Nimeingia choo cha kike .... part 8 (Mwishooo, nipeni pole!)

Nimeingia choo cha kike .... part 8 (Mwishooo, nipeni pole!)

HP,brilliant if it is fiction but if it is based on true story of yours,am sorry for what happened to you.Leaving you citing that that you were not strong enough as one of the reasons was a mistake.Hakuna mtu perfect bana,udhaifu wako ulikuwa mdogo sana kulinganisha na majority ya mtu anemtaka yeye.

Kama nihivyo hujaingia choo cha kike kwani huna sababu ya kuwachukia wanawake unless labda kwa yule wa kwanza ambae hatujui alikutenda nini.

Kama nilivyosema kama ni fiction,ni story nzuri sana kuandika na kuisoma lakini kama yalikukuta kweli nakupa pole sana.Lakini tusichukiane,wanaume kwa wanawake kwayale mabaya tunayotendeana,inauma kweli kutendwa,ila tusamehe baada ya makovu ya kutendwa kupona.

Umetufundisha mambo fulani katika story yako,lakini mawili makuu ni kuwa na upendo wa kweli na pili tunachaguaje watu wa kuwa nao katika maisha yetu(kuoa/kuolewa) ili kupunguza yale ambayo yanatukuta kila siku ndoa kuvujika nyingine kabla ya hata kufungwa.
Niliweka thread moja hapa ya kipande cha maisha yangu kabla ya kuoa na regrets nilizokuwa nazo na ilikuwa na maswali kadha yanayoshabiana na hii story yako lakini haikupata michango ya maoni ya watu wengi.Ulichangia kitu fulani katika hiyo thread nakumbuka,inaitwa .....she wasn't a girl........she was not yet a woman.Inahusika sana katika hii story .

Asante sana tena HP,mungu akubariki.

Ntatafuta huo uzi it seems ulikuwa mzuri!
 
Nimejifunza kitu mkuu, nikimpata wa type yako ntakuwa wakwanza kumwambia tukapime hata kama keshanambia ana HIV +Ve...
 
Mkuu pole sana asee (As umesema ni true story) Lakin kama sio ya ukweli then Hongera kwa talent yako mkuu.
Ngoja niongee na jeiefu admins wakupe tenda ya kupublish Chombeza la JeiEfu kila wiki...:thinking:
 
Pole kama ni kweli.Achana naye huyo,LOVE sio kibarua hicho ufanyiwe interviews za hatari hivyo.Je kama ungekuwa na presha si ungekufa!!Huyo Angel ni selfish sana + a manipulative beutiful lier(texted u hakuachi ng'oo hata ufanye nini).Binadamu sio perfect sisi ajue,if she couldn't trust you without all that HIV +ve drama,SHE DOESN'T DESERVE YOU!

P.S Remember love is a choice!
 
Pole sana kaka kwa hayo yaliyokukuta, mwanzoni nilifikiri utani ila kwenye hii part ya mwisho nimeelewa kwanini unasema umeingia choo cha kike.
Kwa maoni yangu tu ni kuwa wasichana wengi huwa wanapenda kutupima akili sisi wanaume lakini pamoja na hayo bado mimi nina wasiwasi kuwa inawezekana huyo dada hakukupenda kwa dhati coz kama angekupenda kwa dhati baada ya kugundua udhaifu wako angetafuta njia ya kukusaidia ili muwe pamoja maishani... haya ya kusema huna msimamo ni visingizio tu brother..... ebu check majibu haya hapa “Majibu yako, yalinifanya nikose tumaini la kuishi duniani” “Kimbilio langu na tegemeo langu lilikuwa ni kwako” sitegemei mtu huyo aliyesema hivo (kwa dhati) akaona tatizo kwako halafu akajibu vitu kama hivi Kwanza HorsePower una upendo wa dhati, lakini hujiamini, Pili una moyo wa huruma lakini ni mtu unayeyumbishwa na marafiki. Kwa hivyo nimeshindwa mimi.
Napata wasawasi kuwa alikuwa ana mambo yake mengine, labda alitaka awe record ya kutongozwa na wewe kwa ajili ya umaarufu wako ofisini au kuna jambo lingine lakini kama angekuwa anakupenda basi angekuvumilia na kukuambia ubadilishe mtazamo wako ili uwe na msimamo na ujiamini.
Kwa hiyo nakushauri jitahidi kumsahau coz kwangu mimi nahisi alikuwa anachezea akili yako and she was not there for love.

Nakutakia mafanikio ila nakushauri usikate tamaa naamini utampata wako kwani naamini si wanawake wote watakuchukia huyo achanan nae brother.

Thanks
 
halafu umenikumbusha na mie niliwahi kutegwa na ex bf wangu. siku moja alinipigia cmu kwa sauti ya unyonge akaniambia ana mimba, kwanza aliponiambia nilipatwa na mshangao nikakata simu ghafla ila kama baada ya dakika moja nikampigia simu huku nikiwa na sauti iliyochangamka nikimwambia nimefurahi sana kwa taarifa za ujauzito, kwa kweli alishangaa kwani na nikaongeza kumwambia kua huo ndo mwanzo wa mimi nae kuishi pamoja. ila nilimwambia twende hospitali kuhakikisha ujauzito na kupewa ushauri wa kitabibu, hapo alijizungusha zaidi ya wiki tatu visingizio haviishi. ndipo baadae aliponiita na kuniambia kua yeye si mjamzito alitaka kuhakikisha km nampenda. Cha kushangaza baada ya hapo alianza kunifanyia visa na vituko vya hapa na pale, nashukuru Mungu niliweza kupita salama ktk kipindi cha upweke baada ya hapo ndipo nimeamua kuingia ktk harakati za kuoa
Kwa hiyo mara nyingine hawa wenzetu wanapima upendo kwa njia ambazo si sahihi sana na haziendani na uhalisia lakini bado lipo tumaini
 
we ni level za wakina shaban robert kaka.
 
Duuuh!



Pole sana HP kama ni kweli ila usikate tamaa, kila jambo na wakati wake, wakati wako ukifika utampata atakayekupenda kweli!
 
HOSEPOWER, we ni mkareeee....., i like the whole story.
 
nenda kauze hiyo story global publishers.....
 
Back
Top Bottom