Tafuta Machinjio ya MBUZI, fanya yafuatayo :-
1. Nunua vichwa vya mbuzi kwa 2500 - 3000/- kila kichwa
2. Andaa sehemu ya kupikia, ( Karibu na grocery/bar au sehemu yenye mkusanyiko)
3. Andaa Vifaa kama vile, sufuria kubwa, jiko, visu, bakuli, sahani.
4. Mahitaji, unga, chumvi, pili pili, nyanya, vitunguu, kiberiti, mkaa,
Maandalizi
Chukua kichwa cha mbuzi, kiandae ukiwa bado upo nyumbani ( koka moto wa kuni, choma vichwa hakikisha manyoya yote yanaungua, baada ya hapo tafuta sufuria kubwa vichemshe mpaka vinaiva kisawa sawa, ( kazi hii ifanyike asubuhi ikifika mchana kila kitu kiwe tayari,)
. Mida ya saa nane andaa sufuria ndogo ndogo kwa ajili ya ku roast vichwa vya mbuzi, ( nyanya, kitunguu, chumvi, pilipili ni mhimu, ) ( usiuze kichwa kama kilivyo unakiponda ponda kama ulojo fulani vile, Wataalam wa haya mambo waananielewa ninacho maanisha)
. Kichwa kimoja fanya elfu 6000 - 7000/- nusu kichwa fanya elfu 3000 - 4000/- plus ugali 4000 - 8000/-,
. Vichwa 5 × 2500 = 11500/-( gulioni)
. Baada ya kuuza 6000 × 5 = 30000/-
. Ugali 1000 matonge 10 =?
. NB: kwenye kila mteja atakaye kuja kuorder iwe nusu au Kichwa kizima hakikisha unapunguza nyama 2 au 3, mpaka unapata kichwa kingine cha ziada, ( hii utalipia nauli, kuni, chumvi na kitunguu), but Tamaa ni mbaya, ukigundulika wataje watahama wote.
. Mwisho Acha ubishoo na kupenda uliko zaliwa/toka..
Jumla ni laki 3, alafu unabakiwa na salio la laki 2 mfukoni