Nimeibiwa pesa zangu kwenye Kibubu na 'Chuma Ulete'

Nimeibiwa pesa zangu kwenye Kibubu na 'Chuma Ulete'

chimamii

Member
Joined
May 24, 2022
Posts
5
Reaction score
14
Wakuu nina swali,

Kuna jamaa yangu amenihadithia kuwa alikuwa anatunza pesa kwenye Kibubu kwa muda wa miezi kadhaa na kwa kipindi hicho alikuwa anatumbukiza noti za pesa na coins pia. Lakini cha ajabu alivyokuja kuvunja alikuta coins mbili tu na moja ya Tshs. 200 ina tobo katikati.

Hivyo swali langu ni: Hili suala la chuma ulete ni kweli lipo? Story ni nyingi mtaani kuhusu kuibiwa na chuma ulete, ni kwamba uchawi upo ama ni mtu wa karibu anaiba? ama kuna janjajanja inayofanyika hatuijui?

Ahsante.
 
Chuma ulete ipo,kama watu wanaweza kukuhamishia mazao kimazingara wanashindwaje kuhamisha pesa?
Kuna wadada naishi nao hapa jirani wanalalamika kila wakitoka kwenye biashara zao buku au jero halipo na hawakumbuki hizo hela zinapotea vipi ..
 
Kuna mlinzi mmoja waliiba usiku eti akasema itakuwa ni majini sababu hakuwasikia..., waajiri wake walimwambia aache upuuzi sababu wakikubaliana na hio Hoja hao majini watarudi kila siku na waajiri watajikuta wanajiunga na mlinzi kutafuta kibarua baada ya kufilisika....
 
Back
Top Bottom