Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Anna Mghwira

R I P
Joined
Mar 9, 2012
Posts
206
Reaction score
362
Leo wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali, Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.

Uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii. Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.

Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi nyingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii.

Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii, wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara.
 
..LOL!!

..lakini sisi tulisema HATUTASAINI na mkataba huo UTATUUMIZA KIUCHUMI.

..and it took us a long time to arrive at that decision.

..tukibadili uamuzi huu basi Tz itakuwa " imeonyeshwa njia."

..zaidi tutakuwa tumekubali KUONGOZWA NA KUSALIMU AMRI KWA NCHI MAJIRANI.
 
Anna Mghwira,

Ni kweli kwa hili namuunga mkono Magufuli japo sikubaliani na mambo yake mengi. Sasa kwenye hili inabidi atumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha anapitia mikataba mingine nchi iliyoingia huko nyuma ili kuona kama ina faida kwa nchi au ilisainiwa na 10%.

Kwa mara ya kwanza nimeona nchi yetu ikisimama kidete dhidi ya mikataba inayotengenezwa ulaya huku ikivalishwa vazi la nia njema.

Sasa tuhakikishe tunapinga mikataba hii lakini tuhakikishe tunajitahidi kujikwamua na hali hii ya kutegemea bidhaa toka nje kwani ninavyojua kuna uwezekano wa nchi hizi za Ulaya kuanza kutupa wakati mgumu.
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi?

Kama hakuna faida kwanini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla?

Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
 
Ngoja ukawa waje wapingane na hili maana kila kitu wanapinga ata kiwe kzuri vipi
 
Asante mtoa mada. Hivi huyu Anna Mghwira ndiye aligombea urais uchaguzi mkuu wa mwaka jana (2015) kupitia ACT Wazalendo au ni mwingine?
 
Msimamo ni kutupilia mbali mkataba. Kwa sasa wako mbioni kutulazimisha chanjo ya ugonjwa wa ZIKA.
 
Heko Mama!

Ila kwa maoni yangu nadhani kuna kama kuviziana au unafiki fulani ktk mambo hasa upande wa masuala yanayohusiana na diplomasia miongoni mwa Nchi wanachama wa Jumuiya yetu pendwa ya EAC na nchi za ng'ambo.

Sisi kama TZ ipo haja ya kutafakari kwa kina kila jambo linaloletwa mezani kuhusu Jumuiya yetu hii. Japo zama zimebadilika natoa rai tuwe makini na katu tusirejelee makosa yaliyo sababisa Jumuiya ya mwanzo kuvunjika na kutuachia makovu hadi leo.

Ujinga ni wakati wa kwenda, ilhali wakati wa kurudi tunajua pema na pabaya.

Mungu ibariki TZ na watu wake, Mungu ibariki EAC, Mungu ibariki Afrika!
 
Back
Top Bottom