Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Kwa kweli nimemkubali Mh Rais katika misimamo yake safii sana maana Tanzania ingekua ndio dampo la bidhaa za nje bila kulipiwa ushuru tungechakaa sana, Hawa wazungu walitaka kutuingiza mkenge, lakini Mh Rais na washauri wake waliliona muda tuu, BIG up Your excellency president Dr JPM
 
Kwa Rais wa Tanzania kuivimbia EU ajiandae nae kuisoma namba.
 
Huu mkataba tukisaini nadhani ile dhana ya "nchi ya viwanda" inaweza kugeuka ndoto, nilimsikia leo Rais akiliongea hili jambo kwa kina...hizi Jumuiya mara nyingine inabidi tu kutofautiana nazo kama haziendani na mipango ya nchi yako.
Mkuu hata kama tusiposaini suala la viwanda its not an overnight issue. Lazima tuwe na mkakati wa muda mrefu tusitegemee 2020 Magufuli akatuonesha viwanda. Namshauri aweke mpango mkakati wa kuwa na viwanda kwa muda hata wa miaka 10 au 15 ijayo.
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi? Kama hakuna faida kwa nini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla? Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
Nchini mwetu hawapewi nafasi kisawasawa katika nchi zilizoendelea hata jambo dogo sana maamuzui mengi yanatokana na wataalamu.
 
Hongera JPM maamuzi mazuri na heri kwa Taifa lets have time first to digest.
 
Rwanda na Kenya watasubiri sana sisi hatusaini ng'oo watajiju nani aliwaambia wakiuke mikataba ya makubaliano katika jumuiya yetu mpaka wakapita mlango wa nyuma na kusaini??! , Hongera Mh Rais wetu,Washauri wako hasa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kikanda na Afrika Mashariki Mwanadiplomasia Nguli Balozi Augustine Mahiga, wataisoma wale waliokua wanasubiri mtego unase waanze pa kusemea katika ofisi Mh Job Ndugai
 
Hongera sana mheshimiwa Rais
Hongera mama Mghwira

Huu mkataba wa EPA ni mkataba wa kilaghai, haufai kabisa.

Huu mkataba ni Strategy ya nchi za Ulaya kuicontain China, Wanataka wajihakikishie soko la bidhaa zao at the expense of our industrial development capacity buildup.

Wazungu wanajua sisi hatuna cha kuoffer kwenye market zaidi ya raw materials tu hahahahaha
 
Tungekuwa na wapinzani wa type hii Tanzania ingekuwa mbali sio wale wa Billcanas kwao kila ifanyacho serikali ni sifuri
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu.

Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi? Kama hakuna faida kwa nini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla? Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?

Wewe hakuna kitu unajua unajiropokea tu, kwenye Mikataba ya kimataifa ni mambo ya kawaida kabisa kuahirisha na kusogeza mbele muda ili kujiridhisha zaidi kumbuka hii ni Mkataba na ina mambo mengi ukiingia hakuna kutoka kirahisi na hii hutokea Dunia nzima nitakupa mifano NAFTA ambayo ni North American free Trade Agreement ilikuwabaliwa tangu mwaka 1994 kati ya USA, Kanada na Mexiko lkn mpaka leo hii bado wanashauriana na bado hawajafikiana na hata D.Trump ameahidi kuiondoa USA ktk NAFTA kama mambo fulani hayajakaa sawa, haya tuje kwenye TTIP (Transantlantic Trade and Investment Partnership) ambapo ni kama vile EPA lkn ni kati ya EU, USA na Kanada mpaka leo hii bado wanavutana, Ulaya imegawanyika na baadhi ya nchi hawataki TTIP baadhi wanataka na mpaka leo TTIP haijasainiwa wakati ilipaswa iwe imeshasainiwa mpaka kufikia mwaka 2014 sasa wanasema hata mpaka kufikia mwaka 2020 itakuwa bado haijasainiwa!

Na hawa ndiyo Wazungu wenye wataalamu wote na mavyuo Vikuu yote na Mabingwa wa Mikataba wako huko lkn pia wanasogeza mbele na kushindwa kukubaliana sembuse sisi third World?

Sasa kwa nini unataka sisi tu rush? Tumia akili kijana acha kushikishwa kichwa na Mbowe, Mbowe ni School drop out hakuna anachojua, Pombe Magufuli (PhD) ni intelligent man na yuko kwa ajili ya manufaa yetu sisi kama nchi, nimekupa hiyo mifano kama school of thought!
 
Mkuu hata kama tusiposaini suala la viwanda its not an overnight issue. Lazima tuwe na mkakati wa muda mrefu tusitegemee 2020 Magufuli akatuonesha viwanda. Namshauri aweke mpango mkakati wa kuwa na viwanda kwa muda hata wa miaka 10 au 15 ijayo.
Nakubaliana nawe hili suala la viwanda sio la kukamilika overnight lakini huu mkataba naona utakuza tu viwanda vya huko ulaya kwa kuwawezesha kuleta bidhaa zao huku with tax exemption, sisi hatuwezi kushindana nao kamwe, tutaishia lada kuuza raw materials halafu wataziprocess kwao na ikiwezekana kuzirejesha huku kama finished products kwa faida maradufu.

Kwa hali hiyo hamna kiwanda hapa nchini kitakachoweza kufunguliwa na kuzalisha bidhaa itakayoshindana na hizo zinazotoka Ulaya tutaishia kuwa dependent on importing goods kutoka nje wakati Rais kwa maono yake anataka sisi tuweze kujihudumia kwa bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu wenyewe mpaka kufikia hatua ya ku-export kwa wengine.

Hayo ni mawazo yangu japo mimi sija-specialize kwenye maswala ya uchumi wenye ujuzi zaidi wanaweza kunirekebisha au kukubaliana nami.
 
Viwanda viko wapi wa kuuza bidhaa labda magwangala kule Geita !!
Mwambie mwenyekiti alipe kodi ya pango kwanza, hiyo na ya wengine itusaidie katika kujenga viwanda na maendeleo mengine
 
Ulaya wenyewe wamegoma Kusaini TAFTA na marekani, Ufaransa kaweka moshi mweusi, sio lazima kusaini mikataba hasa kama unaona wewe hunufaiki chochote
 
Mama Anna Mghwira, kama wanataka free trade ya marchandise basi kuwe na free movement ya watu pia.

Hahahaha, tukiweka ya free movement of people btn East Africa and Europe, lazima watakimbia nduki.
 
Tanzania kugomea au kuwa na mashaka na Mkataba ambao unakwenda kutufunga kwa miaka mingi ijayo ni jambo la muhimuna la kawaida na kila nchi makini kama TZ yetu hufanya hivi!
Hili suala limekuwepo kwa miaka mingi, imekuwaje leo serikali imeshindwa kukataa na kulizika moja kwa moja wameamua kuongeza miezi mitatu, je hawajapitia makabrasha? Je hawajui nini wanataka? Kukwepa kuwajibika ni mojawapo ya sifa ya wapenda sifa wengi, huwa wanaogopa kuwajibika kwa maamuzi yao. Serikali ya awamu ya tano inaogopa kutake risk, ndio maana imeogopa kuupiga chini moja kwa moja mkataba wa EPA leo. What a shame
 
Nimekupa mifano ya Mikataba ya Kimataifa mingi tu ambayo ipo kwa muda mrefu kuliko hata EPA yetu na mpaka leo hii bado majadiliano yanaendelea, sasa kwanini unataka kwetu iwe tofauti?
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi? Kama hakuna faida kwa nini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla? Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
Mtafute Ben Saanane akufundishe lugha ya kidiplomasia
 
Mama Anna kama wanataka free trade ya marchandise basi kuwe na free movement ya watu pia,hahahaha tukiweka ya free movement of people btn East Africa and Europe,lazima watakimbia nduki.
Free movement wakati nchi yako inaonekana ndio ya pili kutoka mwisho kwa skilled manpower afrika mashariki!?

Mtaishia kuondoka na kwenda kufanya kazi za kufagia barabara na kuosha vyombo hotelini huku wao wanakuja huku kuchukua kazi zote za maana.

Kifupi ni kwamba kwa sasa hatuna cha ku offer kwenye hiyo EPA turudi home kujipanga tusubiri viwanda huku tukikamata wanaolala mchana
 
I have no comment. Sijafanya research kujua merits and demerits za EPA.
 
Nimekupa mifano ya Mikataba ya Kimataifa mingi tu ambayo ipo kwa muda mrefu kuliko hata EPA yetu na mpaka leo hii bado majadiliano yanaendelea, sasa kwanini unataka kwetu iwe tofauti?
NAFTA ilishasainiwa siku nyingi sana sana Trump analalamika kuwa nchi yake inapoteza kuliko kupata. By the way sisi tunataka nini kwenye EPA? Maana nisijekuwa nabishana na kopo tupu na mfuniko wake!?
 
Back
Top Bottom