Nimegundua mdogo wangu ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu

Nimegundua mdogo wangu ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu

Mwache!Maumivuu yataisha,Utasahau.Na kuopoa Mwingine.Mbona wako wengi.Kila kitu kinatokea Kwa sababu.Chukulia kama funzo Kwa yaliyo kutokea.
 
Kufa waoane.
Piga kimya tafuta chombo kipya yaani pisi kali kuzidi muonyeshe mahaba ndi ndi ndi. Malipo ni hapa hapa duniani...sa we unataka kwenda wapi
 
Ngoja nikwambie kitu, kama umeamini ni kweli Waite wote wakalishe hafu waambie walete simu zao waoneshe chati zao Kisha waambie endeleeni na mapenzi yenu na wewe ondoka kaendelee na mambo mengine wasichana ni wengi tu wazuri na waaminifu. Mwisho usiwe na roho nyepesi yaani unywe sumu kisa mwanamke ebo! Huo ni utoto
Kwahiyo watoto ndiyo huwa wanakunywa sumu kwa sababu ya mapenzi? 😳
 
Pole, mwachie dogo zigo we fanya ile ela uliyokuwa unatumia kumhudumia idundulize ukapange uhame kwa mama.
We kwanza chukua tena simu ya dogo uchukue ushahidi kisha wachane ukweli na uwaambie umeacha waendelee na mahusiano.
Uwa tunaamini sana wadogo zetu ila wanakulaga sana mashemej wao
Amwachie dogo huyo mwanamke,yy ajipige kifua ahame pale kwao akapange huko, kwasababu ningumu kuharibu mahusiano nanduguyako kisa mwanamke,isitoshe huenda couple Yahuyo demu wake namdogo wake ikadumu kuliko yy,awe mpole Tu akubali kushindwa namdogo Ake, asiyekubali kushindwa sio mshindani!
 
Ngoja nikwambie kitu, kama umeamini ni kweli Waite wote wakalishe hafu waambie walete simu zao waoneshe chati zao Kisha waambie endeleeni na mapenzi yenu na wewe ondoka kaendelee na mambo mengine wasichana ni wengi tu wazuri na waaminifu. Mwisho usiwe na roho nyepesi yaani unywe sumu kisa mwanamke ebo! Huo ni utoto
Hapo atakua kamdhalilisha mdogo Ake!aondoke Tu hapo home aiseee
 
Mbona issue yako ni ndogo tu,yaani ujiue kwa ajili ya jitu mlilokutana mkiwa tayari mmeota vuzi,
Kata mawasiliano kimyakimya na ikiwezekana hama hapo kwenu kajitegemee,akikutafuta mwambie uko busy utamcheki na akiendelea zaidi mwambie maagizo yote kuhusu yeye umemuachia mdogo wake,hivyo kama ni pesa mdogo wako atampa,pia kama na tango mdogo wako pia atampa,na kumbuka kizuri kula na nduguyo acha uchoyo.
Ushauri Bora kabisa mkuu,mshikaji asipoelewa
 
Mbona issue yako ni ndogo tu,yaani ujiue kwa ajili ya jitu mlilokutana mkiwa tayari mmeota vuzi,
Kata mawasiliano kimyakimya na ikiwezekana hama hapo kwenu kajitegemee,akikutafuta mwambie uko busy utamcheki na akiendelea zaidi mwambie maagizo yote kuhusu yeye umemuachia mdogo wake,hivyo kama ni pesa mdogo wako atampa,pia kama na tango mdogo wako pia atampa,na kumbuka kizuri kula na nduguyo acha uchoyo.
Ushauri Bora kabisa mkuu,mshikaji asipoelewa nahapa daahhh,amwachie mdogo Ake awe busy namambo yake mwisho ahame hapo!
 
Habari za muda huu wanajamvi? Ni matumaini yangu kwamba mnaelendea vyema na majukumu yenu.Nimekumbwa na msongo mkubwa sana wa mawazo baada ya kugundua mdogo wangu wa kiume Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu ninayempenda kwa dhati Sana.Kwa hyo Naomba mnishauri vizuri baada ya kusoma kisa changu kifuatacho.

Nina mpenzi wangu mwenye miaka 24 na nimedate naye kwa muda wa miezi Saba Sasa.Ni mwanamke ambaye ninampenda kea dhati yangu yote na nilikuwa na malengo makubwa Sana naye ikiwemo ndoa.Tumekuwa tunapendana Sana na Mara nyingi anakujaga home kwetu kunitembelea mixer kutangamana na familia yangu( ndugu na wazazi wangu).
Alijenga mazoea makubwa Sana na familia yangu hasa ndugu yangu mdogo wa kiume ( ninamzidi na miaka 4) Hadi wakafikia hatua ya kubadilishiana mawasiliano wakawa wanaongea kwa pigo za kishemeji shemeji.Hilo sikuwa na tatizo nalo maana nilijua huyu Ni ndugu yangu mdogo namwaminia kwahyo sikuwahi waza kwamba anaweza date na demu wangu.

Huyu mpenzi wangu nilikuwa nampenda kwa dhati Sana na toka nianze kudate naye Wala sijawahi mcheat na demu mwingine.Nilikuwa namprovaidia Kila kitu ambacho mwanamke anahitaji kutoka kwa mpenzi wake.Nilikuwa namtazamia kula yake,mavazi,nauli,hela ya saloon,namuungia bundle na vocha kwenye simu yake,namtoa out mixer hela ya matumizi mengine ya kawaida.Chumbani Napo nilikuwa Nampa tango Yaani nilikuwa napiga shoo za nguvu Hadi ananistukia.Kwahyo ninaweza kusema kwamba mpaka muda huu sijawahi mzingua kwa lolote.
Naye hakuwahi kuonesha ishara za kudate na mwanaume mwingine tofauti na Mimi mpaka leo nilipogundua kwamba anadate na mdogo wangu[emoji24][emoji24][emoji24]

Leo mida ya asubuhi tulikuwa sebuleni kwa mama tunashusha kiamsha kinya mixer kupiga story za matukio.Mdogo wangu alikuwa amekaa mkabala na Mimi na simu yake alikuwa ameiweka juu ya meza.
Sasa kipindi tunaendelea kunywa chai alikuja rafiki yake akamwita nje waongee kdgo.Alipotoka ghafla simu yake ikaanza kuita nikaona jina imeandika " SAM" afu number Nikaona ni ya huyo mpenzi wangu kbsa.Nilishtuka Sana na nikaanza kujiuliza kwanini mdogo amsevu mpenzi wangu( shemeji yake) jina tofauti na lake.Mpenzi wangu anaitwa Suzie afu yeye amemsevu SAM,kwanini?[emoji848][emoji848][emoji848] Nikajua Kuna kitu kitakuwa kinaendelea Kati ya Hawa wawili.

Brother aliporudi ndani nikamwambia simu yake ilikuwa inaita akaichukua akaona missed call akasema this is confidential akatoka nje akampigia.Waliongea muda mrefu Sana nami nikawa nimechanganyikiwa mazima Moyo ukaanza kutetemeka Hadi nikashindwa kuendelea kunywa chai.

Aliporudi ndani nilijifanya sijui kinachoendelea nikachora plan ya kumuomba simu yake niujue ukweli wote.Nilianza kuzuga zuga kwamba nahitaji kuongea na mshikaji wangu mmoja nifanye naye biashara fulani muhimu kbsa ila Sina vocha kwenye simu.Nikamwambia mdogo wangu Kama Ana credit kwenye simu yake anipe japo kwa dakika tano nionge na jamaa aje tufanye biashara.Bro hakumaind Sana akachukua simu akaweka password akanikabidhi nikatoka nje.

Moja kwa Moja nilingia kwenye what's up yake nikafungua chats za Sam( ambaye ndio mpenzi wangu Sasa). Aisee nilihisi nimepigwa na kitu kizoto kichwani mwangu baada ya kusoma baadhi ya charts Kati ya mdogo wangu na Mpenzi wangu.Nilikugundua Hawa wawili Wana mahusiano ya kimapenzi yaliyo serious kbsa.Texts za mahaba na picha za uchi ndo zimesheheni kwenye what's ya ndugu yangu.Mpaka wakaelezana walivyoenjoy sex kipindi fulani [emoji24][emoji24][emoji24]

Nilibujikwa na machozi mengi Sana mixer kosononeja moyono baada ya kukutana na Mambo ambayo kamwe sikuwahi tarajia kama yanaweza kutokea.Nilifuta machozi yangu nikaosha uso ili kuficha sonona yangu.Nilimrudishia simu yake nikatoka upesi huku natetemeka Sana.

Kiukweli Nina hasira nyingi Sana kwa ndugu baada ya kugundua unyama anaonifanyia na Mpenzi wangu.Nawaza Mambo mengi kichwani na nimekosa amani ya moyoni kbsa.Muda huu nipo kwenye baa fulani kwenye mtaa najianda kuagiza pombe ninywe nilewe nijaribu kupoza maumivu ninayohisi pindi nitakapomaliza kuiwasilisha hii thread kwenu Wana JF mnipe ushauri.

Natamani ninywe sumu nikafe tu maana mwanamke niliyekuwa na malengo makubwa Nate ndo huyo ananicheat na ndugu yangu.Waliowahi kupatwa na maumivu ya mapenzi bila Shaka wanajua magumu ninayopitia muda huu.Akili zimesimama,Moyo unauma,kichwa kinaumwa na mwili unatetemeka.Bado nampenda Sana na kumuhitaji mpenzi wangu ila Niko njia panda sijui nifanyeje tu.

Ushauri wenu utanifaa zaidi katika huu msala nilionao.
Pole sana kwa changamoto husika! Ni dhahiŕi kwamba, huyo mwanamke hakufai tena kwa sasa! Aidha, shukuru hilo umelifahamu mapenzi yenu yakiwa katika hatua ya kawaida!

Ushauri wangu, tafuta mwingine sahihi wa kuambatana naye, mind you, "ni rahisi kuchagua kibaya kwenye vingi vizuri, ila ni ngumu kuchagua bora zaidi katika vingi vizuri".

Chukua hiyo hali kama changamoto, na mara nyingi, changamoto ni fursa.
Cheers.
 
mda mfupi baada ya kunywa sumu na kufanikiwa kufa
FB_IMG_1647160657319.jpg
 
Amwachie dogo huyo mwanamke,yy ajipige kifua ahame pale kwao akapange huko,kwasababu ningumu kuharibu mahusiano nanduguyako kisa mwanamke,isitoshe huenda couple Yahuyo demu wake namdogo wake ikadumu kuliko yy,awe mpole Tu akubali kushindwa namdogo Ake,asiyekubali kushindwa sio mshindani!
Ahsante Sana mkuu kwa ushauri wako
 
Pole sana kwa changamoto husika! Ni dhahiŕi kwamba, huyo mwanamke hakufai tena kwa sasa! Aidha, shukuru hilo umelifahamu mapenzi yenu yakiwa katika hatua ya kawaida! Ushauri wangu, tafuta mwingine sahihi wa kuambatana naye, mind you, "ni rahisi kuchagua kibaya kwenye vingi vizuri, ila ni ngumu kuchagua bora zaidi katika vingi vizuri". Chukua hiyo hali kama changamoto, na mara nyingi, changamoto ni fursa.
Cheers.
Nashukuru Sana mkuu kwa ushauri wako,nimeupenda Sana na nitaufanyia kazi
 
Mm nashauiri Bora tu Unywe Sumu Ufe.

Wanaume tumejitolea kuja Kukuzika maana umetuaibisha sana kwa Mawazo yako hayo
 
Achana na huyo mwanamke. Yes, siyo uamuzi rahisi kufanya lakini you have tu.

Na ni lazima ujue kabisa break ups zote huwa na maumivu makali, jiandae kisaikolojia.

Habari njema ni kuwa muda huponya, kubali kupitia hayo maumivu wakati una-heal.
 
Kama una uwezo wa kumhudumia manzi inakuwaje unakubali kugombania vitumbua na mdogo wako ndo maana na yeye kajiongeza
Ushauri anzisha ghetto mbali na kwenu na hutasahau kirahisi halafu acha uboya wa kuwa na dem mmoja utakufa siku si zako
 
Back
Top Bottom