Nimegonganisha mabwana kanisani, nimetoka mzima, wanaume watu wa ajabu sana

Nimegonganisha mabwana kanisani, nimetoka mzima, wanaume watu wa ajabu sana

Money Penny

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2016
Posts
17,694
Reaction score
17,131
Mrembo: unajua Penny, nimefurahi umeanzisha youtube channel buana, sasa kuna ishu nataka nikupe

Money penny: enhe nambie mrembo

Mrembo: kuna wanaume wawili wananitaka,

Mmoja ni mtu mzima miaka 55 - Mpenzi A
Mwingine kijana miaka 35 - Mpenzi B
Kati ya hawa wawili wote siwaelewi,

Mwanzo Mpenzi A alinifukizia kwa mapenzi yote, baadae spidi ikaisha akapoa kabisa

Mpenzi B alianza kwa spidi sana, kadri nimemkazia akawa bado anataka tuwe wapenzi

Nikawaza sana ,nifanyaje nikaamua wote nikutane nao, nikalengesha waje kanisani wakaja

Mpenzi B akaja wa kwanza amewahi akaanzq kunitongoza wee, nikaona mpenzi B kama ametumwa na mpenzi A

Baada ya kutongozwa kwa dk 20 mpenzi A akaingia akatukuta tunaongea, mimi bila kupaniki nikamkaribisha mpenzi A nikamtambulisha kwa mpenzi B kuwa nae ananipenda na amekuja kunitongoza

Sasa kaeni hapo mniambie nani nimkubali kati yenu wawili

Wakakaa hapo money penny wananiangalia hawaelewi cha kufanya, baada ya dk 10 za kuduwaa, nikainuka nikaondoka kwenda nyumbani,

Mpaka leo nakuadithia hakuna hata mmoja alienitafuta ni wiki ya 3 sasa

Sielewi wanaume wanataka nini? Wanaume watu wa ajabu sana
 
Back
Top Bottom