Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA, Tanzania tumeonesha njia

NAFTA ilishasainiwa siku nyingi sana sana Trump analalamika kuwa nchi yake inapoteza kuliko kupata. By the way sisi tunataka nini kwenye EPA? Maana nisijekuwa nabishana na kopo tupu na mfuniko wake!?


Hilo swali kawaulize wahusika, na isitoshe Mama Mghwira amesema atakuja hapa na kuandika kirefu zaidi hivyo utapata muda muafaka wa kusoma kama ukiweza na kuuliza maswali!!
 
Hili suala limekuwepo kwa miaka mingi, imekuwaje leo serikali imeshindwa kukataa na kulizika moja kwa moja wameamua kuongeza miezi mitatu, je hawajapitia makabrasha? Je hawajui nini wanataka? Kukwepa kuwajibika ni mojawapo ya sifa ya wapenda sifa wengi, huwa wanaogopa kuwajibika kwa maamuzi yao. Serikali ya awamu ya tano inaogopa kutake risk, ndio maana imeogopa kuupiga chini moja kwa moja mkataba wa EPA leo. What a shame
Kwa nini unasema ni makataba?

Kitu ambacho hakijasainiwa hakiwezi kuwa ni mkataba.

Kilichopo kwa sasa ni proposal ya Economic Partnership Agreement ambayo inaweza kubadilishwa kulingana na makubaliano ya pande zote kabla ya kuwa signed and ratified.

Kwa maana nyingine, majadiliano bado yanaendelea kwa sababu msingi wake ni diplomasia pamoja na kwamba EU wanatumia bullying economic diplomacy technique.
 
Yakiwa yamebanwa kati ya mwamba na mahali pagumu, mataifa ya Afrika na Pasifiki bado hayana uhakika kama yafuate wenzao wa Caribbean na kusaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Ulaya (EPA). na hiki ndio kipimo pekee cha KATI nilichobakisha kumpima John Magufuli na timu yake ya ushauri wa Masuala mbalimbali ya kiuchumi na kidplomasia.

Hakika Umoja wa Ulaya unayatumia madhaifu ya nchi za Africa kuzilazimisha ziusaini Mkataba huu mbovu ambao ni Mwiba mchungu kwa Maendeleo na kujitegemea kwa nchi za bara hili.
 
Napendekeza Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, atumie uwezo wake, kikatiba, kutoa nafasi yake moja ya uteuzi kwa huyu mama kuwa mbunge.

Japo sio CCM mwenzetu natumaini nafasi haitakuwa imepotea maana hata anapokosoa anatumia lugha ya kistaarabu na vilevile anatoa masuluhisho ambayo yanaweza kuleta manufaa kwa taifa!
 
Alaaa kumbe mama Mghwira upo huku?

Naomba nikueleze tu kuwa Magufuli atake asitake huo mkataba atasaini tu!! Wenzake Kenyatta na Museven ndo wameshinikiza hilo na hicho kikao cha dharura ni kuweka mambo sawa.
Ninafikiri tofauti.

Sisi tuko mkutano tofauti Arusha lakini tujadili mambo haya yaliyotokea Dar Es Salaam leo:

Kuahirisha kusaini: Kwa jinsi ya mazungumzo hapa, si rahisi asaini, kwa sababu hata Kenya iliyosaini, watu wake wanakataa kwa kigezo kuwa makampuni ya Kikenya yanayoletea uhalali wa kuingia mkataba, ni ya wageni. wakenya wanasema biashara kubwa inayounganishwa na mkataba ni biashara ya maua.

Kwa hali hiyo mashamba mengi - 85% si ya Wakenya:
Wanasema ni kama Ulaya inafanya biashara yenyewe kupitia Kenya ama Afrika Mashariki. Mwakilishi wa Rwanda katika mkutano huu alitaka kuingiza dhana ya kusema Rwanda ilisaini kwa niaba ya ukanda kwa sababu hii mikataba yote inapaswa kuingiwa kwa makubaliano. Wajumbe toka kwenye ukadna wote tulikataa.

Kujipa muda kujibu ni hatua nzuri:
Mpaka sasa tafiti hazioneshi faida. Zinaonesha hasara, lakini inahitaji maridhiano ya wote. Ndio sababu wa kuhitaji muda zaidi.
 
Hapa tumehoji kwa nini EPA zinaeleza faida zake kwa afrika, hazielezi faida na hasara kwa Ulaya. hatukupata jibu. Hata hivyo ni wazi kuwa hasara inaonekana waziwazi. Waliosaini nao wanaona mapungufu.
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi? Kama hakuna faida kwa nini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla? Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
Shida ni kwamba Tanzania haina vya kuuza nje .
 
Mkuu Ulukolokwitanga, unachanganya mada.

Sisi tuko Arusha kwa mkutano wa asasi zisizo za kiserikali zaidi, wawakilishi wa vyama vya siasa, wabung toka afrika mashariki na umoja wa ulaya, wana azaki toka nchi mbalimbali lakini hasa wadau wa maendeleo toka ukanda wa Ulaya na afrika mashariki.

Walioahirisha kusaini mpaka Januari ili kujiridhisha ni wakuu wa nchi katika mkutano wao wa dharura Dar Es Salaam.

Tulioko Arusha tumeridhishwa na taarifa ya kusitisha kusaini ili kila nchi na Jumuiya kujiridhisha kabla ya kuweka msimamo wa mwisho.

Jukumu la sasa kwa maoni yangu ni wakuu wa nchi na hasa Tanzania kutoa wigo mpana wa ushirkishwaji wakati wa kipindi cha mpaka Januari wengi wetu tuwe tumeelewa maana, sababu na msingi wa maamuzi.

Tafiti zipo nafikiri ni suala la kuzipitia na kufikia maamuzi. Muda huu unaweza pia kutumika kupitia mikataba mingine ambayo imetuletea hasara, ili kuweka utaratibu mzuri zaidi wa kuingia mikataba ya aina hii.
 
Imekuwa tena mpaka January ... siyo kwamba tulishaamua hatusaini?
 
Shida ni kwamba Tanzania haina vya kuuza nje .
Hilo ni jambo jingine, kusitisha ni lingine pia. Tusichanganye ili kujipa fursa kuelewa kila hatua. Kwa hiyo tusiposaini tunajipa muda kujipima. Tukisaini tunajinyima hata hiyo fursa.

Hata hivyo, tuna kazi kubwa zaidi kuhakikisha uzalishaji wa ndani unakua na biashara za ndani zinachangamka.
 
Tulichoambiwa na Waziri Mahiga ni kwamba Tanzania ilishaamua haitasaini huo mkataba. Na sababu zikaainishwa. Kwahiyo mama hapa unatuambia kuwa, tulikuwa tumekurupuka, tumetulizwa na wenzetu, tujitafakari mpaka January ndo tuje na uamuzi mwingine.
 
Hatuna cha kuuza Ulaya. Kenya wanauza sana maua na mboga sasa sisi tusaini tuuze nini? Uliza ile ya USA inaitwa AGO kama kuna tunacho uza
 
Duh hapo ndio ninapochoshwa na wasomi wa nchi hii, inakuwaje mpaka leo hamjafanya utafiti kujua faida na hasara za EPA? Kichekesho cha hali ya juu. Kweli kabisa mwenyekiti wa chama unatoka kwenye mkutano unajisifu kuwa hamjui faida au hasara za EPA na kujipa muda zaidi? Kama hakuna faida kwa nini msionyeshe msimamo na kukataa na kama kuna faida kwa nini msikubali? Je hili suala la EPA limekuja Ghafla? Nyie wanasiasa a wasomi msiofanya utafiti na msiojua wajibu wenu ni mizigo na majanga ya kitaifa. Kufanya utafiti kuhusu EPA mnaitaji miezi mitatu, are you serious?
You have said, tunashangilia badala ya kushangaa!
 
Ngoja ukawa waje wapingane na hili maana kila kitu wanapinga ata kiwe kzuri vipi

Sisi ukawa tunapinga hii hatua kwani itaonyesha watanzania tunauoga.

Hivyo msimamo wetu ni kusaini mkataba ili tuonyeshe tunaubavu wakushindana.

Hivyo nadhani tarehe moja ukawa utatoa msimamo wa kupinga hatua hii
 
Leo wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameamua kwa pamoja kusitisha kuweka sahihi mkataba wa EPA hadi Januari mwakani. Awali, Kenya na Rwanda walikuwa wamekwisha weka sahihi mikataba hii.

Uamuzi huu unaziweka nchi za ukanda huu katika nafasi salama ya kutafakari na kupima faida na hasara za kusaini mikataba hii. Tayari Tanzania imeonesha mfano kwa kusita kuingia makubaliano hadi itakapojiridhisha kuhusu faida na hasara za mkataba huu.

Nimehudhuria mkutano wa ukanda kuhusu mkataba wa EPA Afrika Mashariki na kupata nafasi kujadili mambo haya wakati wakuu wa nchi wakiweka misimamo yao. Umekuwa wakati muafaka kwa matukio haya.

Kwa kusita kusaini na kuzishawishi nchi nyingine kusubiri, Tanzania imeonesha njia katika kusimamia mikataba ya aina hii.

Nitakuja na taarifa ndefu zaidi lakini kwa hatua hii, wenzetu toka nchi jirani wametuheshimu. Tutunze heshima hii na kuendelea kuonesha njia sahihi katika masuala ya diplomasia ya biashara.
Mama ubarikiwe sana
 
Hatuna cha kuuza Ulaya. Kenya wanauza sana maua na mboga sasa sisi tusaini tuuze nini? Uliza ile ya USA inaitwa AGO kama kuna tunacho uza

Lakini hao wanaouza huko Ulaya ni wazungu wakenya wenye connections.

Mwafrika hapati kitu hapo.
 
Mama Anna Mghwira kwanza hapa ungeelezea EPA ni nini, madhumuni yake ni yapi, masharti yake ni yapi, na ugumu wa Tanzania katika kuyatekeleza hayo masharti ukoje,
 
Back
Top Bottom