Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Uchawi ungekuwepo:-

Wakoloni wasingewanyanyasa Babu zetu kiasi kile mpaka wanaume wanne wakiwa nusu uchi wanambeba mwanaume mmoja wa kizungu juu kuanzia Kigoma mpaka Kilimanjaro

Wasingechapwa mijeledi kiasi kile na waarabu

Wanaume wa kinijeria wasingechukuliwa watumwa na kupelekwa America kutumikishwa wazee wao waangalie tu

Timu za Simba na Yanga zingekuwa club bingwa za dunia

Wachezaji wa kibongo wangechezea Barca, Real Madrid, Liverpool etc

Mwisho kabisa hao wachawi wenyewe wangekuwa ni matajiri wakubwa mno sio wa kuomba kuletewa Kuku mweusi
 
Maana ya uchawi kwangu ni wivu na husda tu,ntaamini uchawi siku nikiweza kuroga Atm zitoe pesa ninavyotaka.
Hizo ni vipengele vingine pia vya nguvu ya giza. Uchawi is simply power of darkness. Sasa inajitokeza na kutenda kazi kwa namna mbalimbali, kulingana na mazingira. Kuna uchawi wa kisomi, uchawi wa kitajiri, uchawi wa mazingira ya umaskini, uchawi wa maeneo kama vile baharini, misituni, nk.
 
Wengine Mababu zetu huko nyuma walikuwa ni Watemi ( Chiefs ) hivyo tulishatengenezwa / tulishapikwa mpaka Uchawi ukija unasahaulishwa njia.
You are absolutely right. Shetani na shetani mwenziwe huwa hawagombani. Siyo kwamba wanatoweka, ila unakuwa tayari sehemu ya mfumo wao wa nguvu za giza. Kumbuka anayeshika usukani ni Ibilisi mwenyewe, na ndiye anagawa mamlaka na majukumu kwa agents zake ambao basically wako countless -- wanaoonekana na wasioonekana.
 
Uchawi ungekuwepo:-

Wakoloni wasingewanyanyasa Babu zetu kiasi kile mpaka wanaume wanne wakiwa nusu uchi wanambeba mwanaume mmoja wa kizungu juu kuanzia Kigoma mpaka Kilimanjaro

Wasingechapwa mijeledi kiasi kile na waarabu

Wanaume wa kinijeria wasingechukuliwa watumwa na kupelekwa America kutumikishwa wazee wao waangalie tu

Timu za Simba na Yanga zingekuwa club bingwa za dunia

Wachezaji wa kibongo wangechezea Barca, Real Madrid, Liverpool etc

Mwisho kabisa hao wachawi wenyewe wangekuwa ni matajiri wakubwa mno sio wa kuomba kuletewa Kuku mweusi
Hapo umewaza kwa ufinyu sana, aisee! Unadhani kuna mtu ama taifa lenye hatimiliki ya uchawi na nguvu za giza??? Uchawi ni mtandao mpana wenye lengo na mipango yake. Wanadamu ni chambo tu. Nguvu za giza zinatofautiana, na zinatokea kwa huyohuyo Ibilisi.
 
Back
Top Bottom