Nimegundua mdogo wangu ana mahusiano ya kimapenzi na Mpenzi wangu

Mtoa mada inaonesha mmelelewa kijunior sana ko mna elements za kike kike hivi.

Sasa kinachokuliza nini hapo? Waite wote uwaoneshe ushahidi afu upige chini mazima.

Simple.
 
Ushauri wangu, pole najua ni ngumu sana kuwa na hii hali ila niamini Mungu ni Mkuu amekunusuru na mwanamke muovu ambeye angekuja kukuumiza akiwa ndani ya ndoa.

Kuna kitu huwa vijana mnakosea sana kwenye mahusiano, Lengo kubwa la kuwa wachumba ni kusomana kujuana vema ili kama kuna vijimambo visivyo vumilika unakutana navyo basi ndiyo fursa uliyo nayo ya kuachana na Mchumba wako na sio wakati wa ndoa.

Kwenye uchumba kuna mambo ambayo unapaswa kuya seti pamoja kwa level hiyo ya uchumba na kuna mambo ambayo mnayaseti mkiwa na ndoa, inaonekana wewe uliruka hatua moja ukaenda ya mbele.

Kipindi cha uchumba ndicho kipindi ambacho unatakiwa umpime mchumba wako kwa nyanja zote, uaminifu, upendo, mahusiano na watu, wivu, uchoyo na ndio kipindi cha kumjaribu uwaminifu wake kwa mfanyia visa, ndio wakati wa kugombana sana.

Sasa wewe Mungu kakuonyesha panapovuja wewe badala ya kutoa shukrani una lialia huo ni udhaifu mkubwa sana.

Kaa chini mpige chini halafu usimwambie ndugu yako atasikia kupitia kwake
 
#KataaWahuni.

Songa mbele...
 
Kusononeka moyoni
 
Eeh jamani Hadi unawaza kujiua kweli?? Usijiue bwana hayo maumivu kawaida tu utasahau na yataisha halafu utakuja kukumbuka ulitaka kujiua kisa ujinga unaanza kujicheka tu😄😄,Ila kwa jinsi ulivyoandika inaonekana wewe ndo ulimpenda zaidi Suzy.Usije ukarudiana nae maana next time utakufa kweli bila kujiua mwanamke ambaye anatembea na ndugu yako ujue huko kwa majirani na mtaa mzima kamaliza.Mapenzi nayo ni ujinga tu Kama ujinga mwingine kua tu single ufanye zako ujasiriamali ☹️☹️achana na mapenzi bongo hii utakufa kweli nakuambia shauri yako.
 
Acha wivu ww wacha dogo afaidi yaliyomo kwa shemeji yake
 
Oya we mzee mbona umesusa uzi? Ushajiua nini?
 
Nice Guys, finish Last.

Usirudie huo Ujinga huko unakoenda,,, Hao kenge hawana jema,, fanya vile utavoona wewe inakufaaaa...

Kingine unasema unawaza ujiue..??? Unataka kuthibitishia Dunia kuwa Wazazi wako walilea PUMBAVU moja hivi..
Acha ufalla na kuendekeza mapenzi,, hama nyumbani... Mtaani kwenye utafutaji kuna stress nyingi mno,,hizo zikikukuta si ndio utauza tiGo kabisa,,
Achana na huyo mwanamke au kubali kuendelea kula na mdogo wako,, Mtu isipomfaa akili yake, basi utamdhuru ujinga wake.

Narudia tena Dogo achana na mawazo ya kujiua,, umenitia hasira sana natamani nikuzabe makofi,,watu wanapammbania uhai humu kwenye hospital halafu wewe kenge unataka kujiua kisa tundu katikati ya miguu ya Demu,, Pumbavu kweli wewe...

Ukiona hii ni ngumu kuitafuna, basi jitahidi usiimeze haraka.....
 
Unapaswa umshirikishe mama yako aone matendo ya mdogo wako na huyo mwanamke ushahidi wa mama ni mzuri yeye anaweza kuwa na namna nzuri usilibebe wewe ongea na mama ila hakikisha uwe na hio simu na mjifungie ndani wewe na mama na mhakikishie mama kuwa hutaleta ugomvi, hii muhimu kwa mustakabali wa undugu na maisha ya badae.

Mengine sikwambii mfano mimi maadui zangu nina 5-10yrs za kuwadhuru na kuwangamiza ila kwa sasa hakuna ajuae ninalopanga na naishi nao normal tu kwa sasa ni methods nshazipanga kbsa.

The mamba the lion hybrid
 
Analysis:
Demu ana around 24 yrs means utakua umemzid (Assumption) na kama dogo umempiga gape la 4 years nakadilia upo around 29/30,bro pambana hama hapo home.Tafuta ule uzi wa "ulianzaje kukaa ghetto"
Ushauri:
Huyu dogo na shemeji yake wameivana na penzi limenoga kufikia hatua wanatumiana nudes,fanya kumpiga chini tu afu pambania issue za msingi kwasasa
 
Ahsante Sana mkuu kwa ushauri wako,Mungu na akubariki Sana.
 
Mkuu akishajiua mwambie aniambie nimshauri maana kama ni utoto na ushamba,

Hao viumbe ni tabu tupu, mwanamke mpende kiasi na umchukie kiasi yaani kila kitu ufanyacho fanyavkwa kiasi hautojutia maishani mwako

Kama atapita kusoma tena kwa akili njema za malezi ya wazazi wake walizomlelea atajifunza kitu
 
Mengine sikwambii mfano mimi maadui zangu nina 5-10yrs za kuwadhuru na kuwangamiza ila kwa sasa hakuna ajuae ninalopanga na naishi nao normal tu kwa sasa ni methods nshazipanga kbsa.

The mamba the lion hybrid

Hivi kwanini lazima rafiki yako/zako baadae wageuke kuwa your enemies, nlikua nadhan sitoweza pata hao adui lakin yule ambae sijamtegemea ndio kawa adui eti
 
Hivi kwanini lazima rafiki yako/zako baadae wageuke kuwa your enemies, nlikua nadhan sitoweza pata hao adui lakin yule ambae sijamtegemea ndio kawa adui eti
Ukweli ni kuwa anakuwa sio rafiki anakuwa ni mtu mwenye wivu na wewe ila amepata hifadhi ya ukaribu na wewe, au yupo karibu kwa sababu kuna unafuu unaupata kwako au kampani,
 
ukweli ni kuwa anakuwa sio rafiki anakuwa ni mtu mwenye wivu na wewe ila amepata hifadhi ya ukaribu na wewe, au yupo karibu kwa sababu kuna unafuu unaupata kwako au kampani,

Game of Thrones ina maneno mazito sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…