Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

nimekwambia naamini mungu yupo,,,ila shetani jini sijui uchawi hivyo vyote siamini hata dhambi siamini kama kuna dhambi
Ukishaamini Mungu yupo, kimsingi unakosa sababu ya kukataa kuamini uwepo wa shetani na uchawi.

Unaamini Mungu gani?
 
Usiye na akili ni wewe unayeamini UJINGA

Imani ya kichawi ni sababu kubwa iliyowarudisha nyuma watu weusi

Badala ya kuwekeza katika elimu na teknolojia wakawekeza katika Imani ya kishenzi kama unayoamini wewe Mshenzi

yaani wewe ni mjinga kabisa
 
Ukishaamini Mungu yupo, kimsingi unakosa sababu ya kukataa kuamini uwepo wa shetani na uchawi.

Unaamini Mungu gani?
Mungu alietumba sisi binadamu naamin yupo,,ila izi mambo za uchawi mashetan majini malaika siamin kama vipo
 
Kama unaamini Mungu yupo, Shetani naye yupo, na ndiye huyu chanzo cha nguvu za giza
mkuu niamini mm uchawi sijui majini shetani ni story tu,,, ngoja nikitulia ntakuletea kisa changu kwann nawaambia uchawi ni stori tu
 
Hio challenge uli toa maelezo haya ?

*majina yako matatu

*majina ya baba yako na mama yako

*tarehe yako ya kuzaliwa

*picha yako

Weka haya maelezo au MPE haya maelezo mtu anayetaka kukuloga halafu uje utoe ushuhuda kama lakini utakua hai
Nipo tayari kutoa details zote hizi..nipe namba za huyo mchawi nimtumie WhatsApp
 
Usiende unless ushajipigilia FIREWALLS za kutosha
Mimi nilikuwa sinaga Habari kabisa na uchawi, lakini yalivonikuta hadi mji wangu mwenyewe nikaukimbia.

Nawaza narudi vipi kwenye boma langu
 
acha kubisha usichokijua mkuu, huduma za ziada wanatoa sana madaktari hasa kwenye matatizo yanayoleta utata, kama una marafiki madaktari jaribu kuwaulizia utapata jawabu.
 
Huyo daktari ni wakumfukuza kazi kabisaa...

Dawa uliotumia haihusiani kabisa na uchawi ni dawa za kawaida kabisa za mitishamba zilizotumika na mababu zetu.

Mke wangu nae alipitiliza siku za kujifungua tukaenda hospital sikutaka maneno mengi nikaacha uchawi wa kizungu ufanye kazi,akala kisu chap mtoto katoka salama kabisa na mama yake akawa vizuri kabisa,ila ninge zubaa pale ningeanza kuletewa ngonjera za kua kafungwa na mambo mengine kibao ya kipuuzi
 
Usiende unless ushajipigilia FIREWALLS za kutosha
Walinirudisha nyuma sana, kila ninachofanya hakiendi biashara zote zikafa na mwisho wakaamua waninyoe nywele, wakanyoa mara ya kwanza ikabidi niende saluni kuzikata zote maana hazikufaa Tena kuwa hivyo, zilivyoota mara ya pili wakaninyoa tena. Nikaona bora niondoke kwanza nikae mbali na hapo.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Hatari sana hao wachawi wanadharau.
 
mkuu Hazard CFC ni ngumu kukuelewesha ukanielewa bt nakushauri jenga urafiki na watu wa afya kisha katika maongezi uwe unawaulize juu ya haya mambo, pia kitu kingine kama uliwahi shuhudia hata mazingaombwe wakati upo shule basi itatosha kujua kua uchawi upo.
 
Nakubaliana na wewe kabisa.

Mimi nimeshuhudia zaidi ya mara 5 nikiwa muhusika.


Uchawi upo aisee
 
Uchawi siyo just supernatural power & knowledge of exceptional mysteries, pia lengo lake ni ultimate control of humanity, degradation na destruction. Hata mtu anaeenda kwa waganga kutafuta njia mkato ya utajiri, kwa nguvu za giza anaweza kupata lakini hatimaye lengo kuu ni kumwangamiza yeye na kuwaangamiza wengine kupitia kwake. Kwa hiyo, utajiri unakuwa kama chambo tu cha kunasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…