Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yeah... Mnunuzi hapati hela mpk bidhaa imfikie mnunuaji ndio maana watu wanatumia paypal... Hawa kupatana mtu anaweza bidhaa za uongo anaibia watu wao wamekaa tu, ilitakiwa kuwe na utaratibu maalum wa muuzaji kujiunga na mtandao wao ili iwe rahisi kumpata akitapeliTena watakuwa jipu kama agent wanatakiwa kubaini nani mwenye bidhaa na ni nani ni tapeli ili kuongeza imani kwa wateja wao. Mbona ebay watu wanafanya biashara vizuri tena kutoka mbali na unapata bidhaa yako kamili
usisahau kutuletea mrejeshonasisitiza tuanze kuwa tunatumia akili zetu zifanye kazi . kuna utapeli mwingine wa kizembe sana tena sana. unapoambiwa biashara nawe ni msomi au mtoto wa mjini hebu tikisa kichwa kidogo ubongo ushtuke ikiwa ulikuwa umelala kwa muda mrefu. linganisha bei ya hicho kitu na anayokuuzia muuzaji tena ameweka kwenye mtandao hujiulizi huyu mtu kwa bei hii alikuwa na bidhaa ngapi? na tangazo smetme limekaa siku 2 hujiulizi kuwa ina maana wenzio hawalioni? but pia bei halisi na ya kuuzia ziwe na uhusiano kiasi flan hata kama ni za deal kuna kiwango unless otherwise uwe hujui kabisa bei ya hicho kitu. ni sawa na leo mtu anakuja kukwambia anauza gari yake toyota rav namba c model letsa say ya 2010 kwa tsh mil Moja. ukimuuliza anakwambia anashida sana na pesa. picha anakutumia gari bado ipo safi kabisa. then anakwambia mtumie advance ili mtu mwingine asije akaichukua nawe unamtumia pesa una akili wewe?
halafu unakuja hapa utuambie tukutafutie huyo mtu? anyway nimependa kuwa mhusika umekuwa jasiri na kuweka suala hili wazi wengine wametapeliwa wameshindwa hata kuwaelimisha wenzao. wewe Ubarikiwe kwa kuwa umeamua kuielimisha jamii hii inayopenda vitu vya utelezi,vitu vya deal n.k
huyo tapeli namtaka nimwoneshe sisi wengine tulianza utapel toka siku ya kuzaliwa. yeye utapeli wake kajifunzia tu ukubwani.
Mimi huyo jamaa nimemtafuta Jana na Leo nikaongea nae sana kuwa nahitaji hyo macbook akanitumia macbook pro ya 2015 mpya tena ndani ya box nikamuuliza bei gani? Akajibu 250,000.
Hivi hapa ukitapeliwa si utakuwa umejitakia mwenyewe? Macbook pro 2015 bei yake ni $1800-2500 approximately 4,000,000 alaf mtu anakwambia bei 250,000 yaan bei ya shipping of macbook pro from USA to TZ ndio anakwambia anaiuza. Mtu unatakiw ujipime mwenyewe!
Kupatana walisha sema never pay in advance mbona..ukiingia tu unakutana na huo ujumbeHao kupatana nao watakuwa hovyo kama watu wanatumia mtandao wao kwa utapeli
Aiseeeeeeeh!Tehe tehe tehe nimecheka sana, msg moja huyo jamaa anajibu M/Mungu afanye wepesi...
Wapigaji kila kona...mitapeli/ mijizi mingine imejazana humu humu JF..
Amekukosa kosaMkuu nimeiona number aliyo tumia kwangu nii hii hapa... +255 788 570 586..
Alipost simu akiwa anauza.. Nikamcheck.. Na hiyo Number ndo ali ipost pale... Nakumbuka alikuwa anauza samsung A5.. Akidai anauza 250.. Nikamwambia upo wapi,, akasema yeye yupo Iringa bt mm nimtumie hela nusu then akanitumia mzigo ndani ya masaa saba Nishapata mzigo wangu.. Nikamwambia naomba ntumie picha ya hiyoo simu whatsapp .. Akanitumia..
Hapo ndo nikashtuka, kwa sababu ni zile picha za gugo then kama ame crop.. Nikawa na mashaka na biashara yake.. Hapo ndo akaanza kunivuta na kuniambia yeye askari si niwe na amani kwa usalama wa pesa yangu akanitumia na vitambulisho hivo...
Lakini roho yangu ilisha ingia mashaka....
Nikamwambia Asante mkuu.. Next time.. Tunafanya biashara...
Nikawa nimepona kuingia kwenye mikono ya huyo ngiri...
Kweli pia kuna sehemu kasema "M/mungu afanye wepesi" kweli inaonesha likely wa ukoMkuu samahani kwa kuchanganya maelezo.
Kumbe muhusika hajasema ni wa jeshi gan mkuu.
Ila nilichong'amua kwa haraka ni kua huyo jamaa ana asili ya Uzanzibari kdg kwny matamshi yake,"shemeg" haitumikagi bara mkuu.
mkuu m nmepigwa humhum jf, na nikatoa taarifa ila sikusaidiwa, jamaa alisema anaweza kuunganisha dish za kawaida nikapata za mpira, mwanaume nikamlipa asee kanipiga mpaka leo biashara ya mtandao sifanyi, hum jf wapo wengi,Hmm humu JF sifikiri kama kuna hao majizi na matapeli kama wapo itakuwa utapeli wao wanafanya kwenye mitandao mingine sio humu kwa uongozi wa JF upo makini hauwezi kuruhusu vitendo vya uhalifu vifanyike humu. Kama umetapeliwa na wanachama wa humu na unawafahamu kwa majina ni busara ukatoa taarifa kwa uongozi ukawachulia hatua mapema wasiharibu sifa ya mtandao wetu pendwa.
mkuu m nmepigwa humhum jf, na nikatoa taarifa ila sikusaidiwa, jamaa alisema anaweza kuunganisha dish za kawaida nikapata za mpira, mwanaume nikamlipa asee kanipiga mpaka leo biashara ya mtandao sifanyi, hum jf wapo wengi,
Screen peke yake ya iphone 6 ni zaidi ya 300KMimi nashauri Watanzania tusipende vya Bure Computer ambazo mtuhumiwa kazitaja hata iwe used vipi haziuzwi hiyo bei Computer za Apple ni expensive huwa zinafika hadi 4Million na zilizonyingi Laptop za chini kabisa ni 1.5million halafu mtu anakwambia 250K unakubali Kadhalika iPhone 6 Plus haiwezi kuuzwa 250 kwa sababu bei ya hizo simu nia kuanzia 1.6Million tutumie akili za kuzaliwa S6 haiwezi kuuzwa hiyo bei pia tuache Ujinga na kuibiwa kwako ni Sahihi kabisa Hizo bei Hata Screen ya iPhone haizwi kwa bei hiyo tusipende vya Bure!
Pole mkuu, hiyo ilikuwa mwaka gani? Kuna taratibu za kufata unapofanya biashara na mtu humu JF. Uongozi wa JF umetutahadharisha hili mapema.
mwaka jana mkuu, jamaa aliweka detailz zake, nlipompigia akanipa maelekezo mazr kisha akaniambia nitume adv, i think 70000, baada ya hapo sijampata tena, nikawasilisha malalamiko ila ckupata msaada.
pengine mkuu npe utaratibu wa namna ya kuwasilisha malalamiko yangu..
Narudia kusema humu JF kuna mitapeli na mijizi...trust me! Ngoja nipunguze ubusy kidogo nije kutoa ushuhuda na evidenceHmm humu JF sifikiri kama kuna hao majizi na matapeli kama wapo itakuwa utapeli wao wanafanya kwenye mitandao mingine sio humu kwa uongozi wa JF upo makini hauwezi kuruhusu vitendo vya uhalifu vifanyike humu. Kama umetapeliwa na wanachama wa humu na unawafahamu kwa majina ni busara ukatoa taarifa kwa uongozi ukawachulia hatua mapema wasiharibu sifa ya mtandao wetu pendwa.