Nimegundua madaktari wengi wanaoa wagonjwa wao!

Kila mtu anakutana na watu wengi mahala pake pa kazi, na pale mahala unapokutana na wengi ndio mahala ambapo likelihood ya kupatia mwenza ipo! Ndio maana wapenda disco wanakutana disco, wapenda kusali wanakutana kanisani, waenda bar wanakutana bar, makonda wanakutana kwenye dala dala (kila mara anapanda hilo gari mpaka wanazoeana na kuanza kupunguziana nauli), walimu wanaoa wanafunzi wao etc etc
 
Ongezea ma lecture wengi wanaoa wanachuo wanaowafundisha hasa IFM
 
Siyo kweli,huo ni mtazamo fanya utafi wa kutosha..maana wengine wanasema always dr vs nurse, dr vs dr, dr vs mwalimu...

Jaribu kufanya utafiti na wewe mkuu, watu wengi wanaingia katika mahusiano na watu wanao onana nao katika mazingira ya kazi zao kila wakati!
 

Hiyo sentensi ya mwisho mbona imepingana na maelezo yako!?? Au ni kimombo mkuu dokta!



BTW hizo huwa stereotypes ama generalizations kama maaskari kuwaoa wanaokujaga vituoni kuleta malalamiko, watuhumiwa or the likes!
 
Hata waalimu pia, hasa wa vyuo, huoa wanafunzi wao. Ni hali iliyopo ambayo haizuiliki.
 
kiasi si sana,ingawa wengi wao huchepukia kwa ma nurse wa kike
 
Hiyo sentensi ya mwisho mbona imepingana na maelezo yako!?? Au ni kimombo mkuu dokta!



BTW hizo huwa stereotypes ama generalizations kama maaskari kuwaoa wanaokujaga vituoni kuleta malalamiko, watuhumiwa or the likes!

Mkuu..i meant to say simply because the idea seems to work..with defined logical path way...does not necessarily mean we have enough evidence to conclude...hapa katika line ya argument ya mtoa mada kuna potential BIAS...so huwez kuconclude based on that....in other words numbers speak for themselves
 
Mimi natoa mifano ya kweli Dada yangu kaolewa na Daktari wakati yeye ni Nurse, jirani yangu mume ni daktari wakati mkewe ni mwalimu. Shemeji yangu ni Daktari wa Jeshi, mkewe ni Nurse. Family friend wetu ni Daktari na mke wake ni nurse, hiyo ni mifano ya kweli ninayoijua.
 
Jamani, sasa daktari akaoe mfungwa? Labda we daktari wa magereza.

Waswahili wanasema, kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.

Walimu wanaoa wanafunzi, kama huamini angalia vyuoni.

Wanafunzi wanaoana wao kwa wao.

Sioni ajabu, ingekuwa ajabu kama madaktari wangeoa sana waganga wa kienyeji, ngestukia dawa zao.
 
My hezbend C6 hivi mie na wewe tulikutana wapi vile???
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…