Nimegundua matajiri wengi hapa Tanzania hawajasoma

Hii obsession ya kwamba eti wasomi (wengi/wote) wanapaswa kutajirika kwa vile tu wamesoma ni kiinimacho tu ambacho hakina uhalisia katika kanuni za kiuchumi na uhalisia wa maisha.
Bongo hii unakuta mtu ni muuguzi hapo hapo ana mawazo ya kuwa kama bakhressa angali ameajiriwa 😀
Sijui watu hawaja tambua bado kuwa sifa ya pesa ni kuwa scarce hamna pesa ya kumtosha kila mtu
 
Mpumbavu kwanini ulisoma ungebaki Bila elimu ili na wewe uwe tajiri
 
Kwani hao wasomi si ndio wamerudikana serikalini? Hao wasomi si ndio wanao kula rushwa makazi I mwao? Mbona serikali inapo sign mkataba mibovu na sheria mbovu hawajitokezi kupinga au ushauri. Hao wasomi si ndio machawa? Mbona hatuoni vyuo vikuu vigoma au kujadili udhaifu wa serikali?
 

#Mfumo

Haijalishi ni Mzuri au mbaya ukishaingia kwenye mfumo mbovu ni lazma utakuwa mbovu. Aidha ukae nje ujilinde, upambane na mfumo pasipo kujali uhai wako au la ujue kula na vipofu ili maisha yako yanyooke. Hizo ndio codes za mjini

By the way kuna maandamano mengi tu duniani yalichochewa na kukuzwa na watu ambao hawana elimu rasmi.

Kwa hiyo, jukumu la kuwa mzalendo ni la kila mtu Ila kama tutawakuza watoto kwa familia dhaifu, sidhani kama elimu inaweza kuwajengea ushupavu. Tuishi humo kwanza mkuu
 
Tajiri maana yake ni nini?
Alafu Kuwa tajiri inategemea na dili ulilokutana nalo 😀😀,serikalini matajiri wapo kibao ila wamejificha hawajulikani

Ingia kwenye mfumo haijalishi una akili au huna

Wewe ni masikini kwa kua haupo kwenye mfumo tu
 
Utajiri wa Tanzania hauhusiani na taaluma wala teknolojia. Unapatikana kwa janjajanja nyingi, utapeli, ukwepaji kodi, connection za serikali, ndumba (kwa wanaoamini) na vitu aina hiyo. Haufundishiki. Kipaji asilia ndicho kinahitajika.

Shule haihitajiki wala hauwezi kurithishwa kikawaida. Labda kwa zindiko. Hauna value-added kwa jamii. Ni kama uganga wa kienyeji au uchawi. Tuseme ni kipaji asilia. Matajiri wamejaa bungeni; hawatoki kirahisi ila kwa fitna.
 
Haya kunya boga
 
Halafu hii kuona utajiri hauna uhusiano na shule ndio umetufikisha kwenye kukabidhi njia kuu za uchumi kwa wawekezaji (read: matajiri) wa nje: bandari, gesi, migodi ya madini, mobile telephony, n.k. Baadaye kidogo tutawakabidhi reli, ndege, misitu, mashamba na Vinginevyo watuendeshee.

Hizo ni fursa kubwa sana za utajiri. Lakini kwa vile tuna sema hatuna technical-know how basi inabidi tuwaachie wenye “kujua” wafanye yao bila watu wetu nao kuwa na ushiriki wa kutosha katika manufaa ya ukwasi huo. Sisi tunaridhika kubakia na utajiri wetu wa “ndumba” usiohitaji elimu ya shule.

Imagine makampuni ya Kenya yanaingia nchini kukusanya maparachichi, mahindi, kahawa, n.k. kwenda kwao kuchambuliwa kwa grades, kufungashwa kitaalamu na kuuzwa nje kama Produce of Kenya!

Serikali ina jukumu zito la kuhakikisha uwekezaji wa kisomi unatamalaki nchini. Waangalie jinsi serikali ya Kenya inavyoshirikiana na private sector kuimarisha uchumi. Pamoja na umuhimu wa kubalance na huduma kwa “wanyonge”, serikali inatakiwa ishughulike na hizo complexes zote. Siasa rahisi rahisi za enzi za “ujamaa” hazisaidii zaidi ya kujenga jamii yenye unafiki mwingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…