Nimegundua namna ya kufanya mvua inyeshe

Nimegundua namna ya kufanya mvua inyeshe

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Leo ni mara ya 6, kila nikiosha kigari changu jioni usiku au asubuhi sana mvua itanyesha. Mpaka naanza kuwaza au huyu jirani yangu ananifanyia hujuma?

Maana huu mtaa mzima mimi ndio nina gari kali, tena ya miaka ya hivi karibuni tu; ni Toyota Corolla ya mwaka 1986 kama imetoka Japan jana tu. Watu wengi hata hawaifahamu hii gari, ni very unique.

Nimehesabu mara ya 6 leo, jana nimeosha gari vizuri sana nikalikausha nikalipaka na tumafuta kidogo ling'ae. Tena wife akasema umeosha hivyo sijui kama mvua haitanyesha. Leo tumeamka mvua inakazana kweli kweli.

Sasa hapa nimegundua namna ya kuleta mvua. Nadhani kama si jirani yangu basi kuna namna tu kuosha kwangu gari kunavutia mvua. Naweza amua kwenda kijijini mbwinde nikawa nafanya hii shughuli ya kuvutia mvua.

Maana mtu unawaza mara 6 zote itakuwa coincidence? Hapana, kuna kitu.
 
GARI YA MWAKA 1986 NA MTAANI KWAKO WEWE NDO MWENYE GARI🤔🤔🤔

NGACHOKA KABISA
 
Hiyo hiyo ni kigari lakini pia gari kali!!!
 
Naona upo hatua za awali kuwa mchawi wa mvua, upigwe na radi Sasa😂
 
Hongera!!Umefanikiwa kutufahamisha ya kwamba,,umebahatika na wewe kumiliki gari!!
 
Back
Top Bottom