Nimegundua matajiri wengi hapa Tanzania hawajasoma

Utajiri ni wide concept na Utajiri haupatikani tu kwa kusoma, unaweza uka approach kwa mbishe mbishe nyingine, take as kusoma kama silaha ya kuuondoa umaskini, una utilize vipi elimu yako kupata utajiri hapo ndio kipengele
 
Huyu ndio Simba wa buyenzi my man πŸ˜‚
 
Hili wasomi wengi wakilitambua litakua na matokeo chanya na kuijenga upya jamii yetu.

Si ajabu hii ya kila mtu kutaka kua tajiri mkubwa ndo chanzo kimojawapo cha kutowajibika, rushwa, ufisadi ulikithiri nk

Kila mtu atataka afanikiwe kwenye sekta yake, muhasibu OKW BOBAN SUNZU atataka kujenga maghorofa kwa pesa za umma na wengine kula kwa urefu wa kamba zao.
 
Elim ya Tanzania na Africa kwa ujumla Ina wafanya wa watu kuwa watumwa wa elimu Yao. Nchi kama tanzia hautaji Elim ya natharia, inahitajika elimu ya vitendo zaidi.
 
Nowadays mkubwa unaleta vitu heavy mno kimsingi l appreciate.
 
Kwani inahitaji elimu kubwa sana katika kuchimba madini, kulima, kufuga, kuchuuza vitu, kuiibia serikali au kufanya udalali??....

Kiuhalisia, Tanzania ni nchi ambayo imekaa kiukulima, kiuchuuzi, kiufanyakazi na vitu vyote ambavyo havihitaji MIFUMO. Kwa hiyo watu wenye elimu, vipaji na uwezo kiakili sio rahisi kutoboa maana nchi haina mfumo wa kulinda gunduzi zao kiasi cha kuwanufaisha ndio maana ni ngumu kukuta matajiri waliotengenezwa na teknolojia ama sanaa..

Benjamin fernandez tu aliona akaipeleke NALA nairobi kuliko Dar maana aliona atafeli

Cha kusikitisha watu wengi wanaendelea kulaumu wasomi daily kwa kuwashauri wafanye hand to mouth, lakini ni nani anaewashauri viongozi wetu kuweka system za kulinda gundizi na kazi za sanaa ili watu kama hai wasife njaa..

Sio kila mtu anatakiwa kuwa mkulima wa jembe la mkono kwa karne hii ya 21
 
πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ

Kinachostahili kuwekwa ni mfumo, ukiangalia duniani, working class au middle income class wengi ni elites kutokana na professional works

Ukiangalia pia, nchi hizo zimeweka mifumo thabiti kiasi kwamba kila mwenye potential, iwe ya darasani au si ya darasani anatoboa..

Mfano leo hii msanii kama Michael Jackson, pesa anayoiingiza akiwa amelala kaburini inaweza kulea beneficiaries wake pasipo wao kufanya kazi.

Hao kina Mark, bill gates au elon, wote wanafanikiwa kwa sababu patent system ipo vizuri.. Njoo huku kwetu

Leo msomi akifanya invention, anafaidikaje nayo

Kina kanumba au Ngwair, Leo kazi zao zinafaidishaje familia zao

The issue is, katika nchi ambayo brains zinazoiendesha zinawashauri wasomi kutofikiria au kufanya makubwa zaidi ya kwenda kwenye kilimo cha jembe la mkono. Matajiri gani wanaweza kuzalishwa

Issue hii ni pana brother but in reality, mifumo kwa Tanzania hakuna ndio maana hata private sector inachechemea. Na bila private sector kubwa, matajiri watapatikana wapi brother??
 
Rostam Aziz Hana degree ya uchumi!!
 
Mzee Mengi ni CPA holder wa Kwanza Kwanza.
 
Elimu versus Akili versus Mafanikio katika maisha.

Unaweza ukasoma sana lakini unaweza ukawa haujaelimika.

Aidha, unaweza kuelimika sana lakini Elimu yako ikawa haijakukomboa katika maisha yako.
Kusoma ni jambo moja, akili jingine, juhudi, maarifa na utajiri (wa mali, ambao siyo lazima yawe mafanikio) ni mengine pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…