Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Nimehitimisha kwamba watu wasioamini uchawi upo hayajawakuta, na yakiwakuta huteseka bila kupona mpaka kifo

Uchawi upo lakini unashindwa na roho ya kijasiri isiyo na hofu!!
Mkuu kuna nyumba huku inapangishwa, huwa watu hawamalizi week wanakimbia.. njoo na roho ya kijasiri mkuu me unipe hela ya udalali tu
 
Mkuu, Kinapatikana wapi hicho kitabu?
Unaweza kuagiza tu online mkuu kama havipo kwenye maduka makubwa ya vitabu hapa Tz au Nairobi.

Mimi nilipatiwa na Mzee mmoja wa kanisa letu miaka kadhaa nyuma...yeye ana access kubwa na wachapaji wa vitabu vya dini ya kikristo wa ulaya na Marekani.

Kwa Amazon ni rahisi sana kukinunua.
 
sasa ww unamini vipi kwamba kuna visivo onekana wakati huvioni
Unaandika hata usichokijua; uchawi, ushirikiana hauonekani kwa macho mechanism inavyofanyika ila athari zake zinaonekana wazi. Wapo wachawi wengi wanatumika tu sana, mvuta-uzi akiwa ni Iblisi mwenyewe.
 
Uchawi upo na Wazungu walianza kabla yetu....now kwao wameupa jina zuri tamu wanauita SAYANSI &, TECHNOLOGY.
Sisi bado tuko ujima Uchawi ila tunasogea sogea slowly tutawafikia na sisi.
Hapo unaposema uchawi ni sayansi & teknolojia, unapitiliza aisee. Tafuta maana ya sayansi na maana ya uchawi, utaelewa
 
Kuna mtoto wa rafiki yangu alipotea mara ya kwanza three days akaja okotwa porini na wachana mbao, alipoulizwa alikua wapi anasema hajui ila ameacha wenzake, last year alipotea one week alitafutwa mpaka wakakata tamaa kwamba atakua amekufa na kumbuka baada ya kupotea mara ya kwanza alipopatikana wakaanza kumfungia ndani hata shule wakamwachisha kwa muda, siku hyo walisahau kufunga mlango na watu wote wako kazini house girl yuko uani anafua dogo akachomoka akapotea, tulienda kwa fundi mmoja hv tukamwelezea akasema huyo mtoto bado yuko hai na anarudi, ndani ya dakika chache mke wa jamaa anapiga cm mtoto karudi ilikua saa mbili usiku anaulizwa ulikua wapi anasema alikua porini wanavuna karanga na amewaacha wenzake wanaendelea yy ameshamaliza, dogo alipelekwa kwa fundi akatengenezwa mpaka leo yuko vizur afungwi kamba hapotei na shuleni wana evening prepo anaenda na kurudi mwenyewe usiku, so uchawi upo nimeshuhudia kwa macho.
Kwa nini hawajenda church kumsalia?
 
Mkuu leo niambie ukakasi wako upo wapi ili nikupe elimu ya uchawi
Mkuu sihitaji hiyo elimu duni aisee. Inatosha to kusema giza haliwezi kamwe kuzidi mwangaza. Iblis atawatumieni, akishawakamua kila kitu anawatema na kuwaaibisha. Hebu fuatilieni jinsi wenzenu wanavyopukutika deile kama mbelewe kwenye upepo.
 
Yohana 1:4-5 Inasema Nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza Nuru.

Nuru ni Yesu Kristo, ndie Bwana wa mabwana wote, ndie Mfalme wa wafalme hao.

Hao wenye vyeo kuzimu vya uchawi mpaka kufikia kuitwa wafalme wa wachawi, nao wana Mfalme wao, nae si mwingine ila ni Yesu Kristo, Simba wa Kabila la Yuda kutoka uzao wa Mzee Yese.
 
Hizo ni imani tu na wenge lenu usiku

Hakuna kitu kama hicho (uchawi) uyo mtoto aliyekuwa kipofu, kiziwi nk apelekwe hospitali utapewa chanzo na nini kifanyike
Mungu akuepushie mbali maana mtu kama wewe ukiguswa kidogo tu unakuwa msukule kwani unafahamu upande mmoja tu wa dunia na hayo maneno uliyoyaandika yaishie humuhumu jf ukienda ukatamke maneno haya mbele ya wazee cha kwanza watakusoma jicho usiku.
 
Mkuu sihitaji hiyo elimu duni aisee. Inatosha to kusema giza haliwezi kamwe kuzidi mwangaza. Iblis atawatumieni, akishawakamua kila kitu anawatema na kuwaaibisha. Hebu fuatilieni jinsi wenzenu wanavyopukutika deile kama mbelewe kwenye upepo.
Hujaelewa kama huelewi
 
Yohana 1:4-5 Inasema Nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza Nuru.

Nuru ni Yesu Kristo, ndie Bwana wa mabwana wote, ndie Mfalme wa wafalme hao.

Hao wenye vyeo kuzimu vya uchawi mpaka kufikia kuitwa wafalme wa wachawi, nao wana Mfalme wao, nae si mwingine ila ni Yesu Kristo, Simba wa Kabila la Yuda kutoka uzao wa Mzee Yese.
Yesu mwenyewe alikuwa anafanya maajabu nyinyi mnaita miujiza lkn hakuna tofauti Kati ya uchawi na miujiza zote ni kuenfluence natural power
Tofauti ni jinsi utakavyotumia ili kuangamiza wenzako au kuuwa hapo tunasema uchawi lkn hata Yesu mwenywe alikuwa anapractise uchawi

Ngoja nimwite Astronomer
 
Wengi hawajui amini nakuambia kuanzia Mussa Suleimani hadi Yesu wote walikuwa wana practise uchawi

Na kabla ya kujua walikuwa wana practise vp uchawi unatakiwa ujiulize uchawi ni nini?
 
Unajuaje wewe unaweza kunipa elimu mimi na si mimi ninayeweza kukupa elimu wewe?
Yote sawa tu hakuna asiejua yote na pia hakuna pia anaejua yawezekana ukawa unajua mengi na pia yawezekana pia mm nikawa najua kidogo
 
Hizo ni imani tu na wenge lenu usiku

Hakuna kitu kama hicho (uchawi) uyo mtoto aliyekuwa kipofu, kiziwi nk apelekwe hospitali utapewa chanzo na nini kifanyike

Shukuru Mungu hujawahi kutana nayo.!
 
Back
Top Bottom