Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Tulichoambiwa na Waziri Mahiga ni kwamba Tanzania ilishaamua haitasaini huo mkataba. Na sababu zikaainishwa. Kwahiyo mama hapa unatuambia kuwa, tulikuwa tumekurupuka, tumetulizwa na wenzetu, tujitafakari mpaka January ndo tuje na uamuzi mwingine.

Mahiga amesema Tanzania haitosaini huo mkataba mpaka itakapojirisha na baadhi ya mambo.

Hivyo hilo neno "mpaka itakaporidhika" linaangukia na huo muda mpaka January.

Lakini haimaanishi kwamba ifikapo January Tanzania itatia saini mkataba huo.
 
Kama Uhuru Kenyatta na Paul Kagame wamesaini basi huo mkataba utakuwa uko vizuri tu make hao wawili ndo marais wenye bongo safi na zinazochemka ukanda huu.
 
Kama Tz ingekuwa makini kuhusu mikabata, leo tusingekuwa na IPTL, RICHMOND, EPA (BOT 2006), meremeta, Tangold, RADAR, mikataba kibao ya madini ni mibovu.

Huo umakini ni upi? Unaweza darasani ukajidai unasomaaa weee kumbe mbumbumbu tu unapoteza muda tu.. na unaweza kujifanya na busara kumbe akili hamna!

So, mm sijaona umakini wowote! Labda na mikataba mingine tulio ingia ingekuwa mizuri hapo sawa, sijaona umakini hata kidogo.
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi?

Kama hakuna faida kwanini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla?

Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?

Ulukolokwitanga: Huna la kujadili ila hoja ya kupinga pasipo na ushahidi kwamba suala la EPA halijafanyiwa utafiti! Du, wewe utafiti umejifunzia wapi!

Kwa kifupi utafiti wowote ni lazima ukubaliwe na watafiti wengine, na wakati mwingine, matokeo ya utafiti mmoja huweza kubatilishwa na tafiti zingine. Kwa hili la EPA mbali na kufanyiwa utafiti lazima likubalike na nchi zote husika. Kwa taarifa ya mtoa mada, Mama Anna, tayari Uganda na Rwanda walikuwa wametia saini. Hivyo kuwaaminisha hadi wakerejea kuutizama upya ni hatua kubwa.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
kama Uhuru Kenyatta na Paul Kagame wamesaini basi huo mkataba utakuwa uko vizuri tu make hao wawili ndo marais wenye bongo safi na zinazochemka ukanda huu

Ingawa wamesaini kabla raisi Magufuli hajaingia Ikulu.
 
haibadirishi mkataba, mkataba ni uleule

Mkuu, kumbuka mikataba yote ambayo ilikuwa ikisainiwa huko nyuma na hatukusikia mawaziri wetu wakisema wanataka muda ili kuipitia.

Unaweka kukumbuka mkataba hata mmoja ikianzia Buzwagi?
 
Mkuu, kumbuka mikataba yote ambayo ilikuwa ikisainiwa huko nyuma na hatukusikia mawaziri wetu wakisema wanataka muda ili kuipitia.

Unaweka kukumbuka mkataba hata mmoja ikianzia Buzwagi?

Wewe nishakuambia ukiona kagame kasaini jua huo na mkataba swafi, we ushaona kwa kagame kuna mikataba ya kibuzwagibuzwagi.
 
Ni hatua ya kushangaza kidogo lakini si vibaya ku fanya tena mazungumzo kama tunazo point ambazo zitatupa faida zaidi au kama kama kama kuna kipengele ambacho sio rafiki na nchi zetu.
sababu za UK kujitoa EU hazina msingi.

kurejea moja ya kifungu kilichopo kwenye huu mkataba ni kuhusu haki za binadamu kwa nchi husika...isije kuwa kimetukimbiza.
12. A clause linking the EPA to the Cotonou Agreement and its essential elements such as
human rights, democracy and the rule of law;

Kwa ajili ya Kujadiliana vizuri na Mama mwingira kwa hoja zake ni vyema kila mmoja akasoma makataba wote unasema nini ili tujue wapi unatubana na wapi tuurekebishe. naweka hapa chini agreement hizo kama zilivo wekwa kwenye tovuti ya EAC...
Kuna points muhumu na makataba mzima. TUOSOME KWA MAKINI ILI TUSAIDIE KUPATA BENEFIT STAHIKI...POINT YA KUKUMBUKA HUU NI MKATABA WA PANDE MBILI HIVYO USIEGEMEE UPANDE MMOJA. KILA MMOJA LAZIMA APATE FAIDA YA MASHIRIKIANO...SOMENI...
KWA SABABU YA UKUBWA WA FAILI NIMEWEKA EPA 1-150 , EPA 151-350 AND EPA 351-640
 
Attachments

wewe nishakuambia ukiona kagame kasaini jua huo na mkataba swafi, we ushaona kwa kagame kuna mikataba ya kibuzwagibuzwagi.
Ni kweli, Tanzania itajengwa na Rwanda
 
Hatuna cha kuuza Ulaya. Kenya wanauza sana maua na mboga sasa sisi tusaini tuuze nini? Uliza ile ya USA inaitwa AGO kama kuna tunacho uza
Hii ni zaidi ya hivyo mkuu.
Pale Kenya wanaouza ni wazungu ingawa wafrika Wakenya wapo lkn ukiangalia kinachopiganiwa hapo ni zaidi ya hicho kitu.

Wanachotaka ni kurudi kama kule Zimbabwe ilivyokuwa.

Hawa wazungu wanazagaazagaa huku mitaani ndiyo wanaotumwa kuja kufanya research nchi nzima wakishirikiana na wale wabobezi wa miaka nenda rudi
 
Lakini hao wanaouza huko Ulaya ni wazungu wakenya wenye connections.

Mwafrika hapati kitu hapo.
Kwani EPA ni mkataba wa kibiashara unaohusisha ukanda na ukanda? Au race na race?

....mmewaruhusu wawekezaji waje nchini mwenu kwa masharti fulani sasa hiyo EPA itakuwa nje ya masharti muhimu ya msingi?
 
kama Uhuru Kenyatta na Paul Kagame wamesaini basi huo mkataba utakuwa uko vizuri tu make hao wawili ndo marais wenye bongo safi na zinazochemka ukanda huu
Inferiority complex ya kiwango cha lami
 
Ulukolokwitanga: Huna la kujadili ila hoja ya kupinga pasipo na ushahidi kwamba suala la EPA halijafanyiwa utafiti! Du, wewe utafiti umejifunzia wapi!

Kwa kifupi utafiti wowote ni lazima ukubaliwe na watafiti wengine, na wakati mwingine, matokeo ya utafiti mmoja huweza kubatilishwa na tafiti zingine. Kwa hili la EPA mbali na kufanyiwa utafiti lazima likubalike na nchi zote husika. Kwa taarifa ya mtoa mada, Mama Anna, tayari Uganda na Rwanda walikuwa wametia saini. Hivyo kuwaaminisha hadi wakerejea kuutizama upya ni hatua kubwa.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Wanarudia kuutizama? Au wanawasubiri wasiosaini kwa vile ni mkataba kati ya union na union na sio single countries?
 
Leo wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali, Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.

Uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii. Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.

Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi nyingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii.

Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii, wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara.
Vizuri Mama wa Heshima
 
Anna Mghwira,

Ni kweli kwa hili namuunga mkono Magufuli japo sikubaliani na mambo yake mengi. Sasa kwenye hili inabidi atumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha anapitia mikataba mingine nchi iliyoingia huko nyuma ili kuona kama ina faida kwa nchi au ilisainiwa na 10%.

Kwa mara ya kwanza nimeona nchi yetu ikisimama kidete dhidi ya mikataba inayotengenezwa ulaya huku ikivalishwa vazi la nia njema.

Sasa tuhakikishe tunapinga mikataba hii lakini tuhakikishe tunajitahidi kujikwamua na hali hii ya kutegemea bidhaa toka nje kwani ninavyojua kuna uwezekano wa nchi hizi za Ulaya kuanza kutupa wakati mgumu.
Nz vipi kuhusu mikataba mibovu na ya siri ambayo serikali imekwisha sign kwa mfano ya madini na Richmond?
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi?

Kama hakuna faida kwanini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla?

Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?

Umenena vyema mkuu. Na haya majadiliano yameanza miaka 14 iliyopita. Ni kitu gani kimejificha mpaka tutumie muda wote huu kujadili haya makubaliano?

Namshukuru Mkapa alishaliona na kutangaza wazi kwamba haungi mkono. Kama kitu hakina tija kwanini tunatumia muda kujadili badala ya kufanya mambo ya maana. Au delay tactics za wakuu wa nchi wakiogopa kunyimwa misaada? Siyo mtaalam wa uchumi lakini sioni kwamba hili linahitaji shahada ya uchumi kulielewa.
 
..LOL!!

..lakini sisi tulisema HATUTASAINI na mkataba huo UTATUUMIZA KIUCHUMI.

..and it took us a long time to arrive at that decision.

..tukibadili uamuzi huu basi Tz itakuwa " imeonyeshwa njia."

..zaidi tutakuwa tumekubali KUONGOZWA NA KUSALIMU AMRI KWA NCHI MAJIRANI.
Kamwe hatutasaini
Mkutano ulikuja kwa presha za kenya na Rwanda ambao wamefeli baada ya kukurupuka.
Tumepiga teke hadi 2017,kwa kua tutakuwa back benchers,utaona vumbi tutakalotimua
 
Back
Top Bottom