gfsonwin, binafsi nakushauri hiyo J4 uende kama alivyokuahidi. Ukikuta ameishaifanyia kazi poa shida yako imeisha, ukikuta hajaifanyia kazi atakwambia sababu, ukiona sababu ni kwamba mpake umvulie chupi wewe mwambie tu kwa lugha nzuri kwamba kama ni hivyo acha nitatafuta haki yangu ngazi za juu. Ukishamwambia hivyo we ondoka zako. Then, baada kama ya wiki 1 au 2 hata 3 nenda tena bila hata ya appointment ukamuulizie kama ameishaifanyia kazi. Ukikuta bado njoo tena tukupe mawazo.
Ila siku zote kumbuka haki ya mtu haipotei ila inacheleweshwa tu. Hiyo miezi sita uliyokaa bila kupata mshahara mpya si muda mrefu kwenye serikali yetu. Nafahamu watu waliokaa mwaka na zaidi, tena wengine hadi wanastaafu hawajalipwa mshahara mpya, lakini mwisho wa siku wanalipwa. Kwahiyo don't be desperate coz of six months length.
Halafu dada yangu kama walivyokushauri baadhi ya watu, vita ya kupinga rushwa ya ngono maofisini linahitaji kujitoa muhanga. Ndo maana nilikushauri uwe ngangari kweli kweli, ukilegea tu utakuwa pozeo la kila boss. Huna haja ya kujilaumu kuumbwa mwanamke, tena inabidi uringie uwanamke wako badala ya kuwaza na kumlaumu Mwenyezi Mungu kwa kukuumba hivyo ulivyo.
Take this from me: mwanaume yeyote rijali hasa mwafrika, akisha kuwa na uwezo fulani (fedha, madaraka, elimu, mali, umaarufu n.k) halafu hana roho wa Bwana (yaani he is not committed to God), there is no way ataepuka uzinzi hata kama ameoa! Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba ni wanaume (of course na wanawake pia) wachache wana roho wa Mungu. Fanya utafiti wako utagundua nilichokiongea hapa ni sahihi. Sasa ukishalikubali hilo basi huna haya ya kusikitika na kukuona unadhalilishwa. Mwisho wake utashindwa kufurahia maisha bure kwa sababu ya kutongozwa na wanaume.
Tena kama umefuatilia kila comments kuna baadhi wamekwambia wazi kwamba mwanamke kutongozwa ni kitu cha kawaida, ni wewe tu na akili yako kichwani. Hii kauli inatokana na ukweli niliousema hapo juu kwamba watu wengi hawana roho wa Bwana, wanasukumwa na tamaa zao za mwili ndo maana akimuona mwanamke cha kwanza anaanza ku-imagine akiwa mtupu je! matokeo yake ndo hii tabia ya kutongoza tongoza kwa kwenda mbele. Na ukijilegeza anakula kweli, ukipata maradhi shauri yako, ukiharibu ndo yako shauri yako, ukijidhalilisha ktk jamii shauri yako ili mradi yeye alishapata alichokuwa akihitaji!
Kwahiyo we dada yangu hii tabia ya wanaume ya kupenda kutongoza tongozwa ichukulie poa tu, otherwise itakumbua bure akilini mwako wakati huna uwezo wa kuwabadilisha. Tena usipoangalia utaanza kuwachukia wanaume karibu wote. Sasa sijui utaenda kuishi wapi ambako hakuna wanaume! Tena huna haja ya kuwakwepa, just interact with them, wakichenji mada, you stick to your big NO, tena wakishakujua utabaki uhusiano wa kaka, dada, shem na maheshima kibao!