Nimegoma Kuwa Mnyonge Mbele ya Polisi

Nimegoma Kuwa Mnyonge Mbele ya Polisi

Hapana mkuu siishi huko nipo hapa hapa nchini ila nimebahatika mno kusafiri ndani ya nchi hii, chaguzi zao hazina migogoro na nilikua navutiwa mno na president wao ,mara nyingi alikua anatumia usafiri wa pikipiki (ride himself)na akiingia uwanjani anajichanganya na raia, Botswana wapo Safi sana mkuu, kwenye Army check points ndio pits stop za kulala usiku!,je unaweza park gari pale Lugalo Barracks na kuwaomba wale sentry kuwa unataka kulala!hii ni debate for another time
Heeeeh watakunyonya na nya.
 
Acha kuhalalisha ushenzi na ukatili huu,Zambia tu hapo check points zipo Safi kabisa, na wazee sisi wa road trips ndio tunawekaga pit stops (na za jeshi pia),Namibia wapo safi, SA wapo Safi unaweza kuendesha kutoka mother city hadi Egoli city bila ya kuingia kwenye road blocks yoyote (1400kms),Botswana ni A1 police na jeshi lao,Tanzania police wetu hili jeshi linahitaji kufanyiwa total overhaul, tuanze upya ikiwa na kuachana na hizi uniform za kikoloni, joto la Dar police wa kiume wave pensi, shirt jepesi, mkanda na service 🔫 kwenye kiuno, rangi za uniform iwe light blue!!
Jeshi letu si wanasema ni la kikoloni tulirithi kama lilivyo.
 
shida moja ni kwamba, jamaa alifanya ujinga wa kushuka kwenye gari. kati ya ujinga hutakiwi kuwafanyia polisi ni kushuka kwenye gari, kuwapa ufunguo, na kuwapa leseni. hatari nyingine ni kwamba, ukishafura ukawatishia kama alivyofanya yeye hapa, umewapa justification ya wato kukutreat kama mtu hatari.

Yaani kama wao wanatembea na bastola, manake wanaweza kukushuti kwasababu umewatishia na pengine wanahisi na wewe una mguu wa kuku, si ukute ukawa unajikuna tu kiunoni wakajua unawavizia uwalenge wakakupa ya kichwa.

ni kosa kubwa kumtishia polisi. we ongea naye maneno ya kawaida akikuzingua washa gari ondoka zako, akianza kukufukuza nenda tu kituo cha polisi au kama una mawasiliano na wakubwa zake wapigie adhalilike.
[emoji419]
 
Mkuu pambana ndivyo hivyo ulichagua kumaliza hilo jambo,wenzako wakiona kelele nyingi wanachana wallet,kama hela hamna unawasikiliza tu.

Huyo RTO mwenyewe kakujibu kisiasa,bila kujali wewe ndiye unakutana nao kila siku yeye akiwa ofisini tu hajui chochote.

Sasa kama una akili kubwa mfate huyo askari mpange awe mshkaji,sio kwa sababu wewe ni dhaifu sana,ila ni kwa sababu hujui kesho utakutwa na janga gani road hiyo na wa kukusaidia atakuwa nani.

Ukiona ni umama endelea kukaza tu.
Amfuate ya nin huna kosa alafu umfuate mtu muyajenge watanzania ni waoga sana Hana haja ya kumfuata huo ni mkwara tu
 
Thanks mkuu kwa taarifa hii, honestly usinielewe vibaya, nitajie road blocks or check points yeyote katika T1 yote ambayo iko na traffic officer's wanaotekeleza majukumu yao vema nitashukuru mno,maana nitakwenda mwenyewe na kuwapa high five
Acha huo ujinga wewe huna Kosa acha ufisi yaan unashindwa mpaka na madereva daladala
 
Nawasalimu! Tarehe 25/7/2022 nikiwa mizungukoni nilisimamishwa na Askari wa usalama barabarani wakaniomba leseni nikatoa kisha wakaikagua gari na kubaini sina dosari kisha nikaruhusiwa kuendelea na safari zangu.

Kesho yake tarehe 26/7/2022 nikiwa na familia yangu yaani mke na watoto wawili mahali fulani nilikutana na askari wa usalama barabarani wapatao 7, Wakanitaka niweke gari pembeni nikatii , Wakaitaka leseni nikawapa, Mmoja akaizunguka gari kisha akaja dirishani na kuniambia tairi moja imeisha hivyo nishuke garini ili waipeleke kituoni.

Shida ikaanza nilipomwambia mkuu mbona jana tu nilionekana sina tatizo lakini leo tayari tairi imeisha? Akanijibu vibaya kidogo nikaona niwe mpole, Nikamuomba niifikishe familia kisha nitaenda mwenyewe kituoni akagoma akawa mkali, Nikamuomba anipe muda mfupi ili nilifanyie kazi tatizo Akakataa na Kulazisha tushuke garini ili ipelekwe kituoni.

Kama baba Mbele ya Mke na Watoto sikuiubali Unyonge kwani Wazi Niliona Sitendewi haki, Nilishindwa kujizuwia nikamwambia Afande kusema Ukweli hakuna mtu yeyote atakayeshuka kwenye gari na Wewe au mwingine yeyote hapa hataendesha gari yangu.

Hali ikawa tete, Askari wawili wakapandisha Mori lakini kwa hakika Nilivurugwa kidogo kisaikolojia kwa wakati ule Nikawaambia wakati wowote kuanzia sasa endapo yeyote atanigusa au kufanya tofauti na maelezo yangu Hakika jambo baya sana litaenda kutokea. Mimi ni Mhehe original na kwa wakati ule nilijiona naenda kuacha historia mbaya muda wowote. Kwa Ufupi nilidhamiria kufanya jambo baya sana.

Wife anajua kuwa mimi sio mkorofi lakini nikifika kwenye point of no return huwa nakua mnyama, hivyo alishuka akawasihi wanitreat kwa tahadhari, nadhani kuna mmoja aliniangalia akajua sitanii na baada ya kujumoisha maneno ya wife akaona hapa tutaharibu hali ya hewa, Akaanza kuwasihi wenzake watulie kwanza ili yeye asolve ishu lakini hakufanikiwa.

Kufupisha ni kwamba Wawili walikomaa wakakaa garini na kunitaka nifuate maelekezo yao lakini nilivurumusha gari mpaka Ofisi za Polisi za Mkoa Nikashuka na Kuelekea Ofisini kwa RCO jamaa wakawa hawaelewi wakanifuata. Mwisho wa Yote niliacha kizaazaa kati yao na RCO. Walifokewa mno mbele yangu kwakuwaa maelezo yao hayakuwa na maana. Kitu nilipenda ni pale Walipoambiwa kuwa

"Mtakuja kufa kijinga nyinyi Watu Wamevurugwa na Maisha Na nyie mnawaletea fedheha mbele ya familia zao"

Niliambiwa niendelee na safari zangu na niachane na lolote waliloniambia wale askari, Nikawasha gari nikaondoka. Jana nimepita njia fulani nikamkuta mmoja kati ya Wale askari aliponiona aliniambia Bro mji mdogo huu tutaona mimi na wewe nani mjqnja. Hii kauli imenifikirisha sana, Hebu nishaurini nifanyaje aisee manake naanza kuona dalili za kutokea kwa yale ya Iringa enzi zile za Yule mkuu wa mkoa na yule Mkulima. Nadhani nimeeleweka.

Nawasilisha.
MWANAUME KUWA NA MSIMAMO, USIPIGWE MKWARA MDOGO HIVYO UNASHTUKA
 
Mikwara ya kijinga hiyo asikutishe hakuna kitu chochote atakachokufanyia fanya mambo yako tu Bongo wahuni wana vitisho wakati hawezi kufanya chochote na yeye mwenyewe anaweza kuwa mtuhumiwa vile vile..mimi huwa nakua mpole sana kwao ila wasinipande kichwani tuu...
 
Jamaa mwoga tu, hapo ana gari nzuri anatishwa hivyo,
Ajiulize virikuu vilivyo vibovu vinapita wapi? kama sio barabarani, na akihonga hela nyingi buku tatu, kuna wengine hadi hutoa buku tu,
Ukuwazoea traffic husumbuki unapeta tu,
Ukiwa na gari ya biashara tofauti na binafsi hawachukui hela hovyo hovyo mkuu
 
Jamaa mwoga tu, hapo ana gari nzuri anatishwa hivyo,
Ajiulize virikuu vilivyo vibovu vinapita wapi? kama sio barabarani, na akihonga hela nyingi buku tatu, kuna wengine hadi hutoa buku tu,
Ukuwazoea traffic husumbuki unapeta tu,
kweli kabisa, kujiamini muhimu
 
Broh ulichokosea ni kujua kama ww unakosa kweli.wakati hapo kesi ilikuwa kuwapa elfu 5 tu na kuondoka.wenyewe wanakusanya jion wanapiga pasu siku imeisha....vurugu za nini mji mdogo huu siku utapewa kesi ya ugaidi bureee kisa elfu 5
 
Jiandae kuwekewa Bangi kwenye gari yako mkuu
 
Mfute mwambie akae mbaliiii na gari lako maana Iko siku utampitia nalo aiache familia yake.
 
Unadhani hapa kwetu polisi wazuri hamna,ila wabaya wachache wanafanya polisi wote waonekane ovyo,lakini wazuri wapo wengi tu

Bro 90% ya traffic officers ni wasenge sana, labda hujakutana nao kwenye anga zao unaweza tamani kumtoa mtu mshipa.
 
Back
Top Bottom