Nimeibiwa, nitamkamataje huyu mtu!?

Tena watakuwa jipu kama agent wanatakiwa kubaini nani mwenye bidhaa na ni nani ni tapeli ili kuongeza imani kwa wateja wao. Mbona ebay watu wanafanya biashara vizuri tena kutoka mbali na unapata bidhaa yako kamili
Yeah... Mnunuzi hapati hela mpk bidhaa imfikie mnunuaji ndio maana watu wanatumia paypal... Hawa kupatana mtu anaweza bidhaa za uongo anaibia watu wao wamekaa tu, ilitakiwa kuwe na utaratibu maalum wa muuzaji kujiunga na mtandao wao ili iwe rahisi kumpata akitapeli
 
Hivi jamani ni kwa nini mitapeli a.k.a mipenda kitonga inatangulizaga ooh mi ni askari Mara usalama wa taifa? Ili iweje....sijawahi pata jibu ila nahisi hili, MOSI upate amani ya moyo ( yaani usishtukie kuwa utatapeliwa)) pili ili likishakupiga uogope kulifatilia. To hell with yo all (Mitapeli/ mijizi)
 
usisahau kutuletea mrejesho
 
Mimi huyo jamaa nimemtafuta Jana na Leo nikaongea nae sana kuwa nahitaji hyo macbook akanitumia macbook pro ya 2015 mpya tena ndani ya box nikamuuliza bei gani? Akajibu 250,000.
Hivi hapa ukitapeliwa si utakuwa umejitakia mwenyewe? Macbook pro 2015 bei yake ni $1800-2500 approximately 4,000,000 alaf mtu anakwambia bei 250,000 yaan bei ya shipping of macbook pro from USA to TZ ndio anakwambia anaiuza. Mtu unatakiw ujipime mwenyewe!
 
Siku zote... kama kitu ni toooo good to be true.. alarm zako za kichwani zinatakiwa zipige na uwe makini kufanya hicho kitu. Matapeli wanatumia udhaifu wa binadamu wa kupenda mteremko/Gullible.
 
Ni kwel smetme tunawaonea tu hawa matapeli tatizo ni sisi wenyewe. Hatutak kufikiri.then tukitapeliwa tunalalamika wakat sisi wenyewe ndo chanzo. Tumeacha akili zetu zimedumaa hatuzitumii.

 
Hao kupatana nao watakuwa hovyo kama watu wanatumia mtandao wao kwa utapeli
Kupatana walisha sema never pay in advance mbona..ukiingia tu unakutana na huo ujumbe

Alaf pia wewe kitu cha million huko uuziwe kwa laki 2? Hivi inakuja?
Kupatana hawana makosa


Sasa kama hiyo pavilion kwa hizo specs na bei ni sawa?
 
Wapigaji kila kona...mitapeli/ mijizi mingine imejazana humu humu JF..

Hmm humu JF sifikiri kama kuna hao majizi na matapeli kama wapo itakuwa utapeli wao wanafanya kwenye mitandao mingine sio humu kwa uongozi wa JF upo makini hauwezi kuruhusu vitendo vya uhalifu vifanyike humu. Kama umetapeliwa na wanachama wa humu na unawafahamu kwa majina ni busara ukatoa taarifa kwa uongozi ukawachulia hatua mapema wasiharibu sifa ya mtandao wetu pendwa.
 
Amekukosa kosa
 
Mkuu samahani kwa kuchanganya maelezo.
Kumbe muhusika hajasema ni wa jeshi gan mkuu.
Ila nilichong'amua kwa haraka ni kua huyo jamaa ana asili ya Uzanzibari kdg kwny matamshi yake,"shemeg" haitumikagi bara mkuu.
Kweli pia kuna sehemu kasema "M/mungu afanye wepesi" kweli inaonesha likely wa uko
 
mkuu m nmepigwa humhum jf, na nikatoa taarifa ila sikusaidiwa, jamaa alisema anaweza kuunganisha dish za kawaida nikapata za mpira, mwanaume nikamlipa asee kanipiga mpaka leo biashara ya mtandao sifanyi, hum jf wapo wengi,
 
mkuu m nmepigwa humhum jf, na nikatoa taarifa ila sikusaidiwa, jamaa alisema anaweza kuunganisha dish za kawaida nikapata za mpira, mwanaume nikamlipa asee kanipiga mpaka leo biashara ya mtandao sifanyi, hum jf wapo wengi,

Pole mkuu, hiyo ilikuwa mwaka gani? Kuna taratibu za kufata unapofanya biashara na mtu humu JF. Uongozi wa JF umetutahadharisha hili mapema.
 
Screen peke yake ya iphone 6 ni zaidi ya 300K
 
Pole mkuu, hiyo ilikuwa mwaka gani? Kuna taratibu za kufata unapofanya biashara na mtu humu JF. Uongozi wa JF umetutahadharisha hili mapema.

mwaka jana mkuu, jamaa aliweka detailz zake, nlipompigia akanipa maelekezo mazr kisha akaniambia nitume adv, i think 70000, baada ya hapo sijampata tena, nikawasilisha malalamiko ila ckupata msaada.

pengine mkuu npe utaratibu wa namna ya kuwasilisha malalamiko yangu..
 

Mkuu, kabla hujafanya biashara yoyote humu ni vema ukaushirikina uongozi wa JF. Ikiwa utafanyika utapeli uongozi wa JF unajua utakusaidia kwa njia ipi. Huo ndio utaratibu wa kufuata...
 
Narudia kusema humu JF kuna mitapeli na mijizi...trust me! Ngoja nipunguze ubusy kidogo nije kutoa ushuhuda na evidence

Over!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…