Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.
Kwa sie tulioanza kufuatilia suala la EPA zaidi ya miaka 5 iliyopita inakera sana tena sana kusikia eti "...hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu!" Mtu mwingine anaweza kudhani suala la EPA ni jambo jipya kumbe lina miaka na miaka sasa!! Ina maana hadi leo Waheshimiwa wetu walikuwa hawafanya tathminini kufahamu faida na hasara za EPA?! Nilitarajia kwa ile jana iwe ni YES au NO, PERIOD... kumbe bado tunatafakari kufahamu pros and cons!!!!

Mkataba wa EPA ni mzuri lakini unaonekana ni mbaya na YES, kwetu ni mbaya au hauna manufaa si kwa sababu EPA as EPA ni mbaya bali ni sisi wenyewe ndio tuna akili mbaya! Tusingekuwa na akili mbaya EPA ingekuwa ni opportunity! We have a lot to sell to EU but we don't know which among them! A country like Tanzania with abundant and virgin land ni kufuru kwa Mwenyezi Mungu hadi leo tunalilia kwamba sisi hatuna cha kuuza EU... community iliyojaa junk and inorganic produces everywhere wakati sisi tukiwa na uwezo na kuzalisha organic produces at minimal cost ambazo ni valuable anywhere na kuweza kulisha the whole of EU!!! Hapa napo Watendaji wa Serikali watalia lia kwamba ni ngumu ku-compete na European Farmers kwa sababu wanapewa subsidize... so why don't you offer the same kwa wakulima wenu?!
 
Woga wa kufanya maamuzi tu,yani for more than five years tulikuwa hatujapambanua faida na hasara za haya makubaliano!!!!!watu vilaza humu,eti nampongeza rais kwa kukataa kusaini!!!amekataa au ameahirisha!
 
Umenena vyema mkuu. Na haya majadiliano yameanza miaka 14 iliyopita. Ni kitu gani kimejificha mpaka tutumie muda wote huu kujadili haya makubaliano?

Namshukuru Mkapa alishaliona na kutangaza wazi kwamba haungi mkono. Kama kitu hakina tija kwanini tunatumia muda kujadili badala ya kufanya mambo ya maana. Au delay tactics za wakuu wa nchi wakiogopa kunyimwa misaada? Siyo mtaalam wa uchumi lakini sioni kwamba hili linahitaji shahada ya uchumi kulielewa.
Jee mkapa alitoa sababu gani za kukataa ? Jee sio viwanda vya sukari vya masahibu wake ?
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi?

Kama hakuna faida kwanini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla?

Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
Mkuu upo sahihi 100 %!!

Yaani mkataba umekuja siku zote hiz mpaka wameupitia lakini mpaka sasa hawajui faida na hasara zake. Hicho ni kichekesho cha mwaka!!

Kwa kweli kwenye mkutano kama huu walitakiwa waseme tumekataa kusaini mpaka vipengere fulani vilekebishwe au tujadiliane na kukubaliana siyo hii mpaka tujiridhishe!! Sasa kama wameshindwa kuona faida na hasara zake kwa kipindi chote hicho hiyo miezi mitatu waliyojipa nini kitabadilika?? Labda kama itabidi wabadili team ya wataalamu!!

By the way, hivi ni Mkataba gani mzuri ambao nchi yetu imesaini miaka ya karibuni kuanzia enzi za TPIL. Mwenye kumbukumbu atusadie!!
 
Free movement wakati nchi yako inaonekana ndio ya pili kutoka mwisho kwa skilled manpower afrika mashariki!?

Mtaishia kuondoka na kwenda kufanya kazi za kufagia barabara na kuosha vyombo hotelini huku wao wanakuja huku kuchukua kazi zote za maana.

Kifupi ni kwamba kwa sasa hatuna cha ku offer kwenye hiyo EPA turudi home kujipanga tusubiri viwanda huku tukikamata wanaolala mchana
Nimefuatilia michango yako hapa inaonekana wewe una jambo lingine nje ya hii mada. Hilo ndio linakusukuma kuchangia hapa
 
Ninafikiri tofauti.

Sisi tuko mkutano tofauti Arusha lakini tujadili mambo haya yaliyotokea Dar Es Salaam leo:

Kuahirisha kusaini: Kwa jinsi ya mazungumzo hapa, si rahisi asaini, kwa sababu hata Kenya iliyosaini, watu wake wanakataa kwa kigezo kuwa makampuni ya Kikenya yanayoletea uhalali wa kuingia mkataba, ni ya wageni. wakenya wanasema biashara kubwa inayounganishwa na mkataba ni biashara ya maua.

Kwa hali hiyo mashamba mengi - 85% si ya Wakenya:
Wanasema ni kama Ulaya inafanya biashara yenyewe kupitia Kenya ama Afrika Mashariki. Mwakilishi wa Rwanda katika mkutano huu alitaka kuingiza dhana ya kusema Rwanda ilisaini kwa niaba ya ukanda kwa sababu hii mikataba yote inapaswa kuingiwa kwa makubaliano. Wajumbe toka kwenye ukadna wote tulikataa.

Kujipa muda kujibu ni hatua nzuri:
Mpaka sasa tafiti hazioneshi faida. Zinaonesha hasara, lakini inahitaji maridhiano ya wote. Ndio sababu wa kuhitaji muda zaidi.
Ni vyema zaidi kama uwakilishi wenu utaleta manufaa kwa Tanzania yetu
 
Jana wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali, Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.

Uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii. Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.

Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi nyingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii.

Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii, wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara
 
Mama Anna Mghwira, kama wanataka free trade ya marchandise basi kuwe na free movement ya watu pia.

Hahahaha, tukiweka ya free movement of people btn East Africa and Europe, lazima watakimbia nduki.
Hapo nilipo bold nmepapenda sana, lazima wakimbie maana sio kwa utitiri wa watu watakao kimbiliaaa europe kutoka east africa hasa TZ hahahahahhahahhah.
 
Mkuu you nailed it...hata huko EU ni mbali kwa vigin land tulionayo inatosha Kabisa kututajirisha kwa kulisha majirani Zetu tu...tatizo hapa ni kutawaliwa na watawala wale wale wenye mawazo na akili zile zile kwa miaka hamsini..

Wananchi wa Kenya nao wanalalamika kuwa watakachouza EU sana sana ni maua na maua yenyewe wanaolima 85% ni kampuni za kigeni..

Kwa sie tulioanza kufuatilia suala la EPA zaidi ya miaka 5 iliyopita inakera sana tena sana kusikia eti "...hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu!" Mtu mwingine anaweza kudhani suala la EPA ni jambo jipya kumbe lina miaka na miaka sasa!! Ina maana hadi leo Waheshimiwa wetu walikuwa hawafanya tathminini kufahamu faida na hasara za EPA?! Nilitarajia kwa ile jana iwe ni YES au NO, PERIOD... kumbe bado tunatafakari kufahamu pros and cons!!!!

Mkataba wa EPA ni mzuri lakini unaonekana ni mbaya na YES, kwetu ni mbaya au hauna manufaa si kwa sababu EPA as EPA ni mbaya bali ni sisi wenyewe ndio tuna akili mbaya! Tusingekuwa na akili mbaya EPA ingekuwa ni opportunity! We have a lot to sell to EU but we don't know which among them! A country like Tanzania with abundant and virgin land ni kufuru kwa Mwenyezi Mungu hadi leo tunalilia kwamba sisi hatuna cha kuuza EU... community iliyojaa junk and inorganic produces everywhere wakati sisi tukiwa na uwezo na kuzalisha organic produces at minimal cost ambazo ni valuable anywhere na kuweza kulisha the whole of EU!!! Hapa napo Watendaji wa Serikali watalia lia kwamba ni ngumu ku-compete na European Farmers kwa sababu wanapewa subsidize... so why don't you offer the same kwa wakulima wenu?!
 
Ni vema kufanya hivyo lakini ifike mahala tubadilishe sheria zetu zinazo ongoza michakato ya mikataba yetu ili mikataba hiyo inakuwa wazi na Wananchi wanapewa furusa ya kuijadili ili waweze kunufaika nayo.
 
Nimejaribu kufuatilia kidogo, hii kitu inaitwa Economic partnership agreement( EPA) ambayo kimsingi ni makubaliano ya kibiashara, kati ya nchi za Jumuiya ya Ulaya( EU) na nchi za Afrika, Caribbean na pacific( ACP)

Kwa kweli naunga mkono, tena kwa dhati msimamo wa serikali yetu Tanzania, kwa kutokukubali kusaini makubaliano hayo kwa sasa

Kwani, kwa kusaini makubaliano hayo, kwa mtizamo wangu, itahatarisha adhama ya serikali yetu, ya kuifanya nchi yetu kuwa ya uchumi wa viwanda ifikapo 2025

Pia makubaliano haya , ni hatari kwa mustakabali wa sisi wazalishaji wa bidhaa ndogo za ndani na pia wakulima wa Tanzania kwa ujumla, hasa ukizingatia nchi za ulaya utoa ruzuku kwa wakulima wao

Pia ukiangalia manufaa amabyo sisi kama Tanzania tutapata, tayari tunayapata kwenye makubaliano kama, African Growth and Opportunity Growth Act( AGOA),

Kwa hiyo kiufupi, makubaliano haya yatazinufaisha zaidi nchi za ulaya na kuzidi kudidimiza uchumi wa nchi zetu za kiafrika
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi?

Kama hakuna faida kwanini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla?

Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
Wewe ndio mzigo....unadhani faida na hasara za kitu ni static??

Sasa hivi tunaijadili EPA kwa muktadha wa ki-brexit na mambo kama hayo ...hii ni tofauti na miaka kadhaa nyuma....

sasa hivi tunaijadili EPA kwa muktadha wa sera ya viwanda nchini....hili halikuwepo 14 years ago.

Wewe ndio kiilaza na mzito wa kuelewa
 
Anna Mghwira: Nimesoma post yako mara kadhaa na kwa kina. Lakini sijaweza kupata ujumbe uliotaka kuupeleka. Je ulitaka tu kutaarifu wana JF kuwa umehudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa EAC, licha ya kuwa Kiongozi wa Chama cha Upinzani? (By the way, vyama vingine vya siasa vilialikwa kwenye mkutano huo? ODM? FDC? CUF?) Au ulitaka kusema kuwa kutokana na ushawishi wako, Wakuu hao wameahirisha (si kukataa) kusaini EPA? Au ulitaka kutuambia kwamba Wakuu hao wamekutana kwa lengo la kusaini EPA bila kujua faida na hasara zake? Au kwamba ulitarajia nchi washirika zitapingana na msimamo wa Tanzania kuhusu EPA na hivyo unashangaa kuwa nao wamekubali kujipa muda zaidi kutafakari jambo hilo? Msimamo wa Tanzania ni kutosaini Mkataba huo. Kwa nini unasema kuwa Tanzania imeheshimika kwa kuwa tu tarehe ya kusaini imeahirishwa? Kwani baada ya miezi mitatu, ni nini kitabadilika? Je, muda huo ukiisha Tanzania itakuwa tayari kusaini Mkataba huo? Au Kenya na Rwanda ambazo zimeshaini, zitabadili msimamo wao?
 
Kwa sie tulioanza kufuatilia suala la EPA zaidi ya miaka 5 iliyopita inakera sana tena sana kusikia eti "...hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu!" Mtu mwingine anaweza kudhani suala la EPA ni jambo jipya kumbe lina miaka na miaka sasa!! Ina maana hadi leo Waheshimiwa wetu walikuwa hawafanya tathminini kufahamu faida na hasara za EPA?! Nilitarajia kwa ile jana iwe ni YES au NO, PERIOD... kumbe bado tunatafakari kufahamu pros and cons!!!!

Mkataba wa EPA ni mzuri lakini unaonekana ni mbaya na YES, kwetu ni mbaya au hauna manufaa si kwa sababu EPA as EPA ni mbaya bali ni sisi wenyewe ndio tuna akili mbaya! Tusingekuwa na akili mbaya EPA ingekuwa ni opportunity! We have a lot to sell to EU but we don't know which among them! A country like Tanzania with abundant and virgin land ni kufuru kwa Mwenyezi Mungu hadi leo tunalilia kwamba sisi hatuna cha kuuza EU... community iliyojaa junk and inorganic produces everywhere wakati sisi tukiwa na uwezo na kuzalisha organic produces at minimal cost ambazo ni valuable anywhere na kuweza kulisha the whole of EU!!! Hapa napo Watendaji wa Serikali watalia lia kwamba ni ngumu ku-compete na European Farmers kwa sababu wanapewa subsidize... so why don't you offer the same kwa wakulima wenu?!
Umenena vyema...Kama Kenya wanauza maua Ulaya...Kwa nini na sisi tusiuze huko Ulaya?
 
Watanzania kama wamerogwa ili wawe na mitazamo hasi kila Mara...

Tupo nyuma na tumechelewa , yote ni sawa lakini je ,hatuwezi kuanza tena kama nchi !!!!........

Je, hatuwezi kufanya yaliyo sawa kwa sasa kwa kuwa tuna historia mbovu ya mikataba ????....

EPA haina maana kwa nchi yetu kwa sasa kwa kuwa kama LDC bado tuna access na soko LA EU kwa vikwazo vidogo vya kibiashara lakini Kenya ina uchumi wa kati hivyo , huwekewa kodi kubwa zaidi na hii ndio maana imeonesha nia kubwa kuliko nchi zinginezo za EAC ...

Tunaitamani nchi ya viwanda lakini hili haliwezi kutokea kama hatutovilinda viwanda vyetu vidogo vilivyopo na vitakavyoanzishwa dhidi ya bidhaa za nje..

Pia tutaendelea kuikumbatia hii hali ya kuuza vitu vyenye thamani ndogo katika soko LA kimataifa huku tukigeuzwa dampo LA bidhaa zao hadi lini ????...

Hatua moja huanzisha nyinginezo
 
Leo wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali, Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.

Uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii. Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.

Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi nyingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii.

Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii, wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara.

Mama yetu tungependa tuelewe na sisi wananchi mkataba wa epa ndio nini na nini kimetufanya tukatae kuusaini kwa sasa. ila usisifu tu kwa kuwa umehudhuria wewe. nimechoka kusikia wewe na chama chako mnaitwa CCM B
 
Back
Top Bottom