strong lady
Member
- May 19, 2012
- 37
- 14
Issue niliyoiona hapo siyo kutongozwa bali mazingira ya utongizwaji. Yaani mtu unakwenda kwa dokta una shida akutongoze huwezi kujisikia vizuri. Ila kama mmekutana kitaa na mtu akapagawa hakuna shobo hapo.
Pole.....ila siku ingine uwe unamwambia hapo hapo ili ajifunze sio kwako tu na kwa wengine pia......kama wewe leo umeweza kumuepuka kesho atakuja mwingine atashindwa kumuepuka......ukiweza mrudie ukampe makavu live ili akome na akomae.....pole kwa kuharibu siku.
ahsante sana sweetlady.
sasa hapa tatizo ni kwamba hata kumpaka live siwez manake bado hajasaini barua zangu. na tatizo la huku kwenye halmashauri ni kwamba mabosi wanateteana sana. yaani natamani niamke j4 niambiwe kafariki ili niwe na amani mambo yangu yaende mbele................ hawa wanaume ni waonevu sana sijui kweli kama ukombozi wa mwanamke utakuja tutasubiri miaka elfu
huo mgongo kwenye avatar unanitempt nimcheat waifu ndani ya wiki. Mboga moja inachosha banahahahahahaaaz loh
sweetlady labda sijui nijaribu kupata msaada wa kisheria zaidi baada ya hiyo j4 naliyosema niende. But nmeumia sana kumbe ukiwa ke hata kama ni haki yako huwez pewa hadi umvulie mtu chupi? kweli kweli haya ndo maisha yetu lol...........sitaki hata kuamini. naumia sana halafu natumika kwa mshahara wa daraja la chini japo cheo nilipandishwa miez sita iliyopita..........yani naumia sana manake akichelewesha nitaanza kulipwa huu mshahara mpya mwaka kesho sasa na areazi mwaka 2015 hii ndo tz. Mungu auwe wote wa staili hiiDaaah!!!!!!...pole tena gfsonwin manake inaonekana kweli umekereka mpaka unamuombea kifo lol....na kwa taarifa yako watu kama hao ndo hawakufagi ng'oooo......wanakufa wale wazuri wenye utu wao......ila nna hakika lazima atakusainia sema kwa kukuchelewesha ......itabidi umvumilie tu au jaribu kutafuta ushauri na kwa watu wengine ....ikibidi kumshtaki fanya hivyo upesi!
Mijitu kama hiyo mnatakiwa museme majina yao kwani hawastahili heshima hata kidogo. Imezoea rushwa ya ngono hata pale unapokuwa una haki ya wazi. Ungempiga kelbu cha dharau!!!
mito muda mwingine napatwa na uchungu wa haya maisha na kauli zako kuwa ndio marupurupu yao nazidi kuumia zaid. Tatizo mimi huwa nu mtu wa kulia sana nikikwazika nashindwa kuvumilia naanza kualia. Yaani sijui kama hiyo j4 hajanisainia nitafanyaje manake nitajikuta nalia tu. Sipendagi mateso au kitu kinachoumiza mwenzenu. sijui nimeumbwaje.
sasa wewe kama haja saini hadi j4 nifanyeje niondoke tu pasi kumuuliza? au niache kwenda hadi muda upite achoke aamue kusaini? na ataamua lini? nisaidie kaka yangu mpendwa.
Ngekewa nimemchukia kwa kua najua mwishowe ni kutumia cheo chake kinaniumiza. asipo sain barua zangu nabaki na cheo kikubwa mshahara wa cheo cha chini
GALIMA nimewaza mengi sana leo, penyewe hapo mimi ni mwl, na yapata miezi kama sita hivi sijaongezewa salry licha ya kuandika barua zisizo pungua 4. leo nakwenda ili kujua status nakutana na haya sasa kweli hii haki yangu nitaipata au ndo niache tu.
Hivi kwani wenzangu huwa wanafanyeje wnapokutana na hali hii katik ofisi zao? nilihofia kumtusi asije sema nina nidhamu mbaya nikashangaa na kazi yenyewe nimesimamishwa.
Teamo wewe kaa pembeni kwanza au nipe maujanja ya kumuweza huyu bosi manake mwenzio snalipwa mshahara wa cheo cha nyuma kwa miezi sita sasa.
mito muda mwingine napatwa na uchungu wa haya maisha na kauli zako kuwa ndio marupurupu yao nazidi kuumia zaid. Tatizo mimi huwa nu mtu wa kulia sana nikikwazika nashindwa kuvumilia naanza kualia. Yaani sijui kama hiyo j4 hajanisainia nitafanyaje manake nitajikuta nalia tu. Sipendagi mateso au kitu kinachoumiza mwenzenu. sijui nimeumbwaje.
sasa wewe kama haja saini hadi j4 nifanyeje niondoke tu pasi kumuuliza? au niache kwenda hadi muda upite achoke aamue kusaini? na ataamua lini? nisaidie kaka yangu mpendwa.
kwakweli akiendelea kuniudhi nitamtaja hapa jamvini na hata takukuru manake naona tunaekeana usiku.
wana jf leo yamenikuta mwenzenu.
Jamani leo nimejikuta naharibiwa siku yangu na katibu tawala wilaya ya ...................... baada ya kurusha ndoana yake kwangu leo ofisi kwake. Loh nimekasirika sana.
nilikwenda huko baada ya kuwa nilihitajika kusainiwa barua zangu za job kama ujuavyo adha za waalim ukipandishwa cheo hadi uanze kupokea mshahara mpya ni ishu.
Jamani hivi ninyi wanaume mna nini? kwanini hamuheshimu hizo ofisi tena za umma? kwanini pia mnapenda kudhalilisha wanawake? au mnataka hadi tuekeane bifu kwa kuwaitieni takukuru?
Jitu lenyewe tumbo lipo kama anakunya humo humo mod nisamehe ni hasira tu. ila kaniboa sana. Na ukweli wanawake tunadhalilishwa sana.
Kwa kweli hizi coments zako zimenitia uchungu sana.
Mungu atakusaidia mpendwa gfsonwin upate haki yako.
Ila ukienda hiyo j4 ukakuta upuuzi usimuoneshe machozi atakuona mdhaifu.
Muombe Mungu akupe ujasiri,usijute kuumbwa mwanamke wala kamwe usiamini kuwa tumeumbwa kufanyiwa hivi.
Twende PM tupeane mbinu za kumkomesha afisa huyu,ila ukiwa wakulia lia hutamuweza huyu baba.
Huyu ni rahisi sana kumtia tumbo joto tatizo wewe unavyoongea inaonesha unaamni yeye ndiye mwenye power za wewe kufanikiwa au usifanikiwe.Yeye ameajiriwa tu kama wewe na asipofuata maadili ya kazi anaweza kupoteza ajira vile vile hicho kiti wakakalia wengine.
Nitakuweka katika maombi naona unahitaji faraja.
Tatizo wanawake wenzenu wanawaangusha wanakuwa weak sana pale wapatwapo shida au msaada wanaliwa ovyo na kutengeneza kuwa ni desturi kuliwa ili upate msaada.WANAWAKE WOTE WANGEKUWA KAMA WEWE TABIA HII INGEKUFA HOngera kwa ujasiri wako dia
gfsonwin, binafsi nakushauri hiyo J4 uende kama alivyokuahidi. Ukikuta ameishaifanyia kazi poa shida yako imeisha, ukikuta hajaifanyia kazi atakwambia sababu, ukiona sababu ni kwamba mpake umvulie chupi wewe mwambie tu kwa lugha nzuri kwamba kama ni hivyo acha nitatafuta haki yangu ngazi za juu. Ukishamwambia hivyo we ondoka zako. Then, baada kama ya wiki 1 au 2 hata 3 nenda tena bila hata ya appointment ukamuulizie kama ameishaifanyia kazi. Ukikuta bado njoo tena tukupe mawazo.
Ila siku zote kumbuka haki ya mtu haipotei ila inacheleweshwa tu. Hiyo miezi sita uliyokaa bila kupata mshahara mpya si muda mrefu kwenye serikali yetu. Nafahamu watu waliokaa mwaka na zaidi, tena wengine hadi wanastaafu hawajalipwa mshahara mpya, lakini mwisho wa siku wanalipwa. Kwahiyo don't be desperate coz of six months length.
Halafu dada yangu kama walivyokushauri baadhi ya watu, vita ya kupinga rushwa ya ngono maofisini linahitaji kujitoa muhanga. Ndo maana nilikushauri uwe ngangari kweli kweli, ukilegea tu utakuwa pozeo la kila boss. Huna haja ya kujilaumu kuumbwa mwanamke, tena inabidi uringie uwanamke wako badala ya kuwaza na kumlaumu Mwenyezi Mungu kwa kukuumba hivyo ulivyo.
Take this from me: mwanaume yeyote rijali hasa mwafrika, akisha kuwa na uwezo fulani (fedha, madaraka, elimu, mali, umaarufu n.k) halafu hana roho wa Bwana (yaani he is not committed to God), there is no way ataepuka uzinzi hata kama ameoa! Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba ni wanaume (of course na wanawake pia) wachache wana roho wa Mungu. Fanya utafiti wako utagundua nilichokiongea hapa ni sahihi. Sasa ukishalikubali hilo basi huna haya ya kusikitika na kukuona unadhalilishwa. Mwisho wake utashindwa kufurahia maisha bure kwa sababu ya kutongozwa na wanaume.
Tena kama umefuatilia kila comments kuna baadhi wamekwambia wazi kwamba mwanamke kutongozwa ni kitu cha kawaida, ni wewe tu na akili yako kichwani. Hii kauli inatokana na ukweli niliousema hapo juu kwamba watu wengi hawana roho wa Bwana, wanasukumwa na tamaa zao za mwili ndo maana akimuona mwanamke cha kwanza anaanza ku-imagine akiwa mtupu je! matokeo yake ndo hii tabia ya kutongoza tongoza kwa kwenda mbele. Na ukijilegeza anakula kweli, ukipata maradhi shauri yako, ukiharibu ndo yako shauri yako, ukijidhalilisha ktk jamii shauri yako ili mradi yeye alishapata alichokuwa akihitaji!
Kwahiyo we dada yangu hii tabia ya wanaume ya kupenda kutongoza tongozwa ichukulie poa tu, otherwise itakumbua bure akilini mwako wakati huna uwezo wa kuwabadilisha. Tena usipoangalia utaanza kuwachukia wanaume karibu wote. Sasa sijui utaenda kuishi wapi ambako hakuna wanaume! Tena huna haja ya kuwakwepa, just interact with them, wakichenji mada, you stick to your big NO, tena wakishakujua utabaki uhusiano wa kaka, dada, shem na maheshima kibao!