KERO Nimeibiwa kamera Tabata, sikupata msaada stahiki Kituo cha Polisi Stakishari. Mwizi anajulikana maeneo yale, amefanya tukio jingine na bado anapeta tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Yaani kesi ya kibaka unampelekea jambazi unategemea nini?

Ila kiukweli haya mambo ya polisi tuendelee kuyasikia tu usiombe siku uwe na shida na kutaka msaada kutoka kwao ndio utawajua vizuri hawa wapumbavu
 
Ukiibiwa nenda polisi kwaajili ya kutoa taarifa tu, chukua RB sepa.
Pambana Kimya Kimya.
Polisi bongo ni wezi na dhulma.
Ukijichekesha polisi wanakuongezea majereha kuliko ya Kibaka.
Hela watachukua na muda utapoteza.
Hatari za kuwa Whistle Blowers.jpg
 
Ndio maana nawachukia wezi.. Mwizi anapokuibia anakuletea matatizo tu.. Hata ukienda polisi nao badala ya kufanya kazi yao ndio wanaona ATM imejileta.. Huku kwetu tunawabanika tu ili wengine wajifunze .
 
Nimesoma maelezo yote, kwanini usiwabane wale wenye nyumba aliyoingia huyu mkaka? Wale ndo wanatakiwa waelezee kwa kina, nahisi hao ndo wanajua kila kitu.

Alitoka vipi? Na alitokea wapi? Km alitokea mlango mwingne wao walikua wapi wasimuonee? Aseeeh unge deal na wenye nyumba kwanii.

Poleee Mr, ila utapata [emoji328] yako usijarii.
Babu uswahilini unaweza pita nyumbani kwa mtu hata sio mwenu na usiulizwe kitu.
 
NIkushauri jambo zuri.

Kesho ni jumaa mubarak, nitaenda kuswalisha katika msikitini Fulani, je upo tayari kumdhuru mwizi wako kwa kumtupia jini baya la maangamizi ya maradhi, kama upo tayari niambie nisome dua kesho masjid. 😃😃😃
 
Au aende Nachingwea kule kuna fundi mmoja, wamama wa mjini Daslamu na Unguja wanamtumia sana kupora waume za watu. Fundi mwenyewe ni wale waganga ambao wanaua kabisa yani jina lako likipelekwa kwake leo basi kesho unazikwa.
Hahaa mkuu noma sana . Huyu Babu hataki uite albadili wanaita kumshtakia Mungu
 
Njoo Tanga Kuna jirani yangu anasoma albadili siku moja tu majibu utayapata na Kwa vile picha unayo wapewe taarifa Kwa ndugu na watu wanaomjua mpe siku tatu tu . Tafuta nauli ya kujia tu kurudi nitakupa na Babu atalipwa na ndugu na jamaa wa karibu na huyo mwizi
Mkuu kama ni serious funguka kuna watu walitupiga matukio ya hatari
 
Njoo Tanga Kuna jirani yangu anasoma albadili siku moja tu majibu utayapata na Kwa vile picha unayo wapewe taarifa Kwa ndugu na watu wanaomjua mpe siku tatu tu . Tafuta nauli ya kujia tu kurudi nitakupa na Babu atalipwa na ndugu na jamaa wa karibu na huyo mwizi
Ndugu wa mwizi watalipa kivipi na kwa njia gani?
 
Au aende Nachingwea kule kuna fundi mmoja, wamama wa mjini Daslamu na Unguja wanamtumia sana kupora waume za watu. Fundi mwenyewe ni wale waganga ambao wanaua kabisa yani jina lako likipelekwa kwake leo basi kesho unazikwa.
😀😀😀😀😀😀Yaani jina likipelekwa tu watu kesho wanafunga Maturubai na kula wali maharage bure
 
pole sana bro,.,.,.,.
yaani hiyo namba ya simu tu inatosha kumkamata....hapo unmtafuta kimafia halafu mnamalizana
naomba mungu yasinikute maana mimi hapo ndio ntaishia jela
NB: ushauri wangu fanya hata kukopa hyo 60 ya askari huyo anakamatwa siku 2 tu,kama ni ngumu bas muachie mungu.
POLE SANA
Rahisi huyu kumdaka, awe na Rb yake tu mfukoni amsake kwenye mabaa ya Tabata na huko Kinyerezi..
 
Habari JamiiForums, naleta kwenu malalamiko yangu labda wakiyaona kutokea hapa ni

Mimi ni mpiga picha, nimejiajiri kwenye kizi hii na ndio inayoniingizia kipato. Sasa nilikuwa nimeweka camera yangu sokoni ili niongezee na kiasi kingine ninunue kamera nyingine itakayonifaa zaidi kwenye kazi zangu, kamera yangu ilikuwa na thamani ya Tsh. Milioni 2 aina ya Nikon D610 pamoja na lenzi ya Nikkor 50mm f1.8.

Tar 10 June 2024 nilipigiwa simu na mteja aliyejitambulisha kwa jina moja la Chris, alinipigia simu asubuhi kwenye saa tano akaniambia anataka kununua Camera. Akasema nifanye delivery maeneo ya Tabata Segerea, karibu na sheli ya Oil Com. Nilipofika maeneo hayo ilibidi nichukue bodaboda mpaka mahali alipokuwa ananisubiri, akanipatia hela ya kumlipa boda (aliniambia nichukue boda atamlipa). Sikumuacha bodaboda aondoke nilitaka baada ya kumalizana na mteja niondoke naye.

Nikamuonyesha camera akaikagua, kulikuwa na kibanda cha Airtel Money karibu na hapo, akasema aliyekuwa hapo ni dada yake anataka amuoneshe kamera. Sikushtuka maana ilikuwa jirani, baada ya kumuonesha na kuongea maneno mawili matatu akasema kamera iko sawa na ameridhika nayo. Sasa ikabaki kufanya malipo, akaniambia pesa iko nyumbani kwake, ambako si mbali na hapo, hivyo twende akamalishe malipo.

Basi tukapanda wote ile boda boda tukaenda, tukafika kwenye nyumba ambayo si mbali na hapo akaingia ndani akisema anaenda kunifatia pesa. baada ya yeye kuingia ndani nikaanza kujisikia vibaya, kama vile naishiwa nguvu na kuwa kama naona mawingu (blur). Karibu yangu alikuepo bodaboda tuliyekuja naye pamoja na dada mwingine pembeni ambao baada ya kuniona katika hali hiyo walianza kunisaidia.

Baada ya muda nilikaa sawa, lakini muda wote huo yule kaka hakuwa ametoka nje, nikampigia simu hapatikani, kuulizia kwenye nyumba hiyo aliyoingia nako wakasema hawajamuona. Hapa ndio nikashtuka kuwa nimeibiwa. Kwa kufikiria haraka haraka nilihisi hela niliyopewa ilikuwa na aina ya madawa ya kulevya yaliyonifanya nipoteze fahamu. Kwakweli nilichanganyikiwa sana nikapanda gari na kurudi nyumbani mbweni, sikufikiria hata kwenda polisi.

Nilipofika nyumbani baada ya kupumzika na kuendelea kujisikia vizuri kiasi ndio akili ikarejea kuwa sikukwenda polisi, nikaenda kwenye kituo karibu na eneo ninaloishi wakaniambia nirudi kwenye kituo cha Tabata ambako niliibiwa. Muda ulikuwa umeshaenda, ikabidi niende kesho yake.

Kesho yake nikaenda toa taarifa polisi kituo cha Stakishali kipo Tabata Segerea. Nikapewa RB na namba ya mpelelezi lakini niliambiwa kuna machaguo mawili, la kwanza ni kuandika barua halafu unasubiri kupewa mpelelezi ambayo kwa maoni yao haifanyi inachukua muda mrefu na haifanyi kazi, na option ya pili ni kutoa elfu 60 kumpatia mpelelezi ambako hapa ndio mambo yataenda fasta fasta, yaani nitoe cha juu. Wkaniambia nikiwa tayari niende na elf 60 ndio kazi ianze. Kwakweli hiyo hela sikuwa nayo, ukizingatia nilikuwa nimeenda kuuza kamera Nikiwa teyari niwacheki

Nikauliza baadhi ya watu ninaowafahamu, imekuaje ninadaiwa pesa ya upelelezi wakati najua huduma hii ni bure, nikaambiwa ndivyo ilivyo tena mpaka nauli ya mpelelezi na pesa ya vocha unatakiwa umlipe ili afanyie kazi kesi yako. Basi wakati wanaendelea kutafakari cha kufanya nikaamua kurudi maeneo yale ambako niilibiwa, kufika pale nilikutana na yule dada aliyenisaidia jana yake nikamuuliza kuhusu yule kaka, kama ni mwenyeji maeneo yale na kumpa picha yake ambayo niliitoa kwenye page yake ya instagram, jina la instagram alikuwa anatumia Hamis_boy (sasa hivi amefuta account yake).

Yule dada aliniambia sura yake si ngeni, ila nimuachie namba yangu atatuma picha kwa rafiki zake anisaidie kuuliza, aliwatumia marafiki zake wakati niko njiani kurudi nyumbani akanipigia simu na kusema baadhi ya marafiki zake walimtambua na kusema anaishi Tabata Kinyerezi, ni mtu ambaye wamezoea kumuona hasa maeneo ya baa.

Sasa juzi nimepigia simu na yule dada nilimuachia namba, kuwa yule kaka kamtapeli mtu mwingine simu yenye thamani ya Tsh. laki 5 maeneo yale yale niliyoibiwa mimi. Inavyoonekana ndio michezo yake na itakuwa amaeshawatapeli wengi.

Sasa kama mimi ambaye sina utaalamu nimeweza kugundua hayo, naamini polisi wangeweza kumdaka ndani ya siku moja au mbili kuepusha watu wengine kufanyiwa utapeli na huenda ningepata kamera yangu, lakini mpaka utoe pesa ndio unapata huduma. Ina maana mtu usipokuwa na uwezo ndio hustahili kupata haki?

Mpaka kufikia hapa nimekata tamaa ya kuipata kamera yangu (ikipatikana nitashukuru Mungu) lakini naamini polisi wale wanaweza kuwajibishwa kwa tabia zao za kutengeza mazingira ya kuchua rushwa na kutia doa jeshi la polisi, na pia itasaidia mtu mwingine asije kuwa muhanga wa mwizi yule.

Kupitia nyie najua haitazidi siku moja yule mwizi atakuwa ametiwa nguvuni kama watakuwa hawajamchoma moto, maana yule dada alisema ikitokea amemuona tena anataka kumtapeli mtu mwingine atamuitia mwizi. Mnaona jinsi baadhi ya polisi wanasababisha wananchi wajichukulie sheria mkononi, maana tukienda polisi hali ndio kama hii.

Asanteni.

Naambatanisha picha ya jamaa aliyenitapeli ambayo niliipata kwenye page yake Instagram, screenshot inayoonesha namba yake, pamoja na RB niliyokata.

View attachment 3032820
Picha Chris, kijana aliyenitapeli

View attachment 3032821
RB niliyokata

View attachment 3032822
Mazungumzo mafupi tuliyofanya ikionesha na namba yake ya simu​
Ungewaambia tu Polisi kuna mtu wa CHADEMA anapanga maandamano, tayari angekuwa amekamatwa ndio baada ya hapo ueleze kesi yako ya msingi.
 
Polisi wa bongo wajinga sana.
Nilitapeliwa karibia 45m, niliuziwa kiwanja kisicho sahihi na diwani mmoja hivi. Diwani akakimbia baada ya kusikia namsaka, kwenda polisi na vile nilikuwa na kiwewe Cha kupoteza pesa ndefu. Wakanipanga niwape 4m ili wakimbizane kumtafuta na wakanihakikishia lazma watampata.

Kwa vile nilikuwa na wenge nikawapa, wale wajinga walichofanya nasikia walienda Kwa diwani wakampanga na yeye akawakatia mpunga hawakumkamata na wakawa wanampa Info namna ninavyomtafuta na jinsi gani ajifiche mini ikawa wananipanga kila siku. Kwa bahati mbaya yule diwani alikimbia mazima na uchaguzi wa 2020 hakuonekana

Polisi ni washenzi sana
Pole sana mimi 2017 walichukua 7m zangu walikua ni polisi ....nlienda kwa rco ambae sasa ni rpc manyara.walirudisha 8m kwa kuniomba sana ...tuliozaliwa mjini tunadeal na majizi kimenomeno tu
 
Habari JamiiForums, naleta kwenu malalamiko yangu labda wakiyaona kutokea hapa ni

Mimi ni mpiga picha, nimejiajiri kwenye kizi hii na ndio inayoniingizia kipato. Sasa nilikuwa nimeweka camera yangu sokoni ili niongezee na kiasi kingine ninunue kamera nyingine itakayonifaa zaidi kwenye kazi zangu, kamera yangu ilikuwa na thamani ya Tsh. Milioni 2 aina ya Nikon D610 pamoja na lenzi ya Nikkor 50mm f1.8.

Tar 10 June 2024 nilipigiwa simu na mteja aliyejitambulisha kwa jina moja la Chris, alinipigia simu asubuhi kwenye saa tano akaniambia anataka kununua Camera. Akasema nifanye delivery maeneo ya Tabata Segerea, karibu na sheli ya Oil Com. Nilipofika maeneo hayo ilibidi nichukue bodaboda mpaka mahali alipokuwa ananisubiri, akanipatia hela ya kumlipa boda (aliniambia nichukue boda atamlipa). Sikumuacha bodaboda aondoke nilitaka baada ya kumalizana na mteja niondoke naye.

Nikamuonyesha camera akaikagua, kulikuwa na kibanda cha Airtel Money karibu na hapo, akasema aliyekuwa hapo ni dada yake anataka amuoneshe kamera. Sikushtuka maana ilikuwa jirani, baada ya kumuonesha na kuongea maneno mawili matatu akasema kamera iko sawa na ameridhika nayo. Sasa ikabaki kufanya malipo, akaniambia pesa iko nyumbani kwake, ambako si mbali na hapo, hivyo twende akamalishe malipo.

Basi tukapanda wote ile boda boda tukaenda, tukafika kwenye nyumba ambayo si mbali na hapo akaingia ndani akisema anaenda kunifatia pesa. baada ya yeye kuingia ndani nikaanza kujisikia vibaya, kama vile naishiwa nguvu na kuwa kama naona mawingu (blur). Karibu yangu alikuepo bodaboda tuliyekuja naye pamoja na dada mwingine pembeni ambao baada ya kuniona katika hali hiyo walianza kunisaidia.

Baada ya muda nilikaa sawa, lakini muda wote huo yule kaka hakuwa ametoka nje, nikampigia simu hapatikani, kuulizia kwenye nyumba hiyo aliyoingia nako wakasema hawajamuona. Hapa ndio nikashtuka kuwa nimeibiwa. Kwa kufikiria haraka haraka nilihisi hela niliyopewa ilikuwa na aina ya madawa ya kulevya yaliyonifanya nipoteze fahamu. Kwakweli nilichanganyikiwa sana nikapanda gari na kurudi nyumbani mbweni, sikufikiria hata kwenda polisi.

Nilipofika nyumbani baada ya kupumzika na kuendelea kujisikia vizuri kiasi ndio akili ikarejea kuwa sikukwenda polisi, nikaenda kwenye kituo karibu na eneo ninaloishi wakaniambia nirudi kwenye kituo cha Tabata ambako niliibiwa. Muda ulikuwa umeshaenda, ikabidi niende kesho yake.

Kesho yake nikaenda toa taarifa polisi kituo cha Stakishali kipo Tabata Segerea. Nikapewa RB na namba ya mpelelezi lakini niliambiwa kuna machaguo mawili, la kwanza ni kuandika barua halafu unasubiri kupewa mpelelezi ambayo kwa maoni yao haifanyi inachukua muda mrefu na haifanyi kazi, na option ya pili ni kutoa elfu 60 kumpatia mpelelezi ambako hapa ndio mambo yataenda fasta fasta, yaani nitoe cha juu. Wkaniambia nikiwa tayari niende na elf 60 ndio kazi ianze. Kwakweli hiyo hela sikuwa nayo, ukizingatia nilikuwa nimeenda kuuza kamera Nikiwa teyari niwacheki

Nikauliza baadhi ya watu ninaowafahamu, imekuaje ninadaiwa pesa ya upelelezi wakati najua huduma hii ni bure, nikaambiwa ndivyo ilivyo tena mpaka nauli ya mpelelezi na pesa ya vocha unatakiwa umlipe ili afanyie kazi kesi yako. Basi wakati wanaendelea kutafakari cha kufanya nikaamua kurudi maeneo yale ambako niilibiwa, kufika pale nilikutana na yule dada aliyenisaidia jana yake nikamuuliza kuhusu yule kaka, kama ni mwenyeji maeneo yale na kumpa picha yake ambayo niliitoa kwenye page yake ya instagram, jina la instagram alikuwa anatumia Hamis_boy (sasa hivi amefuta account yake).

Yule dada aliniambia sura yake si ngeni, ila nimuachie namba yangu atatuma picha kwa rafiki zake anisaidie kuuliza, aliwatumia marafiki zake wakati niko njiani kurudi nyumbani akanipigia simu na kusema baadhi ya marafiki zake walimtambua na kusema anaishi Tabata Kinyerezi, ni mtu ambaye wamezoea kumuona hasa maeneo ya baa.

Sasa juzi nimepigia simu na yule dada nilimuachia namba, kuwa yule kaka kamtapeli mtu mwingine simu yenye thamani ya Tsh. laki 5 maeneo yale yale niliyoibiwa mimi. Inavyoonekana ndio michezo yake na itakuwa amaeshawatapeli wengi.

Sasa kama mimi ambaye sina utaalamu nimeweza kugundua hayo, naamini polisi wangeweza kumdaka ndani ya siku moja au mbili kuepusha watu wengine kufanyiwa utapeli na huenda ningepata kamera yangu, lakini mpaka utoe pesa ndio unapata huduma. Ina maana mtu usipokuwa na uwezo ndio hustahili kupata haki?

Mpaka kufikia hapa nimekata tamaa ya kuipata kamera yangu (ikipatikana nitashukuru Mungu) lakini naamini polisi wale wanaweza kuwajibishwa kwa tabia zao za kutengeza mazingira ya kuchua rushwa na kutia doa jeshi la polisi, na pia itasaidia mtu mwingine asije kuwa muhanga wa mwizi yule.

Kupitia nyie najua haitazidi siku moja yule mwizi atakuwa ametiwa nguvuni kama watakuwa hawajamchoma moto, maana yule dada alisema ikitokea amemuona tena anataka kumtapeli mtu mwingine atamuitia mwizi. Mnaona jinsi baadhi ya polisi wanasababisha wananchi wajichukulie sheria mkononi, maana tukienda polisi hali ndio kama hii.

Asanteni.

Naambatanisha picha ya jamaa aliyenitapeli ambayo niliipata kwenye page yake Instagram, screenshot inayoonesha namba yake, pamoja na RB niliyokata.

View attachment 3032820
Picha Chris, kijana aliyenitapeli

View attachment 3032821
RB niliyokata

View attachment 3032822
Mazungumzo mafupi tuliyofanya ikionesha na namba yake ya simu​
Hawa wapuuzi wanakera...Kama una uwezo mloge awe mwehu tu
 
Back
Top Bottom