Nimegugo dalili zote UKIMWI, ninazo

Kupima NO πŸ˜‚
 
Kwanza kabisa, nataka kukupongeza kwa ujasiri wa kutushirikisha hali unayopitia humi jukwaani.

Tambua ya kuwa u hatua moja mbele katika kupata usaidizi wa tatizo linalokusibu.

Ni jambo la kawaida kabisa kuhisi wasiwasi unapogundua mabadiliko mwilini mwako, na kutafuta taarifa ni hatua muhimu kuelekea kuelewa afya yako. Pia, ninaelewa jinsi inavyoweza kuwa ya kutisha kukabiliana na uwezekano wa kuwa na hali kama HIV.

Ni muhimu kukumbuka kwamba dalili unazopitia zinaweza kusababishwa na magonjwa kedekede, si HIV tu.

Njia pekee ya kweli kujua kinachoendelea ni kupitia upimaji wa kitabibu, ambao ninakuhimiza sana kuufikiria. Hii itakupa uhakika zaidi nini haswa kinakusibu.

Dawa za kisasa (ARV) zimepiga hatua kubwa, na hali nyingi, ikiwa ni pamoja na HIV, zinaweza kudhibitiwa kwa ufanisi mkubwa na huduma sahihi.

Kwenda hospitalini au kliniki kupimwa inaweza kuhisi inatisha, lakini ni tendo lenye nguvu la kujijali. Haijalishi matokeo, kupimwa ni hatua muhimu katika kuchukua udhibiti wa afya yako.

Ikiwa matokeo ni Negative, basi utapata utulivu wa akili na nafsi. Na endapo ikawa ni positive basi kujua mapema kutatuwezesha kuanza matibabu mapema ili kukufanya uwe na afya nzuri kwa miaka mingi ijayo. Kumbuka, utambuzi haukufafanui, na kuna jamii ya watu wanaoishi na virusu bila changamoto.

Ishinde hofu yako. Tafadhali fika hospital kupata uhakika wa afya yako. HIV una unafuu kuliko magonjwa mengi sana yanaoua kwa kasi hapa duniani.

Lakini kumbuka kuwa, wataalam wanapambana sana kupata dawa ya kuutibu ugonjwa husika. Miaka michache ijayo, nina uhakika dawa ya HIV itakuwa imeshapatikana..
 
Sikwenda kupima, mm mambo ya kupima Pima hapana, Ila ulikuwa ni mkanda ule maana upele uliwasha mgongoni mpaka kwa babu
Utakuja kujiua na presha bure
Kwanza leo nenda kapime presha ni lazima uko na presha alafu historia yako ndiyo inakusumbua tu
Inawezekana una kaugonjwa tu kengine lakini historia ya matukio yako ndiyo inakutisha
Hata huo mkanda hujawahi kuumwa kwa sababu kumbe hukwenda hata hospitali


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ila maisha
 
Kuna rafiki yangu nilisomanae Olevel na yeye alikuwa na dalili zote za HIV mpaka mkanda wa jeshi alipata. Muda wote analia tonsils vidonda vimejaa mdomoni Kuna siku daktari alimuuliza au unamchezo wa kunyonya K, kichwa kumuuma ilifika kipindi koo lilikuwa linamuuma anakooa damu kwenda Hospital wakamkuta na TB . Ikabidi wa mcheki HIV wakakuta negative.

So kuliko ujitese bure bora uendee ukapime ngoma ili ubaki na Amani ya moyo maana hata usipoenda haita badilisha kitu zaidi ya kuumia

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 

Mkuu kupima mm hapana naogopa naweza kukutwa na ng'weng'we 🀣
 
Ulipata Mkanda wa jeshi??😳😳
Au uligugo pia na wenyewe?
Nenda kapima achana na Gugo..
Ulipopata Mkanda wa jeshi ulitibiwaje na ulitibiwa wapi?
Maana nina amini kama uliambiwa Hospitali kuwa una mkanda wa Jeshi basi lazma walikupima..
Hajapata mkanda wa jeshi huyo, ni mkanda wake tu aliamua kuutoboa baada ya kukonda kiuno
 
Kupima NO πŸ˜‚
Mkuu nisikilize!
Kupima au kutokupima Haibadilishi uhalisia wowote!

Kwa mfano uliwa hauna na usipopima haikufanyi ukawa na maambukizi..
Lakini pia ukiwa Na maambukizi na usipopima haikufanyi usiwe na maambukizi..

Ila ukipima kwa Either status (Yaani uwe na maambukizi au usiwe nayo) inakufanya kutambua hali yako na kujiepushia Stress za Mara kwa mara..

Niamini nachokuambia Zamani 20% ya watu waliokuwa wanakufa walikuwa hawana maambukizi ila walikuwa na hofu ya kupata maambukizi ....

HIV anxiety au HIV paranoia ndio Huongoza kwa kuua watu sana!

Ukipima utajua nini cha kufanya kujilinda ili usipate maambukizi mapya au kuweza kumantain status yako na kuwa bora zaidi

Asante
 
TB sindodalili kuu ya HIV mkuu
 
Acha kukaa kwenye speculation kapime
 

NEVER GOOGLE YOUR SYMPTOMS

https://www.youtube.com/watch?v=Vn_ZkI7-IZ4&pp=ygUabmV2ZXIgZ29vZ2xlIHlvdXIgc3ltcHRvbXM=
 
Siku hizi watu tuna bahati sayansi imeendelea hiv inadhibitika miaka ya themanini mtu unakonda unadhalilika kabisa , sikuhizi umekuwa kama ugonjwa mwingine wa kawaida siyo tena hatari na wa kuuwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…