Ni mwanangu wa kiume, wa 3 kuzaliwa and he is 5 years now.
Kuepusha maneno mengi ni kwamba muda huu yuko hospitali, na mama yake na baada ya diagnosis ikaonekana ana mchafuko wa damu na homa iko juu ana joto flan .
Baada ya kupata majib maabara na kumuona dokta akauliza
"AMESHAPEWA DAWA?".
Wife akasema HAPANA, DAWA GANI?
Dokta akamwambia "KWA JOTO HILO, ALIPASWA KUWEKEWA KIDONGE KATIKA NJIA YA HAJA KUBWA.
Bas wakiwa kwenye mazumgumzo nikapiga simu (mimi ni type ile ya watu kero wasumbufu hasa napo hisi ishu ni kubwa na mimi ndio nilipaswa kuwepo sasa ndio hivyo tena sipo, sasa huwa napiga sana simu kutaka kujua everything going on)
Wife akapokea akanipa hayo maelezo na ndio alikua anaelekea kutimiza huo utaratibu.
Nikauliza "KUSHUSHA HOMA NDIO LAZIMA KIDONGE KIWEKWE huko?"
akasema "NDIO NIMEAMBIWA HIVYO".
Nikasema "MWAMBIE DOKTA MUMEO KAKATAA, KAMA HAKUNA NAMNA NYINGINE BASI WAMWACHE TU, HIYO HOMA MPATIE PARACETAMOL"
AKASEMA SAWA.
Bahati mbaya sana kila mshkaj wangu ambaye ni dokta nikimpigia hapatikani au hapokei simu.
Nilitaka japo nipate consent zao kitaalam nijue japo sidhan kama ningekubal..atleast nilitaka tu kusikia wanasemaje?
Ndio hivyo wakuu NIMEGOMA.Mwanangu mwenyewe wa kiume ndio huyo huyo, wemgime wote watatu ni wakike, sasa waanze tena kumuweka vidongo njia ya hajakubwa viyeyukie humo halaf nini kitafuata.HAPANA KWAKWEL.
IMAWEZEKANA NIMEKOSEA ILA NDIO HIVYO, NIMEGOMA.
Habari!
1: Suala la kutokubaliana na matibabu au njia ya utoaji matibabu ni HAKI ya msingi kwa mgonjwa.
Daktari na mgonjwa hutakiwa kuelimishana juu ya kwa nini huyu anashauri hili na huyu hajakubaliana. Mwafaka hufikiwa na matibabu kutolewa kulingana na UHITAJI. Mbadala huweza kutumika kama upo kutatua kinachokwamisha.
2: Pale ambapo kuna UHITAJI WA HARAKA na hakuna kukubaliana, daktari anatakiwa kuhusisha uongozi wa hospitali/kituo cha afya (ETHICAL COMMITTEE) ili kupata ufumbuzi. Kama mambo yatakuwa bado na utata wa utoaji huduma, basi Hospitali na mgonjwa/ndugu wa mgonjwa huweza kuangalia mwafaka.
A: Weka mazingiza husika kwa kuhusisha wanasheria pia.
B: Kumpa mgonjwa rufaa ili akapate huduma mbadala kama inapatikana mwingine na ni salama kuhamishwa.
3: Watoa husima ya afya wanafanamu na wanatakiwa kutoa husuma kwa kizingatia MILA, DESTURI UTAMADUNI NA IMANI ya mteja kwa kuzingatia namba 1 na 2 hapo juu.
4: Kwa dawa kutolewa kupitia nhia ya haja kubwa. Dawa zipo na zimekuwa zikitolewa bila shida yoyote mfano: dawa ya kuzuia degedege, dawa ya kutibu bawasili, dawa ya kupunguza homa na uongezaji wa maji/drip kwa wale waliofanya kazi zamani. Msingi wa kutumia njia hii ni UHARAKA wa kufyonzwa dawa kupitia njia husika na kupunguza madhara. Pia kutobu tatizo husika kama liko swhemu husika.
Binafsi, huwa sipendelei kwa watoto zaidi ya miaka 3 (mitatu) kupewa dawa hizi kwa njia husika (Paracetamol vs Diclofenac) kutokana na kuanza kuwa na ufahamu wao. Bali pale ambapo ni hitaji muhimu kwelikweli au hatari mnele kulingana na aina ua mgonjwa.
5: Kwa kesi husika, hatuwezi kuizungumzia sana. Baba katimiza wajibu wake. Daktari pia alitakiwa kutimiza wajibu wake. Tatozo hatina maelezo ya upande wa pili. Hivyo, tuombe na kushukuru tu kwamba mtoto awe amepata huduma hitajika na kurejea kwenye afya yake.
Wito ni kuendela kuzingatia kupeana haki, nafasi na heshima kati yetu wote. Pia kuzingatia mahitaji ya kila mmoja yaliyopo kimaadili.