Nimeikumbuka JamiiForums ya zamani

Nimeikumbuka JamiiForums ya zamani

1- lara1, huyu was one of a kind... Alikuwa ni mtunzi mzuri sana wa hadithi tamu ambazo watu walikuwa wanasubiri muendelezo wa hadithi zake kwa shauku saaana. Alikuwa na mashauzi flani hivi with an amaizing english. lara 1 alikuwa pia famous apa ndani enzi hizo kwa sababu nilikutaga kamjadala ka jamiiforum party iliofanyika na members mbalimbali walikutana akiwemo lara.


I miss Lara kwa kweli, Sijui yupo wapi?
 
Kila zama na zama zake well hata mie walonivutia kujiunga na jf walikuwa lara 1 , DEMBA heven on earth Kaizer Dark City Mentor
Nilikuwa nafurahia namna tu wanavyojamiiana humu ndani, sijawahi kujutia kujiunga.

Well naipenda jf the way ilivyo hata sasa na navutiwa na watu wengi tu kwa michango yao na namna tunavyojamiiana. Jf huifanya siku yangu kuwa murua kabisa

cute b Mentor Heaven Sent manengelo Extrovert Khantwe Evelyn Salt Mother Confessor Madame B MO11 Kaboom Eli79 Hawachi Shadeeya Ulweso Edelyn manengelo @meeya RRONDO Shunie Sakayo Thad The Monk
na wengine weeeeeengi ambao sijawataja.
Malcolm Lumumba na Fisadi kuu umewasahau..
 
Okay,
Siku nyingi sana nilikuwa natamani nianzishe thread na mada nilikuwa nayo lakini sikufanya hivyo hadi leo hii.
Nakumbuka back then nilikuwa advance nafkiri ndipo nilipo kutana na jamiiforumz mtandaoni tu kama bahati. Nikazama ndani and what i saw kilifurahisha macho yangu sana na ikawa ndo tabia yangu kila siku japo sikuwa na uwezo wa kucomment wala kuanzisha thread sababu sikuwa na account.
Kilichonifanya nianzishe hii thread ni members waliokuwa wananipendeza sana nikiona thread au comment zao.
Nitawataja lakini ukikosekana humu na wewe ni mhenga usijisikie vibaya bali comment na mimi nitakuacknowledge.
1- lara1, huyu was one of a kind... Alikuwa ni mtunzi mzuri sana wa hadithi tamu ambazo watu walikuwa wanasubiri muendelezo wa hadithi zake kwa shauku saaana. Alikuwa na mashauzi flani hivi with an amaizing english. lara 1 alikuwa pia famous apa ndani enzi hizo kwa sababu nilikutaga kamjadala ka jamiiforum party iliofanyika na members mbalimbali walikutana akiwemo lara.
2- watu 8,
i dont remember so much about him ila ni kama huwa namuona ona bado humu ndani sio kama lara 1. watu 8 yeye alipenda kujiclassify kama mhenga. Huwa ana majibu yake flani flani yanayojitofautisha na watu wengine. Back then usingeweza kukosa jibu kama vile 'jamani shule zinafunguliwa lini?' maswali kama haya ni kwa sababu ya kukerwa na mada za uongo na za kitoto. Wenyewe waliziita chai.
3- kasie,
bidada huyu ana majibu kuntu. Unaweza kupata shushu ukaenda kulala. Avatar yake ni ya mama mtu mzima sana lakini vitu anavyopost huwa vinawafanya watu kujiuliza maswali. Thread zake nyingi nilizoziona ni kuhusu baecation zake anazoendaga na how they did it like siku moja alipost how nice it was having sex kuendana na beat ya muziki na mpenzi wake ilivyokuwa.
4- heavensent, not much about her lakini nakumbuka alikuwa admired sana na wanaume waliokuwapo japo unaweza kusema ilikuwa ni utani tu.
5- Mentor, huyu bwana nilikuwa natamanigi sana nimuone tu hata yeye mwenyewe alivyo japo sijawahi kufanikiwa. Sikumoja alipost story ya maisha yake and how aliendup kuambukizwa ukimwi. Story zake chini kabisa huwa anamalizia na 'wassalam, Mentor'. Nae ni mhenga.
6- Mshana jr, huyu avatar yake kulikuwa na mbaba hivi kibonge. Kati ya watu wote jamiiforumz, avatar yake ni kati ya chache nilizowahi kuhisi ni avatar za kweli. Kama sijamchanganya na mtu mwingine basi yeye alipenda mambo ya uganga uganga sana.
7-Bujibuji, nimemkumbuka tu kwa sababu ya comments zake. Nae ni mhenga.
8- Mzizimkavu, huyu ni daktari wetu. Hakuna anaebisha nadhani. Kukiwa na kapost ya kaugonjwa lazima awe tagged. Nae pia kama sijamchanganya nafkiri ni yeye aliemjibu Mentor kwenye thread yake ya sitaki dawa jinsi ukimwi ulivyo kisaikolojia zaidi and was ready to help.
Nimeikumbuka sana jamiiforums ya zamani. Jamiiforums ambayo ulikuwa ukitaka kuanzisha thread kwanza unajipima wewe na hiko unachotaka kukiwasilisha sio unajikurupukia tu unaandika andika. Back then mada zilikuwa kuntu. Ukikuta mtu anaomba ushauri basi ujue kweli yamemfika. Na kama ni uongo (chai) utawaskia tu members majibu yao jinsi ambavyo hayako serious. Zamani mada za ooh jinsi kumla housegirl oooh, oooh jinsi ya kuchepuka usikamatwe, mara mwingine kaja na thread kichwa cha habari na habari yenyewe haviendani kulikuwa hakuna.
Tatizo sijajua ni nini ila ninachoweza kuanalyse ni kwamba zamani MMU ilikuwa ina nidhamu utafkiri umeingia jukwaa la great thinkers sio siku hizi ushudu ni mwingi mnooo hadi wahenga wanatukimbia. Unaingia MMU utafkiri umeingia jukwaa la jokes.

Kama na wewe umeimiss jamiiforums ya zamani kama mimi watag wahenga wako na tuelezee what inspired you kuingia jamiiforums.

NB: Naomba thread yangu isitolewe humu ndani. Mods please nimeileta humu kwa sababu ni huku ndipo nilipowajulia hawa watu.
Asante sana mkuu
Vip kuhusu WARUMI na habari za ndani kabisa za watu tofauti?
 
Kulikuwa na jamaa anaitwa Moneystuna, siku hiz nikionaga Money penn ndo najua mwenyewe, Kipindi fulani aliekuwa mpiga picha wa Diamond bwana Kifesi alikuwa na accoun yake ya Heaven on Desert, alikuwa anakabiliwa na hali ngumu sana humu jukwaani

Ila JF inabadilika kila mwaka.
 
Sitaki kujua kwamba imetokea tuu nikawa wakwanza kwenye hiyo list.

Lakini napenda kusema nimefurahi sana jina langu kuwa la kwanza kukujia kwenye akili yaani na ninajidaijee[emoji23][emoji23][emoji23]. Kwangu ina maana kubwa kwamba miaka 5 yote tuliyojuana , haujawahi kujuta kunijua.

Kama vile nakuona unavyokuja kunikatisha tamaa[emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huo mkwara hapo mwisho umesababisha nisahau kabisa nilivyotaka kukushushua.
 
Aisee mbona watu wengi wanasema jamii forums ya zamani ndo ilinoga au kwani kuna jamii forums ngapi? Anyway mimi jamii forums kama jamii forums nimeanza kuitumia vizuri mwaka huu

Natumia app mimi browser huwa inanitia uvivu na nikiingia kwa browser ni dakika mbili nimetoka ila kwenye app huwa nakesha zamani nilikuwa nasoma nyuzi za jf kupitia opera mini na opera news nakumbuka nilivyokuwa nasubiria hadithi za Mzizi Mkavu zile za majini nilikuwa nazifuatilia mwanzo hadi mwisho kupitia opera mini

Ila kuna hawa watu Zero IQ Money Penny aggyjay hawa nilianza kusoma nyuzi zao kupitia opera news mwaka huu na kwa kiasi fulani kupitia zile nyuzi ndipo niliposhawishika rasmi kuwa mwanachana wa freemason sorry jamiiforums

Ila kiukweli sijawahi jutia kuwa member yaani humu ndimo ninamomalizia stress zangu maana kuna watu nawakubali sana na michango yao humu jf

Jassue Khantwe cute b Saint anne Atoto Sakayo Sky Eclat Evelyn Salt Cookie Smokey Rebeca 83 Ulweso joanah kapeace manengelo Extrovert Relief Mirzska rikiboy troublemaker Mshana Jr Equation x

Wapo wengine wengi ambao sijawataja hapa na ninatambua michango yao ila hawa niliowataja aisee huwa wananifurahisha mno humu

Japo kati ya wote hao niliowataja ninafayehamiana naye nje ya jf ni mmoja tu Jassue ambaye ni rafiki yangu sana sema humu hayupo active kivile ila hao wengine wote hatufahamiani nje ya jf huwa ninawakubali tu humu ndani na mimi ndugu na marafiki zangu karibu wote siyo watumiaji wa jf kabisa

NB: Kwa wale wanaopenda kujifunza nasikitika kusema kwamba hii hadithi yangu haifundishi chochote (natania) ila mtoa mada samahani kwa kuweka comment ndefu inayokaribia kufikia thread yako[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji2210][emoji2210][emoji2210][emoji2210]
Hata ya sasa inanoga inategemea ni siku ipi na jukwaa lipi msomaji anapendelea,

Kila mtu yuko na interest zake hatufanani, na vile vile kuna ID zinatema mapumba tu hivyo kuepuka msongamano sichangiagi mada akikera zaidi unaclick kablock makini maisha yanaenda

Weekend kunanoga sana humu mmu,

Mimi nashukuru kukufanya nikuvutie Edelyn vile vile mi napenda tu ulivyo na moyo wa kushushia watu wabishi magazeti ni moyo wa kipekee sana yaani hongera maana mi mtu akibisha huwa nampa ushindi tu sijihangaishi na kushushia mbishi gazeti lakini kwako ni tofauti na nikiyakutaga nakupaga like km kifuta jasho loh

Nawapenda wote tu mimi kutaja humu hata siwamalizi wengine nawasahau majina
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hapana mimi ni mgeni sema tu nimekuja kwa kasi ya 5G zamani nilikuwaga mpenzi mtazamaji ila mwaka huu na mimi nikaanza kuwa mpenzi mtangazaji[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Basi ni vyema mama.
 
Back
Top Bottom