Nimegundua wana Jf wengi si wakweli kama mimi

Nimegundua wana Jf wengi si wakweli kama mimi

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
Habari zenu wakuu
Hayawi hayawi sasa yamekuwa,

Ivi mbona kila mtu nikiangalia Post zake naona kama hakuna wenzangu humu?

Yaani kila mtu utaskia "nilienda na gari sehemu fualani...

Mara mwingine utasikia "tulikutana ATM

Mwinge utasikia "kipindi nipo chuo kikuu nilifanya hivi...

Mara mwingine nae "Nilikuwa hotelin...

Bila kusahau mwingine nae "Nilikutana nae airpot.

Wengine nao "Nimeibiwa Dukani..
na mengine mengi

Jamani Sasa huu mgogoro wa nafsi inabidi leo niutoe
jamani yaani inamaana huku Jf mimi tu ndio muuza maji?

Mbona sijawahi kukutana na wenzangu tunaoenda kuwachek madem kwa baiskel na kuwapakiza?

Jamn mbona sisi tunaosafisha vyoo humu hatupo?

Jamani hata wenzangu tunao tunatembeza mihogo humu hatumo,

Sawa!

Swali jingine jamn inamaana humu Jf mimi tu ndio nimeishia form Two?..

Haya bora mi nilikimbia phiziksi kidato cha pili[emoji23] [emoji125] [emoji125]
Jamani ila mbona kuna wengine walipata ziro form four kwani humu hawafiki?

Mmmmh Hapana jaman mi nimechoka kuwa kenge kwenye msafara wa mamba...

Ndugu zangu wanazungumzia mambo ya hela afu mimi mwenyewe mfukoni sina hata jero jaman kweli?

Mungu anawaona nyie wote mnaodanganya Umma.[emoji23] [emoji23]
 
Ulichosema ni chakweli kabisa japo kama ujafikiria kwa makini utaona kama makuzi, ni kweli kabisa wana jf wengi kwa mada zao yani ni watu wamipango mikubwa mikubwa tu ukiwafuatilia yaani mtoa mada upo akilini mwangu kabisa
 
Ulichosema ni chakweli kabisa japo kama ujafiria kwa makini utaona kama makuzi, ni kweli kabisa wana jf wengi kwa mada zao yani ni watu wamipango mikubwa mikubwa tu ukiwafuatilia yaani mtoa mada upo akilini mwangu kabisa
Hahahaaa mkuu hapa ikiona mtu anatoa povu ujue limemgusa [emoji23] [emoji23] [emoji125]
 
Maisha unayo yaota wewe, upande wa pili kunamtu anayaishi, ichukulie kama changamoto ikupe hali ya kupambana ili “siku moja tuje salimiana sheli kwa milio ya honi”
 
Back
Top Bottom