Nimeishi Moshi, Bukoba, Lushoto aisee watanzania tuna ukarimu sana tofauti na tunavyoshambuliana kwa tofauti zetu


Hii ni [emoji817] mkuu. Tanzania tunatakiwa kushughulikia vitu viwili tu kwa sasa....uchawi(ushirikina) na unafiki (fitina).
 
Mkuu kumbe umeishi Lushoto (Lukozi) nipo hapa mwaka wa 2 sasa uenda nakufaham. Kuhusu ukarimu kuna mzee alishawahi kuniambia Tz ujamaa sana mpaka ukienda nchi za watu unaboreka.
 
Sijakaa maana Utu wa Mtu haujali Dini wala Kabila. Ila Huko Ulipita Hukuishi ndugu ulipita pita tu. Walioishi hasa Kikazi wanawajua Hao watu vizuri .

Wewe umekutana nao Mtaani Kama Raia tu kitu ambacho watanzania Wengi ukikutana nasi tunaonyeshaga Unafiki wa Upendo
 
Ruble kama Ruble ndio habari ya mjini[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ebu kajaribu zenji..uje utupe mrejesho..nenda huko vijijini halafu uanze kula mdudu ndio utajua tz hakuna amani bali utulivu.

#MaendeleoHayanaChama
yni huyu jamaa ni mdini kinoma yani nina mashaka na uwezo wako wa Akili ww
 
Kwenye kaz ndugu yangu ni katika kila eneo popote pale mambo ya fitina na kurogana na kuharibiana si wa maofisini mpaka huku akina sie wa iokote na kesho.
 
Wa huko Dar wamejaa roho mbaya na umaskini kiasi kwamba ukiwatembelea wanakuuliza unaondoka lini? Cha ajabu hapo umeshawabebea debe la mchele, maharage na mandizi yakutosha.
Sio roho mbaya ni hali ya maisha, usione mtu anakwambia mie nakula mara moja tu nikinywa chai basi mpaka jioni mmm hana kitu huyo
 
Ila mtwara mmm wao ukifika mgeni wanataka wale kwako, utasikia Mimi nitakupa nini wanyimi haswaa!
 
Dar nikama kokoro linalobeba kila kitu, labda huko nje ya mji wanakoishi wazaramo- manerumango huko, lakini uende mwenge mwenge ,ubungo masaki utegemee kupokewa kama mfalme uhuuu sahau labda ndugu yako ha ha ha !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…