Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Ujasiri wa kimungu haufungamani na mambo ya anasa. Unaweza ukaomba nguvu za kimungu ukazipewa ila the moment umetomb@na au kufululiza pombe basi unarudi kwenye mikono ya watesi wako chap na nguvu zinakuwa zimefifia.

Hapo ndipo ugumu ulipo.
The moment mtu akimwacha Maulana tu, basi anakuwa amejiweka kwenye uwanja wa mtawala Iblisi Shetani. Ulimwenguni kuna mamlaka mbili tu: giza na nuru. Ukiacha au ukajitenga na nuru basi hapo automatically unakuwa umemchagua "mungu" wa dunia -- mashetani. Wanakutumia kadiri watakavyo. Sasa unakuta mtu anakwambia mbona niko sawa tu, au sina shida hiyo? Hawa ni wazi hawana idea yoyote ya namna Shetani anavyofanya kazi yake tena kiustadi mkubwa, mtu asikudanganye kutumia akili yako tu eti unataka kum-outsmart (kumpiku akili) Iblisi. No way! Hiyo ni nguvu ya level nyingine kabisa. Mtu anaweza kabisa akawa normal 100% kwa mwonekano wa nje, kumbe ndiye amepagawa na mapepo balaa na wala wakati mwingine asitambue. Hiyo nguvu siyo ya kitoto, aisee!
 
Hio challenge uli toa maelezo haya ?

*majina yako matatu

*majina ya baba yako na mama yako

*tarehe yako ya kuzaliwa

*picha yako

Weka haya maelezo au MPE haya maelezo mtu anayetaka kukuloga halafu uje utoe ushuhuda kama lakini utakua hai
Namshauri tu asicheze na uhai kwa sababu generally hauji mara mbili hapa duniani; asije akajikitu anakufuru bure. Asome tu historia maana hizo experiments anazotaka kufanya ni marudio tu, watu walishafanya sana tu, na wamejuta.
 
mkuu samahani, hivi uchawi nini. kuinga kitu usichokijua maana nao ni ujinga, maana leo hata Dunia ya walioelimika, wanajua uchawi upo, ispokua hawaupi kipaumbele, karika kufanikisha au kufelisha mambo yao.

kitu ambacho hata huku, usipoupa kipaumbele kafanikisha ua kufelisha mambo yako, maisha yatasonga na wala hutosumbuka.
Ila uchawi upo, Kwa waumini wa Dini, haya mambo yameandikwa kwenye Vitabu vyao.
Uchawi ni imani na kumbuka katika mambo muhimu yanaomzunguka binadamu imani ni jambo la muhimu hivyo huwezi kukwepa imani
Jiulize kama uchawi upo kwanini usitumike kufanya mambo kama vile kushinda kitu au hata kupata maendeleo
 
Mimi nimeshaomba sana wachawi waniroge ila wanaishia kubwabwaja tu.

Hata hapa nimeshawaambia wachawi waniroge...kama wanataka kucha au sehemu ya nywele zangu au kipande cha nguo waje kuchukua

Huwa wanaishia kutishia tu.
Wachawi gani uliwaomba wakuloge, mchawi aloge hovyo hu target jambo
 
Uchawi ni imani na kumbuka katika mambo muhimu yanaomzunguka binadamu imani ni jambo la muhimu hivyo huwezi kukwepa imani
Jiulize kama uchawi upo kwanini usitumike kufanya mambo kama vile kushinda kitu au hata kupata maendeleo
Fikiria tena aisee! Watu wanaenda kwa waganga na kweli, loh & behold, wanakuwa amazing zillionaires kesho yake asubuhi! Sema tu Shetani anakutumia ukishajikabidhi kwenye anga zake, ndiyo maana hakuna kitu hatari kama kujitafutia utajiri kishirikina. Lazima utazilipa tu, one way or another --- mara nyingi ni kwa gharama ya damu yako, watu wako wa karibu au makafara au hata ajali zisizoeleweka, sometimes.
 
Muwe mnasikai tu fulani karogwa, anasumbuliwa na wachawi usiku, n.k haya mambo yakiwakuta.

Binafsi nilikaa nyumba moja, ikifika saa saba kuna vishindo mithiri ya mtu anakwangua ukuta kwa nondo, na hii ilikuwa kwa wapangaji wote ila ukitoka nje kucheku huko nyuma hakuna kitu.

Ni mpaka siku moja mida hio saa saba kikalia kishindo kikubwa sana paaaa! juu ya bati kila mpangaji alitoka nje ila hakukuonekana kitu, baada ya kufatilia kumbe kuna mlangaji moja alikuwa anateswa na hawa watu usiku, babu yake alikuja siku hio hapo na kuweka mtego wake.

Tukio lengine kuna mtoto moja alikuwa na miaka mitano alikuwa mzima wa afya, ghafla akawa kipofu, kiziwi na hata kushindwa kuongea, Wazazi wake wakagundua hii hali si kawaida, walimpeleka hospitali nyingi muhimbili, kcmc, n.k ilibidi apelekwe kijijini kwa mzee wake, siku hio hio walirudi na mtoto akawa hali ya kawaida kabisa

Mwengine nakumbuka alivimba sana miguu, walimsihi sana waende kwao kuchekiwa ila alikua haamini hvi vitu, hata miezi miwili haikufika tukamzika
kiongozi kama wewe kijana utakua unamaisha duni sana..utakua unashinda sana kwa waganga....Nakuonea huruma
 
The moment mtu akimwacha Maulana tu, basi anakuwa amejiweka kwenye uwanja wa mtawala Iblisi Shetani. Ulimwenguni kuna mamlaka mbili tu: giza na nuru. Ukiacha au ukajitenga na nuru basi hapo automatically unakuwa umemchagua "mungu" wa dunia -- mashetani. Wanakutumia kadiri watakavyo. Sasa unakuta mtu anakwambia mbona niko sawa tu, au sina shida hiyo? Hawa ni wazi hawana idea yoyote ya namna Shetani anavyofanya kazi yake tena kiustadi mkubwa, mtu asikudanganye kutumia akili yako tu eti unataka kum-outsmart (kumpiku akili) Iblisi. No way! Hiyo ni nguvu ya level nyingine kabisa. Mtu anaweza kabisa akawa normal 100% kwa mwonekano wa nje, kumbe ndiye amepagawa na mapepo balaa na wala wakati mwingine asitambue. Hiyo nguvu siyo ya kitoto, aisee!
Sasa lakini mbona watu wengi wapo Neutral tu na maisha yanaendelea. Saingine majaribu hutegemea na mazingira uliopo.

Ukiwa unaishi ushenzini ndio mara nyingi kuna hivi visanga ila huwez sikia wanga wameingia Oysterbay au Masaki kwa matajiri. Mambo haya zaidi ni Chanika,Mbagala, Temeke, Kisarawe, Vingunguti, Tandale, Keko, Mabibo, Magomeni huko.
 
kuna watu mnabisha tu ili siku ziende, lakini ukweli mnaujua kwamba uchawi upo.
 
Wachawi gani uliwaomba wakuloge, mchawi aloge hovyo hu target jambo
Wapo wale ambao kazi yao "kutest mitambo," yaani wanapimana ubavu, bila kijali nini. Hii inatokea sana maeneo ambako kuna watu wa kabila, koo, ama jamii ya nasaba moja inaishi pamoja. Huwa kuna kupimana ubavu. Watu wanachanjwa hadi maeneo nyeti, wanalishwa au kumezeshwa vitu vya ajabuajabu, wanapewa kutafuta vitu mbalimbali ili wawekewe mazindiko ya kishirikina. Duh!
 
Hii ya kutest mitambo ipo Sana na hata sehemu ninayo ishi nikiwa mgeni walikuja hasa ukikaa eneo lenye wenyeji wa asili Wana hizi mambo na wanarogana kwa kwenda mbele. Sijui hupata faida gani?
 
Back
Top Bottom