Nimegundua pia hata Nyama ya Ngamia ni Kharamu...

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Nlikuwa nasoma Taurati/Torati. Ngamia pia ni Kharamu.... Anacheua lakini hana kwato. Ndiyo kwa mujibu wa Taurati mimi huwa nasoma vitabu hata vya watu wa Kitabu.

Hadithi na Mtume na Maswahiba wake nasoma. Biblia nasoma na napendelea sana Taurati... Kumbe Ngamia hana sifa za kuliwa. Kama Sungura,Kama Kambale kama Pweza. Pweza na Kambale hawa hawana Magamba. Ni kharamu.

Na nyama ya Nguruwe tunaruhusiwa kula pale tuna njaa na hakuna chakula kingine hapo karibu. Ila si mara kwa mara. No. Shida ya nguruwe ni kuwa ana kwato zilizochanywa ila hacheui. Hapo ndo shida. Lakini pia huwa anaoga matope. Hapo pia sasa naanza kuona hata Bata naye ana hizo tabia.

Anyway.... Naendelea kujifunza. Na pia nikawa nasoma vitabu vya Dini za kiafrika nako nikajifunza kuwa wamama wajawazito ni kharamu kula mayai, na pia kwa mujibu wao hata Albino kwao ni tatizo pia.

So naendelea kujifunza ndugu zanguni huku nikipata muda wa kutumia akili kutafakari. Nawaza pengine naweza kuna anzisha Dini yangu kutoka katika hizi Dinis zote zilizopo. Karibuni tushirikiane.

Wabillah Tawfiq.
 
Msipende kuongelea masiala ya kisharia na kielimu haliyakuwa hiyo elimu yenyewe hatuna....pia kamwe usitegemee kuyajua masiala ya kisharia(elimu) kihakika yake jamiiforums
 
Masiala ni nini? JF TUNAONGELEA LOLOTE LILE HAKUNA KUTISHANA. HATA WEWE HUJUI SUBIRI WAJE WAKUFUNDISHE WANAOJUA.
 
Google camel toe na kisha uende kwenye images kuweza kujua kwato za ngamia zipoje
You may eat any animal that has a split hoof completely divided and that chews the cud. "`There are some that only chew the cud or only have a split hoof, but you must not eat them. The camel, though it chews the cud, does not have a split hoof; it is ceremonially unclean for you

i believe you understand this kafirs' language.
 
uislamu hakuna sehemu imesema ule nyama ya nguruwe unapokosa chakula ni uongo mkubwa
 
Ni uhuni tu kikundi cha watu kukaa na kuanza kusema usile hiki usile kile ni haramu huku wao wakiwa mstari wa mbele kuzini,kusengenya dhulma kwa mayatima na mali za jamii zaka hawatoi wakitoa wanajionyesha etc.

Kila mtu aachwe ale anachojisikia kama sumu kitamdhuru yeye kama dhambi ataulizwa yeye hiyo kuanza kupangiana mtu ale nini asile nini ni uhuni kama uhuni mwengine tu.
 
uislamu hakuna sehemu imesema ule nyama ya nguruwe unapokosa chakula ni uongo mkubwa
Quran 2:173 na Quran 6:145 , inasema kura ukila NGURUWE kama sehemu hiyo uliopo haina chakula cha mbadala basi Sio dhambi ,
 
Ulisha fuatilia ukajua huyo [emoji247] ana matumbo mangapi? Au unakurupuka!.
 
Kwanini mnapenda kuyafanya maisha ya duniani hapa yawe magumu?
 
Mbona mbususu mnazishambulia, vyakula ndio mnaona dhambi, sasa wewe kama unakula mbususu haujafunga ndoa si bora hata mla kitimoto kilo rosti, ndizi mbili na pilipili, pembeni ana guiness stout ya bariidiii....
 
You may eat any animal that has a split hoof completely divided and that chews the cud. "`There are some that only chew the cud or only have a split hoof, but you must not eat them. The camel, though it chews the cud, does not have a split hoof; it is ceremonially unclean for you

i believe you understand this kafirs' language.
Hivi kucheua na kupasuka kwato kunasababisha vipi mnyama kuwa safi kwa kula na kutopasuka kwato kunasababishaje mnyama huyo kuwa najisi?
1671235841529.png
 
Nlikuwa nasoma Taurati/Torati. Ngamia pia ni Kharamu.... Anacheua lakini hana kwato. Ndiyo kwa mujibu wa Taurati mimi huwa nasoma vitabu hata vya watu wa Kitabu.

Hadithi na Mtume na Maswahiba wake nasoma. Biblia nasoma na napendelea sana Taurati... Kumbe Ngamia hana sifa za kuliwa. Kama Sungura,Kama Kambale kama Pweza. Pweza na Kambale hawa hawana Magamba. Ni kharamu.

Na nyama ya Nguruwe tunaruhusiwa kula pale tuna njaa na hakuna chakula kingine hapo karibu. Ila si mara kwa mara. No. Shida ya nguruwe ni kuwa ana kwato zilizochanywa ila hacheui. Hapo ndo shida. Lakini pia huwa anaoga matope. Hapo pia sasa naanza kuona hata Bata naye ana hizo tabia.

Anyway.... Naendelea kujifunza. Na pia nikawa nasoma vitabu vya Dini za kiafrika nako nikajifunza kuwa wamama wajawazito ni kharamu kula mayai, na pia kwa mujibu wao hata Albino kwao ni tatizo pia.

So naendelea kujifunza ndugu zanguni huku nikipata muda wa kutumia akili kutafakari. Nawaza pengine naweza kuna anzisha Dini yangu kutoka katika hizi Dinis zote zilizopo. Karibuni tushirikiane.

Wabillah Tawfiq.
Umegundua uongo. Ngamia ni halali kuliwa kwa sheria ya Kiislamu
 
Back
Top Bottom