Wazolee
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 3,183
- 3,660
Leo mida ya saa 5 asubuhi nilikuwa maeneo ya airport nimeona bonge la dege linatua yana mle wenye corona hawakosekani
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Eti eeh? 🙄Corona will not affect tanzania...
Neither cause a big tragedy like other European countries..
Do u know why?
Africans have a lot of problems more than corona.
Hapa kweti kuna hotel ya US$50 kulingana na clip ya yule mama aliyekuwa analalamika.Kwa kujibu wa taarifa kwenye hiyo link, Kenya wanapewa alternative, (hadi hostel za chuo zinatumika). Na hata hiyo hotel aghali iliyotajwa rate yake ni US$ 60 ambayo ni chini ya laki mbili inayotozwa hapa kwetu.
Mi nawaza tu,ule alioufanya Makonda pale ubungo si mkusanyiko?Hivi tuko serious kweli au?Kuna jambo gani la maana ameenda kulifanya pale?shame
Hivi Tanzania wakiweka karantii ya kutoka kama hizo nchi nyingine si watu wengi watakufa kwa kukosa chakula kuliko hata vifo vya corona yenyewe? Tusijifananishe na nchi hizo. Maisha ya Bongo asilimia kubwa fedha ya kula kesho inatafutwa leo na wakati mwingine ya kula leo inatafutwa leo leo. Utamwambia mtu asiyejua anakula nini kujifungia ndani?Vita ya corona Tz
Sasa kipi kifanyike au tukae lockdown mwez1 tupime upepo.
Hivi Tanzania wakiweka karantii ya kutoka kama hizo nchi nyingine si watu wengi watakufa kwa kukosa chakula kuliko hata vifo vya corona yenyewe? Tusijifananishe na nchi hizo. Maisha ya Bongo asilimia kubwa fedha ya kula kesho inatafutwa leo na wakati mwingine ya kula leo inatafutwa leo leo. Utamwambia mtu asiyejua anakula nini kujifungia ndani?
Hivi Tanzania wakiweka karantii ya kutoka kama hizo nchi nyingine si watu wengi watakufa kwa kukosa chakula kuliko hata vifo vya corona yenyewe? Tusijifananishe na nchi hizo. Maisha ya Bongo asilimia kubwa fedha ya kula kesho inatafutwa leo na wakati mwingine ya kula leo inatafutwa leo leo. Utamwambia mtu asiyejua anakula nini kujifungia ndani?
Lawama kwa serikali…lawama kwa serikali…lawama kwa serikali!Kwakweli serikali ya Tanzania imelichukilia janga la COVID-19 kama jambo la mzaha kupita kiasi, hali hii imewafanya baadhi ya wananchi kubweteka kupita kiasi kutokana na janga hili.
Kwa haya niliyoshuhudia, nachelea kusema kuwa ikitokea COVID-19 ikaiathiri Tanzania kwa kiwango kikubwa basi mataifa mengine yataandika nne na kutucheka kwa kejeli. Haya yanasababishwa kwa kiwango chote na viongozi wetu wa serikali tuliowapa mamlaka ya kutuongoza. Nitaainisha uzembe huu uliopindukia katika maeneo machache.
1. Ni jambo la aibu sana baadhi ya raia wa Tanzania kuvuka mpaka wa Tanzania na Uganda na kisha kukamatwa ndani ya Uganda wakati kila nchi inalichukulia jambo hili kwa uzito wa aina yake labda isipokuwa Tanzania. Ni jambo la aibu kwa sisi kutumia uzembe wetu na kutokujua mambo kupeleka mzigo kwa wenzetu, kwa hili najisikia aibu sana kama Mtanzania.
Kwa jambo kama hili Uganda watatuona sisi kama watu wa mzaha sana kiasi kwamba mzaha wetu tunaupeleka hadi kwenye nchi za wenzetu ambazo kwa namna ya kipekee wamelichukulia jambo hili kwa umuhimu na ukubwa wa kiwango chake. Kwanini mamlaka za Tanzania mipakani hazikuwazuia watu hawa hadi wakavuka mpaka kati ya Uganda na Tanzania? Hawakuona umuhimu wa kuwaheshimu wenzetu walioamua kufunga mipaka yao ili kuikabili Corona kwa vitendo?
2. Hoteli zetu kutoza kiwango cha chini cha Tshs laki 2 kwa watakaojiweka karantini kwa siku moja pekee. Hili ni jambo la aibu sana kwetu kama nchi. Kwa wenzetu jambo hili limeihusisha jamii yote huku Rais wa nchi akiwa kamanda mkuu wa kikosi pambanaji. Hapa kwetu hakuna control yoyote juu ya jambo hili iliyoandaliwa hadi pale walipogutuka baada ya watu kulalamika.
Hili ni jambo la aibu na fedheha kubwa. Nimejiuliza, hata kwa hili hawakujiandaa? Yani mtu mwenye matatizo ambapo imembidi kuwekwa ama kujiweka pale ili kuwanusuru wengine anaenda kutozwa hela ya malazi ya anasa? What a shame! Mbaya zaidi kamanda mkuu yupo Dodoma anapiga picha akiwa amelala juu ya jiwe! Huu ni mzaha na kuwachukulia watu wako "Too low"
3. Utolewaji wa taarifa za mara kwa mara na kuwekeza nguvu kwenye vituo vya kupimia ugonjwa huu pamoja na kuwekeza nguvu kwenye kudhibiti usambaaji. Ni aibu kubwa kuwa Rais kasema kuwa anapeleka fedha za Mwenge kwenye kupambana na ugonjwa huu ila hakuna lolote kuhusu kupambana huko. Vituo vya usafiri wa umma, mahospitali mengi hakuna viosha mikono, hakuna kupulizia dawa.
Yani tupo kila mtu na lake. Mbaya zaidi hakuna taarifa za mara kwa mara kutoka kwa wahusika wa kutoa taarifa. Yani kwa kifupi ni kama serikali imelala kupita kiasi! Ni aibu eti sampuli zote ndani ya nchi zinapelekwa kituo kimoja pekee cha kupimia. Hatuoni kuwa tutakuwa tunachelewesha kuwabaini waathirika kwa haraka? Hatuoni madhara haya ya ucheleweshaji mpaka sasa?
4. Swala la mkuu wa mkoa wa Dar kutoka asubuhi asubuhi na kupeleka ujumbe kwa watu kuwa kuna mtoto wa Mbowe anaugua Corona. Ukiusoma uso wa Paul Makonda ni kama amepata "relief" fulani kwa mtoto wa Mbowe kuumwa ugonjwa tena kwake furaha zaidi ni Corona. Hakuna kiongozi hata mmoja aliyekosoa ujinga huu! Tunaanzaje kuwaamini kuwa mpo serious? Alichofanya Paul Makonda ni utoto mtupu na kwa alichofanya hakutakiwa kuendelea kuwa kiongozi. Lakini kwakuwa tayari kuna udhaifu, basi limeonekana ni jambo la kawaida kabisa kwa viongozi wa kitaifa wenye dhamana.
5. Hakuna uhamasishaji kwa watu wenye uwezo kujitoa ili jamii nzima iwe salama. Hili kimsingi linatakiwa kufanywa na serikali. Lakini kwakuwa hakuna kujali basi na wao wameamua kujikalia kimya tuu ili mradi liende huko litakakotua.
Mwisho naomba nieleze masikitiko yangu kuwa kwa hili jambo basi ni hatuna serikali makini. Pia ni heri watu wakajichukulia tahadhari wenyewe na pengine wanayoambiwa na serikali ya Tanzania basi wachanganye na zao! Hakuna uaminifu kwa kiwango kikubwa mno kutoka serikalini kuhusu janga hili la COVID-19.
Lawama kwa serikali…lawama kwa serikali…lawama kwa serikali!
Ni wajibu wa kila mtz kujikinga na ugonjwa huu na magonjwa mengine! Kama unasubiri serikali ije ikukinge baada ya kutoa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa huu nchini basi utasubiri sana! Kwa maoni yangu serikali inafanya kinachotakiwa. Imetoa elimu, imefunga shule na vyuo na kuzuia mikusanyiko! haya yanapaswa yapige kengere kwenye masikio ya kila mtz maana siyo mambo ya kawaida kutokea! Unapoona mpaka serikali imechukua hatua hizo ujue imechukulia covd-19 kwa uzito unaostahili!
Na tz kihihivi tutavuka salama na mataifa mengine yatashangaa, Mungu yupo!
Rwanda ni nchi yenye population ndogo sana / Hiko kama watu awazidi 10 Million.... Usijaribu sumu kwa kuionja.
Issue ya Corona kwann yeye aingize siasaLengo la hii mada ni hapo namba 4 tu
Mi nawaza tu,ule alioufanya Makonda pale ubungo si mkusanyiko?Hivi tuko serious kweli au?Kuna jambo gani la maana ameenda kulifanya pale?shame
Huyu jamaa ana ujumbe wa maana ila jinsi ya kuutoa ndipo kachemsha. Ukiwa ni mtu wa mrengo fulani na unajulikana, ni vyema kuhakikisha huongelei cheap politics kam kupiga picha juu ya jiwe. Bashite kutamka kuwa fulani ana.... mihemko inapozidi hata umahiri wa uandishi unakuwa shakani. Ni maoni yangu tuLengo la hii mada ni hapo namba 4 tu
Issue ya korona ni ya kisiasa mkuu, kwani huoni namna marekani anavyopambana na mshindani wake ?? wakitupiana mpira kuwa nani kauleta huu ugonjwa??Issue ya Corona kwann yeye aingize siasa
Hebu msikilize mtaalam huyu watu wenye fani zao, ukweli ndiyo huu
Ova
View attachment 1398555
Sent using Jamii Forums mobile app
Taf.Tuwekeeni hiyo clip nasi tumshangae.Mi nawaza tu,ule alioufanya Makonda pale ubungo si mkusanyiko?Hivi tuko serious kweli au?Kuna jambo gani la maana ameenda kulifanya pale?shame