wife akaona hapa tutaharibu hali ya hewa, Akaanza kuwasihi wenzake watulie kwanza ili yeye asolve ishu lakini hakufanikiwa.

Kufupisha ni kwamba Wawili walikomaa wakakaa garini na kunitaka nifuate maelekezo yao lakini nilivurumusha gari mpaka Ofisi za Polisi za Mkoa Nikashuka na Kuelekea Ofisini kwa RCO jamaa wakawa hawaelewi wakanifuata. Mwisho wa Yote niliacha kizaazaa kati yao na RCO. Walifokewa mno mbele yangu kwakuwaa maelezo yao hayakuwa na maana. Kitu nilipenda ni pale Walipoambiwa kuwa

"Mtakuja kufa kijinga nyinyi Watu Wamevurugwa na Maisha Na nyie mnawaletea fedheha mbele ya familia zao"

Niliambiwa niendelee na safari zangu na niachane na lolote waliloniambia wale askari, Nikawasha gari nikaondoka. Jana nimepita njia fulani nikamkuta mmoja kati ya Wale askari aliponiona aliniambia Bro mji mdogo huu tutaona mimi na wewe nani mjanja. Hii kauli imenifikirisha sana, Hebu nishaurini nifanyaje aisee manake naanza kuona dalili za kutokea kwa yale ya Iringa enzi zile za Yule mkuu wa mkoa na yule Mkulima. Nadhani nimeeleweka.

Nawasilisha.
Mwamwindi nakuamini sana, fanya mambo ikiwezekana nunua hata mguu wa kuku
 
Mi naamini hakuna jambo baya litalotokea kwako kama umeweza kuyashinda hayo yote hapo awali pasipo kuomba ushauri kwa yeyote basi hata hilo lingine halitakuwa suala zito sana
 
Endeleeni kuvimba nao had mwisho usitake ssukuhu Kama vip nikupe namba za kingai au muone katibu mkuu chongolo amishwe kituo haraka sanan
 
Nimesimamishwa na trafik wa ddm siku moja mbeele ya rto wa mkoa nikagoma kusimaa kwani nijifisha nyuma ya lory hvyo nikaendelea na safari huku kulikuwa na ugaguz mkuu nikaendelea na safari kufika mbele Mara naona gari ya police kwa nyuma wako na mapikipik Kama vile wanamfatilia gaidi dah wakaamuru magari mengine yakae pembeni ili waweze kuniteka vzr wakaniamuru niweka gar pembeni na kusiima kbsa bila kujali kuwa pale Kuna pakingi nikasimama Mona kwa moja wakasema nijeuze nirlekee kituo kiuu Cha polic nikiwa naendesha na kuzindikizwa. Nao wakiwa katk deifenda na pikipiki mbili na silaha nzito juu wakaniongoza had kituoni nigaoma kuendelea na gar kuisima ili kuwaomba msamaa wakasema. Shart nifike kituoni ndio nikaongee waktk nabishana nao mkuu wao akshuka ktk gari na kumuona mtu anaewasumbua poilice alfu shuka tu gafla nikaaona amenitambua na mm namjua vzr sna ila sikujuwa kuwa Ni rto wa ddm nikazuga Kama simjui na yey akazuga Kama hanijui ndio akanipiga piga biti akawambia jamaa wasaerach gari Kama nabeba madawa kumbe Sina kitu bas akawamuru matrafiki wankache tu kwani Ni muda mchache tu nilitoka kuandikiwa
 
Nimesimamishwa na trafik wa ddm siku moja mbeele ya rto wa mkoa nikagoma kusimaa kwani nijifisha nyuma ya lory hvyo nikaendelea na safari huku kulikuwa na ugaguz mkuu nikaendelea na safari kufika mbele Mara naona gari ya police kwa nyuma wako na mapikipik Kama vile wanamfatilia gaidi dah wakaamuru magari mengine yakae pembeni ili waweze kuniteka vzr wakaniamuru niweka gar pembeni na kusiima kbsa bila kujali kuwa pale Kuna pakingi nikasimama Mona kwa moja wakasema nijeuze nirlekee kituo kiuu Cha polic nikiwa naendesha na kuzindikizwa. Nao wakiwa katk deifenda na pikipiki mbili na silaha nzito juu wakaniongoza had kituoni nigaoma kuendelea na gar kuisima ili kuwaomba msamaa wakasema. Shart nifike kituoni ndio nikaongee waktk nabishana nao mkuu wao akshuka ktk gari na kumuona mtu anaewasumbua poilice alfu shuka tu gafla nikaaona amenitambua na mm namjua vzr sna ila sikujuwa kuwa Ni rto wa ddm nikazuga Kama simjui na yey akazuga Kama hanijui ndio akanipiga piga biti akawambia jamaa wasaerach gari Kama nabeba madawa kumbe Sina kitu bas akawamuru matrafiki wankache tu kwani Ni muda mchache tu nilitoka kuandikiwa

mkuu unatumia mbao kutype ktk keyboard[emoji80][emoji80]
 
Mkuu pambana ndivyo hivyo ulichagua kumaliza hilo jambo,wenzako wakiona kelele nyingi wanachana wallet,kama hela hamna unawasikiliza tu.

Huyo RTO mwenyewe kakujibu kisiasa,bila kujali wewe ndiye unakutana nao kila siku yeye akiwa ofisini tu hajui chochote.

Sasa kama una akili kubwa mfate huyo askari mpange awe mshkaji,sio kwa sababu wewe ni dhaifu sana,ila ni kwa sababu hujui kesho utakutwa na janga gani road hiyo na wa kukusaidia atakuwa nani.

Ukiona ni umama endelea kukaza tu.
Hii ni yenywe[emoji109]
 
Usihofu huyo hana madhara yoyote,
Haki haiji kwa kubembeleza, haki hutafutwa inapobidi.
Nadhani tuko pamoja nami sikubali kuonewa na yeyote nikiwa kwenye haki.
Niko Tayari kufanya lolote wakati wa kudai haki yangu.
 
Nllishamkunjaga shati trafiki mwaka 2014 mwezi may tar 8 barabara ya kutoka iringa mbeya naamini hakuamini na hato sahau maisha yake yote
 
yaani gari ya kwangu, alafu mtu apande bila ridhaa yangu, zaidi sana anidhalilishe mbele ya mke wangu na watoto. hilo siwezi kulikubali. binafsi traffic akinisimamisha huwa namsalimia akisema anataka kukagua gari namwambia karibu, kagua.

Akiomba leseni uwa namwambia nimeiacha ofisini au nyumbani ila ninayo (kisheria unaruhusiwa kuipeleka ndani ya siku mbili), na sishuki kwenye gari.

Sasa atasema nishuke kwa ajili ya nini?na milango nimelock ataingiaje? aongelee pale dirishani akimaliza kwisha. kama hajipendi sana basi anizuie wakati mimi nimekaa pale usukani na gari inaunguruma.

Wanaangaliaga sura pia wakiona mjinga mjinga ndio wanakunyanyasa, wakiona huyu kichwa kina akili huwa wanajiongeza.

Nikiwa na mke wangu na watoto heshima ile huwa nailinda kuliko hata pesa. huwezi kunidhalilisha mbele ya mke au watoto wangu. huwezi.
Watoto wanamini baba ananguvu kuliki wote lazma kulinda brand
 
Ukiwa na familia jitahidi usidhalilike kwa vyovyote vile
 
Back
Top Bottom