Nimeikumbuka JamiiForums ya zamani

Wahenga wa JF wakuu Mentor na Watu8 wamepoa sana siku hizi.
 
Huyo namba 7 sijui siku hizi amekuwa je?
 
Supu ya mawe..kongosho..fagio la chuma...tunakodisha bunduki ..zamani ulikua ukiingia jf majukwaa yote unakutana na madini ya kufa mtu..siku hizi mara sijui tigo kufanyaje
 
  • Elimu ilikuwa zamani
  • Tabia nzuri zamani
  • Muziki mzuri zamani
  • Mpira na timu bora zilikuwa zamani
  • Wanawake natural ilikuwa zamani
  • CCM bora ilikuwa zamani
  • Upinzani bora ilikuwa zamani
  • Kutongoza ilikuwa zamani, siku hizi ni kama kusukuma mlevi
  • Uaminifu ilikuwa zamani
  • JF bora ilikuwa zamani
Wahenga hawataki kabisa kukubali kushindwa, anyway kila kitabu na zama zake
 
waliokua zamani ndio nyie nyie mliokuwepo sasa hivi, mnakimbiza vivuli vyenu….kama hukuwepo umeajuaje majina ya wahenga kama na wewe sio mhenga kwa ID mpya...😁
 
waliokua zamani ndio nyie nyie mliokuwepo sasa hivi, mnakimbiza vivuli vyenu….kama hukuwepo umeajuaje majina ya wahenga kama na wewe sio mhenga kwa ID mpya...[emoji16]
Rebecca tuambie ID yako ya zamani, huenda nilikutongoza kabisa. Miaka hiyo nilikuwa nazama pm kama sebuleni tu[emoji39]
 
Well
katika kumbukumbu zangu nakumbuka kuna watu walikuja shuleni kwetu wakijitambulisha kua wame toka Jambo forums nazani mi miaka ya 2006/07 kipindi iko nilkua nakaribia kumaliza elim yang ya msingi jina lilinikaa kichwan lakini sikua na idea yoyte kuhusu hawa jamaa (jamboForums)

kipindi nipo Olevel nili bahatika kupata simu yenye access ya internet zilikua ni Nokia kati ya Eseries iv katka ku google mambo yangu nika kutana na matokeo mengi kutokea JF hii ilikua miaka ya 2009/10 kuanzia 2010 nikawa sasa mtumiaji wa JF lakini sikua member

2013 kipindi nimetoka kumaliza kidato cha 6 apa ndo rasmi nika ingia JF baada ya kua guest kwa zaid ya miaka3 zaidi nili vutiwa na nyuzi/mijadala inayo wekwa humu members hawa wali nivutia sana kipindi iko

Mentor Buddy Heaven Sent Heaven on Earth @lara1 Elungata pasco @Raskim Kingz Mshana Jr et al
 
Ahsante sana mpendwa. Naamini bado unavutiwa na kuenjoy JF
 
Badiebey na money stuna nafikiri
 
Watu wa facebook wameivamia Jamiiforums kwa kasi! Kila uki-scroll ni hadithi za uzinzi tu! Wengine hawajui hata Kiswahili nao wamo tu wanang'ang'ana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…