Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Uchawi ni kutumia uwezo usio wa kibinadamu ama nguvu za giza (supernatural power) katika kuathiri na kubadili matukio, kuwatawala watu, kuteka, kuvuruga na kuhilibu (manipulate), kusumbua, kutisha, kutesa, kudhuru, kuangamiza, au kuua.
The arts and practices of individuals who have formed compact with the Devil or with evil spirits, by whose supernatural powers and aid they are able to cause all sorts of injury to living beings and things.
 
PLEASE, SIKILIZA HADI MWISHO USHUHUDA HUU WA KUSTAAJABISHA SANA, UTAJIFUNZA KITU

Uchawi ni ufananishaji wa matukio mabaya kwa kumuunganisha adui yako na mabaya yanayokukuta
 
Uchawi ni kitu kipo kabisa, ni halisi; tena wala haina ubishi. Na upo katika viwango (grades) mbalimbali -- ni aina fulani ya taaluma ya nguvu za giza. Believe it or not.
Kama ulishaona mazingaombwe/viini macho basi jua uchawi upo.
 
Muwe mnasikia tu fulani karogwa, anasumbuliwa na wachawi usiku, n.k haya mambo yakiwakuta ndo mtaijua anaeisimulia mvua basi iliwahi kumnyeshea

Nguvu za giza haziwezi kuonekana kwa macho yetu ya kawaida wala kupimwa na vifaa vya kisayansi, Ni sawa na kurekodi ndoto ya mtu uione kwenye video, haiwezekani, hata mtu akirogwa bado ipo gizani ndio mana hata ukienda hospitalini utaambiwa mashine haziwezi kugundua chanzo cha ugonjwa wako

Binafsi nilikaa nyumba moja, ikifika saa saba kuna vishindo mithiri ya mtu anakwangua ukuta kwa nondo, na hii ilikuwa kwa wapangaji wote ila ukitoka nje kucheku huko nyuma hakuna kitu.

Ni mpaka siku moja mida hio saa saba kikalia kishindo kikubwa sana paaaa! juu ya bati kila mpangaji alitoka nje ila hakukuonekana kitu, baada ya kufatilia kumbe kuna mlangaji moja alikuwa anateswa na hawa watu usiku, babu yake alikuja siku hio hapo na kuweka mtego wake.

Tukio lengine kuna mtoto moja alikuwa na miaka mitano alikuwa mzima wa afya, ghafla akawa kipofu, kiziwi na hata kushindwa kuongea, Wazazi wake wakagundua hii hali si kawaida, walimpeleka hospitali nyingi muhimbili, kcmc, n.k ilibidi apelekwe kijijini kwa mzee wake, siku hio hio walirudi na mtoto akawa hali ya kawaida kabisa

Hapo zamani sijui kama sikuhizi bado vipo, Mashuleni ya porini huko boarding visa vya wanafunzi kukutana na vibwengo ilikuwa ni kawaida sana

Mwengine nakumbuka alivimba sana miguu, walimsihi sana waende kwao kuchekiwa ila alikua haamini hvi vitu, hata miezi miwili haikufika tukamzika.
Mkuu kama unaamini kuwa uchawi upo, basi vile vile uamini kuwa kuna nguvu, tena KUBWA SANA kuliko uchawi.
Nguvu hiyo iko ndani ya Yesu Kristo.
Hapo wachawi wanagwaya na kukimbia na wengine wengi tu hujisalimisha kwa NGUVU hiyo,
Mbembe Yesu Kristo moyoni mwako na uone kwa kshuhudia wachawi wakipagawa!
 
Hakuna asiyejua nguvu ya Muumba wa hii dunia ni kubwa mno, iwe katika jina la yesu au kwa kumwamini mtume mohamed.

Changamoto zake ni dhambi inayofifisha hii nguvu, dhambi kama uzinzi, ulevi, uongo, n.k ndio hurudisha watu nyuma na mbaya zaidi dunia ya sasa watu wanaona ni sifa kuwa mzinzi, mpigaji wa rushwa au wizi, kudanganya, n.k
 
Umenena kweli mkuu!
Mimi siwezi kujigamba kuwa mkamilifu maana kama binadamu wengine ni mdhaifu wa mwili, lakini nimeshuhudia ubaya ukiyeyuka mbele ya Nguvu hii kubwa ya Yesu.
 
Kuna banda niliwahi kupanga Jijini Dar wapangaji wenzangu tuliokuwa tumepanga pale miongoni mwao ni mama mmoja wa kiha ambaye alikua anaishi na wanae 3 wote walikua wakike, huo muziki tuliyopata hapo sio wa nchi hii, mpaka hivi sasa naandika kuna vitu bado vinaniandama nilivyofanyiwa na yule mama wa kiha

Nahitimisha kwa kusema si hayo tuu nimeshuhudia yapo mengi sana nashindwa niyaeleze vipi.
 
Mimi sasa nina miaka 30+ . Sijawai kushuhudia tukio lolote la uchawi zaid ya labda kuona kwenye social media, video,Tv, etc.

Nimesoma shule za bweni jirani yangu analalamika kunigwaa mimi hata sikuwahi kusikia hata siku moja.

Natamani nishuhudie na mimi siku 1. Otherwise siamini kama uchawi upo
 
Back
Top Bottom