Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

🤣 🤣 kama sahizi tu sipindui meza, ukichota nyayo si itakua balaa.. nitarudi kwenye huu uzi kupinga yote.
Haha..!
Mwanangu bado hujakolea, nataka nikukoleze mpaka ukiskia jina langu popote unaamka..!
 
Kumbe wachawi wanaenda majuzi eeh!! Me nilidhani kwa situation Kama hiyo akikukuta anakuua kabsa,Kama ndo hivyo back uchawi ni upuuzi
 
"confidence yako ilikusaidia," really!? Huo uchawi wa kuzimwa kwa "confidence" wala hata siyo uchawi; itakuwa kitu kingine kabisa.
 
Hapo kwenye kuona sababu ya kudhuru,kwann wactumie uchawi kumalizana na makundi ya kigaidi,etc
 
Hiyo huwa inatokea usiku wa manane unaisikia inafunguka na asubuh ukiamka unaikuta iko wazi.
Na kuna nyingine unasikia nyayo za mtu anatembea nje ya dirisha ukifungua pazia kuchungulia hakuna kitu hii nayo utasemaje?
Sasa ushasema mtu unasikia anatembea af unashangaa ukifungua dirisha humuoni,me nataka uniambie kwa mfano umekaa nje af unasikia hatua zinakufuata ila mtu mwenyewe humuon,
 
"confidence yako ilikusaidia," really!? Huo uchawi wa kuzimwa kwa "confidence" wala hata siyo uchawi; itakuwa kitu kingine kabisa.
hujaelewa,sijasema confidence ilizuia uchawi nilichosema kwamba huyo bibi aliamua kumpotezea kutokana na confidence yake kuonesha hana ubaya.
Kwani kuwa na urafiki na mtoto wa mchawi ni kosa?halafu ukizingatia wote ni watoto tu,akitaka kuthibitisha kama huyo bibi kweli ni mchawi au sio mchawi akishakuwa mkubwa aende kumdhulumu kiwanja au kitu chochote chenye thamani ndio ataona.
Uchawi huwa hautumiki kwa michezo ya kitoto
 
Sasa ushasema mtu unasikia anatembea af unashangaa ukifungua dirisha humuoni,me nataka uniambie kwa mfano umekaa nje af unasikia hatua zinakufuata ila mtu mwenyewe humuon,
nitatokaje nje wakati nahofia usalama wangu.
halafu nikidhurika utanisaidia nini zaidi ya ubishani wa kitoto tu hapa.
Hiyo labda uje kuifanya wewe ambaye huamini uwepo wa uchawi,uje ulale halafu tukisikia vishindo utoke nje ukawe mlinzi wetu
 
Naona tunaelekea kuelewana sasa. Hoja kubwa hapa ni kwamba, Uchawi upo ama haupo??? Umesema wazi, "nitaogopaje" maana "haiwezi kufanya kazi pasipo na ww kuikubali;" ukiukubali "umekwisha." Kwa maelezo haya, hakuna mashaka tena kuwa unakubali na kuamini kuwa ushirikina siyo hadithi tu za kubuni -- upo na una madhara makubwa na unaua pia. Nimekuelewa sana!
 
Mbona unashupalia vitu ambavyo guns uhakika navyo yan ngozi bwana!! Sasa hapo wewe una uhakika gan Kama kweli hiyo bibi ni mchawi,na nyie ndo mabingwa wa kuchukua story za vijiweni af unapeleka pale utasema wewe ndo mhusika,
 
ukitaka kujua uchawi upo au haupo nenda vijijini kama usukumani halafu uwaambie wazee kwamba hakuna kitu kinaitwa uchawi na kama kipo kitu kinaitwa uchawi wakuoneshe
Kwann ukiongelea uchawi back lazima uhusuanishe na maeneo ya kijijini kuliko mjini,kushadadia uchawi unapatikana zaidi kijijini inaonesha wazi kuwa uchawi ni udumavu wa akili kwan dunia inatambua washamba,wasioelimika,wakings,vilaza etc wengi wanapatikana zaidi maeneo ya vijijin
 
No uchawi unafanyika sana kwa sababu ya usiri uliopo kule kijijini.
Mjini kutokana na population ya watu waliopo limawanyima uhuru wachawi kuishi mahali hapo kwa kuona aibu kuwa mambo yao mengi yatastukiwa.
 
nitatokaje nje wakati nahofia usalama wangu.
halafu nikidhurika utanisaidia nini zaidi ya ubishani wa kitoto tu hapa.
Hiyo labda uje kuifanya wewe ambaye huamini uwepo wa uchawi,uje ulale halafu tukisikia vishindo utoke nje ukawe mlinzi wetu
Me nlipokuwa nilikuwa natoka saa name za ucku naenda kuisoma darasa zima unanikuta peke yangu,ukiuliza waskaji watakwambia wanaogopa huo uduwanzi
 
mbona wabunge na mawaziri ni matajiri na wanapishana kwenda kwa waganga kuroga hapo utasemaje?
Mosi, sina ushahidi wowote shakinifu na tajisimu (tangible & physical) kwamba viongozi "wanapishana kwenda kwa waganga kuroga"!? Lakini, swali la msingi pengine linahusu sababu ya wao kuwa matajiri ilhali wameenda kwa waganga? Ambacho tunapaswa kujua ni kwamba nguvu ya ushirikina na uchawi inaweza kukupatia vitu karibu vyote unavyoweza kutamani hapa duniani -- mali, elimu, utajiri na mapochopocho na mambo mengine mengi tu. Kila mtu anapewa kwa kadiri ya utashi na tamaa na vipaji na uwezo wake na uwezekano (potential) wa jinsi anavyoweza kuwa baadaye na kutumiwa kifanisi kwa maslahi ya "bosi" wake. Ndiyo maana utakuta kwenye ujinga na ushirikina, matokeo ndiyo hayo -- kunapatikana ujinga na ushirikina; penye mwamko wa elimu na ustaarabu na utajiri -- ushirikina unakupatia vitu hivyo na zaidi. In short, kiwango chako cha uelewa ndicho kitaamua unapewa kiasi & kiwango gani cha "hazina ya kuzimu." Anakupatia uwezo na ushawishi mkubwa ili ukasaidie vizuri kuwaghilimu wengi na kuujenga ufalme wake wa giza.
 
Kama hivyo vitu havipo basi ujue uchawi hauna nguvu
Uchawi ni imani kama vitu vingine kijana acha kuogopa lakn siwezi kukulazimisha kukubali endelea kuugopa uchawi mm nadunda duniani lkn kuhusu uchawi siwezi kurogwa wala kufa kwa uchawi kwangu mm hiko kitu hakitotokea never
Ila kwako kinaweza kukutokea ila sio lazima ukubali navyosema
 
Hata mm nimekubali kwa unayosema wala sipingi kwangu mm uchawi hauna nguvu wala hauniwezi kwa lolote siwezi kurogwa mpk nife kwa uchawi hiko kitu hakuna kwangu
Ila kwako uchawi upo tena una nguvu na tena una nguvu na unaweza kukuroga ww na ukafa mara moja
 
Unaweza usikubali kwamba uchawi upo, lakini ukarogwa na ukafa mazima. Usicheze, aisee! Mshukuru sana Mungu. Pili, wapo wachawi maskini, wapo wachawi matajiri. Hakuna nyanja ya maisha hapa duniani ambapo Iblisi hajafanikiwa kupenyeza usibifu na uchafuzi wake wa kishetani. Magonjwa, ajali na matatizo mengi, yeye ndiye chanzo na mshika-usukani. Tatu, ukishaingia kwenye uwanja wa mashetani, uamuzi wa mwenendo wa maisha yako unakuwa umesalimishwa kwa Shetani mwenyewe. Anachotaka uwe ama ufanye ndivyo utakavyofanya maadamu bado ungali kwenye anga za giza. Anaweza akakutumia kwenye utajiri au katika umaskini au kwenye elimu na mafanikio na umaarufu wako. Anachohitaji yeye lengo lake litimie la kujikusanyia watu wengi kadiri iwezekanavyo katika ufalme wake. Mwisho, kwa nini serikali za dunia zisitumie uchawi kuwaroga wapinzani wao??? Kumbuka hili si jambo geni, mambo kama haya yanatokea duniani. Na visa vipo, vingi tu. Lakini pia, uamuzi wa mwisho wa hatma ya uhai wa mwanadamu yeyote haujawekwa kwa mwanadamu mwingine, bali upo kwa Mungu! Mtu fulani akifanyiwa mauaji, hata kama siyo kwa namna ya kawaida au kifo cha asili, basi lazima Mungu anakuwa ameridhia uhai wake ufikie ukomo -- ingawa mwuaji wake anabaki kuwa mwalifu na mkosaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…