Nimeharibiwa week-end yangu.... lol!

Nimeharibiwa week-end yangu.... lol!

Pole mwenzangu pamoja na elimu yako jambo dogo lakushinda. Mie nilibambikiwa kesi na jamaa yangu Wa karibu kisa wivu Wa kibiashara. Akaenda kunifungulia kesi eti ni mmemtukana matusi na nimmemtishia kumtoa roho.
Kwenda polisi kachukua maelezo yangu mda wote huu, nimewasha iPhone yangu na chukua video taratibu Hana habari. Wazo langu ni kuwa akiteleza kutaka Rushwa ili asiniweke lockup, niwe na ushahidi.
Mwisho Wa siku Ana niuliza je umekuja na wadhamini maana ina bidi nikueke ndani ilikuwa ijumaa ili jumatatu nikupeleke mahakamani.
Ni kwamwambia nitajidhamini akakataa kwa sababu ya hasira ni kasema poa ni weke ndani hadi jumatatu.
Gafla si akatamka SIKILIZA RAFIKI MIMI NIKOTAYARI KUKUSAIDIA JE WEWE UTANISAIDIAJE. NIKAMWAMBIA WE NIPE TERMS. NIPE KITU KIDOGO RAFIKI KUMBUKA LEO IJUMAA UTAPATA SHIDA. JE ULITAKA KIASI GANI? KADAI LAKI MOJA NIKAMWAMBIA POA. Baada ya hapo banduku nikazima kamera. Nikaplay ile video na kuongeza sauti akawa anajisikia sauti yake akastuka vipi ni MIMI HUYO! Nikamwambia ndio subiri usikilize hadi mwisho. Ilivyokuja issue ya kuomba hela si aka shangaa Kama vile kapigwa shock ya Umeme.
Akanisihi nifute na pili niondoke nisije mwaribia kazi.
Sasa jamaa yangu akaenda jumatatu kujua kilicho jiri jamaa kamfokea anadai umeniletea mashushu waje ni haribia kazi hebu achana na Mimi.
HUO UKAWA MWISHO WA KESI YANGU.

sasa hapo siunona ww ulikuwa na ipod hapo, haya mimi nina kicm changu tu na pia nkitaka hata kurekodi sauti hakina namna labda nitafute iyo j4 niende nayo, niiweke on kabisa. umenipa akili pia.
 
Sasa hii ndio yamekukuta?..... JF bana!

Mwenzio juzi kabakwa bila kondom bahati nzuri yeye ndio alikuwa na HIV, wabakaji karibuni wataanza kuishi kwa matumaini. kulaleki!


Heheheh klorokwini bana....
 
Dah,Hongera sana ,umeshinda vishawishim,tehe
 
sweetlady labda sijui nijaribu kupata msaada wa kisheria zaidi baada ya hiyo j4 naliyosema niende. But nmeumia sana kumbe ukiwa ke hata kama ni haki yako huwez pewa hadi umvulie mtu chupi? kweli kweli haya ndo maisha yetu lol...........sitaki hata kuamini. naumia sana halafu natumika kwa mshahara wa daraja la chini japo cheo nilipandishwa miez sita iliyopita..........yani naumia sana manake akichelewesha nitaanza kulipwa huu mshahara mpya mwaka kesho sasa na areazi mwaka 2015 hii ndo tz. Mungu auwe wote wa staili hii

Pole sana mpendwa......mie pia sijui mambo ya sheria labda kama kuna mwana jf anaweza kukusaidia kwa hili atakusaidia.....nenda hiyo j4 huku umeweka thura ya kazi labda ataogopa kukugusia tena lol....
 
Pole sana Dear, Wewe nenda kama alivyokuagiza J4, Nadhani na yeye ni muelewa. Alivyokutongoza alijaribu tu. Anajua kutongoza kuna kukubaliwa au kukataliwa. Sasa inategemea ulimkatalia kwa mazingira gani. Mtu Anayekutongoza usimuone adui, mjibu tu kwa uzuri. Hata yeye angejua kama ungemkatalia asingekutongoza. Hivi kwa mfano angekuvutia ukamkubali ungekuja kumuanika humu. Maana umeanza kwa kumkashifu kuhusu tumbo lake lilivyokubwa, mpaka nikapata wasiwasi kwamba tumbo ndilo lililompoza, angekuwa na tumbo dogo pengine ungemkubali. Hata hivyo nakupa pole.
 
bado muda mchache tu kufika j4.... ngoja tusubiri mpambano tuone kama itavuka au haivuki...
 
Back
Top Bottom