Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Hivyo vitisho mnatoa sana ila tukiwaambia mturoge mnashindwa. Tuokoe nguvu na muda niroge au tafuta mchawi aniroge badala ya kunipa vitisho hewa.
Mkuu...KUWA na akiba ya Maneno.. usijiombee mikosi... Wenzako tunaomba Mungu hayo yasitufike.
 
Uchawi upo na unafanya kazi ...Ila kukupata Ni kadari ya Mwenyezi Mungu.
 
Kuna sister alienda chimbo anataka kuolewa na yule Mzee akamfanyia kazi Kisha akamwambia mwanaume wa 3 kukutongoza ukirudi town lazima akuoe kwa harusi ndani ya siku 90 zijazo. Wiki mbili zilizopita tumekula wali ndani ya time frame ile ile ya mtaalam.
Wakati fulani wachawi ama washirikina wanaweza kuinfluence jinsi matukio yatakavyofanyika maishani mwa watu baadaye, kiasi kwamba wanaonekana kana kwamba wanatambua matukio ya baadaye. Mara nyingi hii inatokea pale watu wanapowaamini na hivyo kile walichowatabiria kinakuwa "blue-print" ya mwenendo mzima wa maisha yao so much so that kile walichotabiri kinawatokea. Hali hii pia, mbali na kutumiwa na hao watu wa nguvu za giza, hutumiwa na wataalamu wa saikolojia. Hivyo, ipo pande zote mbili.
 
Uchawi ungekuwepo:-

Wakoloni wasingewanyanyasa Babu zetu kiasi kile mpaka wanaume wanne wakiwa nusu uchi wanambeba mwanaume mmoja wa kizungu juu kuanzia Kigoma mpaka Kilimanjaro

Wasingechapwa mijeledi kiasi kile na waarabu

Wanaume wa kinijeria wasingechukuliwa watumwa na kupelekwa America kutumikishwa wazee wao waangalie tu

Timu za Simba na Yanga zingekuwa club bingwa za dunia

Wachezaji wa kibongo wangechezea Barca, Real Madrid, Liverpool etc

Mwisho kabisa hao wachawi wenyewe wangekuwa ni matajiri wakubwa mno sio wa kuomba kuletewa Kuku mweusi
Kinje yalimkuta na majimaji yake.

Wazee walizidiwa maarifa ya kizungu fullu stop.
 
Uchawi upo na unafanya kazi ...Ila kukupata Ni kadari ya Mwenyezi Mungu.
Actually Mungu wakati wote anataka tuwe salama; lakini, jinsi mazingira yalivyo, athari za uchawi haziepukiki kabisa hata kwa wale wanaojiweka kwa Mungu maisha yao yote. Lakini kujitenga na Mungu ni sababu kubwa mojawapo ya kutekwa na kushambuliwa na nguvu za giza. Hii haina maana kwamba watu wa Mungu (meaning, waumini waaminifu) wao hawashambuliwi. Hapana. Ila tofauti tu ni kwamba waumini wao wanakuwa na ulinzi zaidi. Wanaweza kushambuliwa, wanaweza kupigwa na magojwa kichawi na ushirikina, wanaweza kufanyiwa mauzauza ya ajali, lakini bado wakawa na ulinzi wa Mungu ama wakawa bado watu wa Mungu. Simply, hakuna aliye immune dhidi ya nguvu za giza. Na usikute walio waumini ndiyo washambuliwao mara kwa mara na nguvu za Shetani.
 
Kuna mtu keshawai nisingizia Uchawi... Wewe Dada Rachel ..Mimi hayo mambo Wala siyajui maskini... Sijui nilikufanyaje Hadi ukaniita Mchawi... Nimemuachia Muumba wa mbingu na ardhi... Anitetee
Hii inatokea pale ambapo mchawi anatafuta kukugombanisha na ndugu, jamaa ama rafiki au hata mwenzio, mfanyakazi, whoever mwenye mahusino na wewe. Sasa unakuta vitu vinakutokea, kwa mfano, hisia (ambazo ni kawaida kwa mwanadamu) zinakupeleka kumtilia mashaka na kumhofu mtu fulani kuwa ndiye mchawi anayekusumbua. Wengi wanagombana. Ndoa zinavunjika na hata biashara zinaharibika kabisa, bila kujua mhusika mwenyewe yuko pembeni anavuta nyuzi za kutawala mawazo yenu na kuwachonganisha. Hata wakati mwingine mtu anaweza kuona kabisa ndotoni juu ya mbaya wake fulani -- na pengine asiwe yeye hata kidogo. Ndiyo maana watu wamefikia hatua ya kuuana ama kutengana kwa sababu tu ya chuki za hisia ya kishirikina. Hii isingeweza kuruhusiwa kama watu wangetambua kwamba uchawi ni nguvu beyond uwezo wa kawaida kibinadamu. Na ndivyo Shetani anavyopenda kufanya mambo yaaminike ndivyo siyo ili azidi kudanganya na kuwanasa wengi zaidi.
 
Actually Mungu wakati wote anataka tuwe salama; lakini, jinsi mazingira yalivyo, athari za uchawi haziepukiki kabisa hata kwa wale wanaojiweka kwa Mungu maisha yao yote. Lazikini kujitenga na Mungu ni sababu kubwa mojawapo ya kutekwa na kushambuliwa na nguvu za giza. Hii haina maana kwamba watu wa Mungu (meaning, waumini waaminifu) wao hawashambuliwi. Hapana. Ila tofauti tu ni kwamba waumini wao wanakuwa na ulinzi zaidi. Wanaweza kushambuliwa, wanaweza kupigwa na magojwa kichawi na ushirikina, wanaweza kufanyiwa mauzauza ya ajali, lakini bado wakawa na ulinzi wa Mungu ama wakawa bado watu wa Mungu. Simply, hakuna aliye immune na nguvu za giza. Na usikute walio waumini ndiyo washambuliwao mara kwa mara na nguvu za Shetani.
Ndo maana nikasema uchawi upo..ila kukupata NI "KADARI YA MUNGU"
sijasema kuwa huwezi patwa na uchawi kwakua Ni mcha Mungu.

Ila Kama unaamini Mungu na unajua Mwenyezi Mungu atosha HUPASWI KUOGOPA UCHAWI.
Kuna watu KILA hatau yeye anaogopa kurogwa..hata kuvaa nguo mpya hawezi.
Naomba Mwenyezi Mungu anikinge na Sihri na Shari za walimwengu...Amin

Naamimi pia nisiwe miongoni mwa wale wanaosababisa Shari, fitna na vitimbwi kwa Watu wengine.
 
Muwe mnasikai tu fulani karogwa, anasumbuliwa na wachawi usiku, n.k haya mambo yakiwakuta.


Nguvu za giza haziwezi kuonekana kwa macho yetu ya kawaida wala kupimwa na vifaa vya kisayansi, Ni sawa na kurekodi ndoto ya mtu uione kwenye video, haiwezekani, hata mtu akirogwa bado ipo gizani ndio mana hata ukienda hospitalini utaambiwa mashine haziwezi kugundua chanzo cha ugonjwa wako

Binafsi nilikaa nyumba moja, ikifika saa saba kuna vishindo mithiri ya mtu anakwangua ukuta kwa nondo, na hii ilikuwa kwa wapangaji wote ila ukitoka nje kucheku huko nyuma hakuna kitu.

Ni mpaka siku moja mida hio saa saba kikalia kishindo kikubwa sana paaaa! juu ya bati kila mpangaji alitoka nje ila hakukuonekana kitu, baada ya kufatilia kumbe kuna mlangaji moja alikuwa anateswa na hawa watu usiku, babu yake alikuja siku hio hapo na kuweka mtego wake.

Tukio lengine kuna mtoto moja alikuwa na miaka mitano alikuwa mzima wa afya, ghafla akawa kipofu, kiziwi na hata kushindwa kuongea, Wazazi wake wakagundua hii hali si kawaida, walimpeleka hospitali nyingi muhimbili, kcmc, n.k ilibidi apelekwe kijijini kwa mzee wake, siku hio hio walirudi na mtoto akawa hali ya kawaida kabisa

Hapo zamani sijui kama sikuhizi bado vipo, Mashuleni ya porini huko boarding visa vya wanafunzi kukutana na vibwengo ilikuwa ni kawaida sana

Mwengine nakumbuka alivimba sana miguu, walimsihi sana waende kwao kuchekiwa ila alikua haamini hvi vitu, hata miezi miwili haikufika tukamzika.
Kiboko yao ni Jina la Yesu Kristo.
Mapepo hayo, yanakimbia kwa imaniisiyo na shaka.
 
Mimi Pia nilikua siamini hadi nimepata matatizo sasa NAAMINI ASILIMIA MIA UCHAWI UPO!!!

Nikiwa na mimba ya miezi mitano niliota nagombania mtoto wangu na watu wawili mwisho wa siku na kweli mwanangu kafa kiajabu ajabu

all in all Mungu yupo ye ndio anaruhusu kila jambo linalotokea cha muhimu ni kumuomba Mungu kwa imani yako!
 
Ninapoishi hapa kuna mlokole mmoja hivi yeye na kanisa ,kanisa na yeye Ila juzi kampeleka mwanaye Kwa mganga baada ya mambo kuwa mengi...
 
Uchawi ni nini? Unaweza kuu define uchawi ni nini?

Ukisema "uchawi una lengo la kumuweka mtu matatizoni" bado huja define uchawi, kwa sababu hata uongo unaweza kuwa na lengo la kumuweka mtu matatizoni, hata kumpiga mtu risasi kunaweza kuwa na lengo la kumuweka mtu matatizoni.

Unaweza kuthibitisha hicho unachofikiri ni uchawi ni uchawi kweli na si kitu kingine ambacho hukijui tu?
Mkuu mbona mgumu kuelewa, naona una tatizo la kuelewa vitu kwa haraka inabidi ueleweshwe mara nyingi ili uelewe (kilaza).

Ushaambiwa uchawi unahusisha nguvu za giza wewe unaanza kuleta tena hoja za mapolisi, Duh ipo kazi, Labda utafute mtu mtaekaa nae siku nzima akueleweshe, Mbona wengine wanaelewa fasta tu, wewe siku ya pili hii huelewi tu 😁😁
 
Mimi simjui Mchawi wakukuroga Wala sikuombei kurogwa..

Ila Ni kheri kukaa kimya kuliko kuomba mikosi ikupate.
Kawaida hiyo.

Pia tuache kudhani waganga wote ni wachawi.

Waganga wapo enzi na enzi ndio waliotutibia babu zetu
 
Mimi Pia nilikua siamini hadi nimepata matatizo sasa NAAMINI ASILIMIA MIA UCHAWI UPO!!!

Nikiwa na mimba ya miezi mitano niliota nagombania mtoto wangu na watu wawili mwisho wa siku na kweli mwanangu kafa kiajabu ajabu

all in all Mungu yupo ye ndio anaruhusu kila jambo linalotokea cha muhimu ni kumuomba Mungu kwa imani yako!
Uchawi upo siku zote.

Ila watu wanachochanganya ni kuamini uchawi haupo badala ya kuamini kwamba haya maisha unaweza kuishi bili kutumia uchawi.

Mfano mtu aliye elimika kufanya biashara, anaweza kutumia elimu hio kufanya biashara bila kwenda kutumia uchawi wa kutoa kafara.

Ishu inakuja kwamba mtu haamini kabisa uchawi upo, Hawa ndio huwa wanateseka sana, Anaamka kila siku kapigwa chale anadhani kakunwa.

Alafu wachawi wajanja sana, wanatuwekaga katika hali ya kuzoea matatizo kama chura, chura ni kiumbe ambae anaweza ku controll joto la mwili wake, huko china wanapokula vyura ukimweka chura kwenye maji yamoto anaruka anatoka kwenye sufuria, ila ukimweka kwenye maji ya baridi ukaanza kuyachemsha kwa moto wastani basi huyo chura hawezi kutoka humo na mwisho wa siku anafia na kuiva humo humo kwenye sufuria.

Sasa na wachawi ndio wapo hivi, Leo unaweza kuamka na ka chale kadogo sana ukasema umejikuna, wiki ijayo wanarudi tena wanakupiga, inafikia kila siku unaanza kupigwa hizo chale tena sehem mbali mbali, kipindi hicho wewe kwako ushazoea unaona sio ishu sana kumbe ndio unaangamia hivo
 
Watu wanateseka na uchawi wewe unafanya mzaha pumbavu zako tena ukome kupotosha watu MBWA WEWE MUSSA NA MTUME WALIROGWA WEWE MBWA KASORO MKIA UMEOKOTA WAPI UPUMBAVU HUO MNAPOTOSHA WATU WANAANGAMIA NYIE MNACHEKELEA MAMA ZENU WASHENZI NYIE
Acha kuamini ushirikina ndio mana africa hatuendelei kwa akili hizo za kuamini upuuzi.wenzetu wanawaza kwenda sayari nyingine sisi tunaamini ujinga wa ushirikina ,hakuna uchawi wala nini duniani ni imani tu za kijinga

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona mgumu kuelewa, naona una tatizo la kuelewa vitu kwa haraka inabidi ueleweshwe mara nyingi ili uelewe (kilaza).

Ushaambiwa uchawi unahusisha nguvu za giza wewe unaanza kuleta tena hoja za mapolisi, Duh ipo kazi, Labda utafute mtu mtaekaa nae siku nzima akueleweshe, Mbona wengine wanaelewa fasta tu, wewe siku ya pili hii huelewi tu [emoji16][emoji16]
Mapolis tenaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hatarr
 
Back
Top Bottom