Waliokuibia ni hao hao waliokufanyia wiring. Watafute uwabinye kende watarudisha
Hii kauli sometimes..
Nakumbuka kipindi hicho kufunga madishi makubwa ndo habari ya mjini..
Kuna mtaa wa kishua ndo nimeamia na ndo nilikuwa naanza kujitegemea jeshi la mtu m1..
Kuna nyumba kama mitaa miwili toka hapo ninapoishi kuna mzee jirani na mama yangu wa hiari nilimfungia dish la ft 6,jipya nimelifungua mwenyewe kwenye box,kipindi hiko tunafunga mpaka LNB 4 michanel mpaka 200 zote za bure,hyo kazi huyo bi mkubwa ndo aliniunganisha istoshe mi ni fundi wake miaka mingi hata kabla sijahamia huo mtaa..
Ikapita kama miezi miwili..
Siku moja nikiwa kwenye misele yangu,maana nilikuwa nazunguka mitaa balaa kwa kazi hiyo,yule mzee akanipigia simu kwamba channel zimekata kutwa nzima hawakuangalia TV, nikampanga nikiwahi kurudi nitamcheki maana tunaishi almost ni kama mtaa mmoja...
Saa mbili ndo nikarudi ikabidi ninyooshe moja kwa moja mpaka kwa yule mzee.
Nikawashiwa TV nikachukua remote ya receiver kipindi hicho MediaCom 930Mft+ ndo ipo juu..
Uzuri wa hii recever kuna button ya kijani ukibonyenza inakuletea status za Satelite dish..
Inatokea mistari miwili yenye asilimia
1.Wa Orange...huu umeandikwa Quality,huwa unaonyesha connection kati ya dish na reciver,na inabidi isome kuanzia 68% so kama connection mbovu au waya umekatika mahali unasoma 0%...
2.Green...huu ni wa Strengh, kwamba dishi limeshasetiwa na picha zipo na asilimia zake..
Sasa
Kuclick buton ya green Quality ikasoma 0%...uzuri mwenyewe akiwepo.
Ikabidi kitaalam niwaelezee kwamba ukiona hivyo either waya umekatika mahali au ni kama dish halipo kabisa So nikaomba ngazi usiku uleule maana dish lilifungwa kwenye Kenop..
Lahaula nafika juu dish halipo,frem zimebaki kama zilivogongelewa manake liliibwa usiku wa kuamkia hyo siku..
Nikawa nawaza nitamwambia nini huyu mzee na ile kauli yangu tukiwa ndani nafanya diagnostic kwamba "ni kama vile dish halipo"..
Dah kutype kazi asee mi naishia hapa....
Licha ya kuwa baadae sana aliponunua dish lingine jipya hakuniita