Mwaka 2014 Jumuiya ya Afrika Mashariki ilisaini makubaliano na European Union, wataalamu wa uchumi wa nchi hii hawakutoka na kueleza nini faida au hata kama kuna hasara katika makubaliano hayo.
Hapa ndipo elimu zetu na vyeti vinapopoteza maana, maana anavyoongea mtaalam wa uchumi na biashara na anavyoongea mtu asiye na weredi kwenye maeno haya ni kama sawa tu, wote wanabuni?
Niliwahi kumuuliza afisa mmoja wa serikali anaelewa nini kuhusu EPA? Hakuwa na majibu zaidi ya kutoa hisia zake na mambo aliyoyasikia kwenye magazeti.
Sasa kama maafisa kama hawa ndio wanamshauri rais katika mambo ya kiuchumi bado tuna safari ndefu.
Nisiingie kwenye maamuzi yaliyofanyika hivi karibuni lakini embu tujiulize maswali machache
1. Unaweza kuepuka kufanya biashara na European Union?
2. Wangapi wetu tumesoma makubaliano ya awali kati EAC na EU yaliyofanyika miaka miwili iliyopita? soma hapa
http://trade.ec.europa.eu/doclib/docs/2015/october/tradoc_153845.compressed.pdf
3. Bidhaa/ biashara kutoka East African Community kwenda nchi za Umoja wa Ulaya ni kahawa, maua, chai, kahawa, samaki na mbogamboga - Hii ni exports, je nchi yetu ni shindani katika kuzalisha mazao hayo ukilinganisha na nchi nyingine za Africa Mashariki?
4. Bidhaa kutoka EU kuja EAC ni mashine na mitambo, vifaa vya viwandani na ujenzi, magari na vifaa vya tiba na madawa - Je kwenye njozi yetu ya kuwa na uchumi wa viwanda hatuhitaji EPA? Au tutatumia zana za mawe?
Note: Kilimo kinachangia asilimia 24.5 ya GDP
Viwanda na ujenzi asilimia 22.2
Haya ni maeneo ambayo wataalamu wa uchumi wa serikali hii wangeweka focus yao hapo, na kupima kama EPA itakuwa na faida kwa upande wetu.
Nimetimiza wajibu wangu wa kuchangia kwa mustakabali mwema kwa taifa letu.