Nimeishi na mwanamke miaka mitatu bila kupata mtoto, nifanyaje

Chancel Mbemba

Senior Member
Joined
Aug 15, 2025
Posts
109
Reaction score
121
Nimekuja hapa JamiiForums kuomba ushauri na msaada Kwa namna moja au nyingine, hapa nimekuwa nikisoma tu nyuzi za watu nilikuwa sina account na mimi nimeona nijiunge nitoe yanayonisibu labda nitapata msaada, hapa naamini ni sehemu sahihi japo kuna ambao sometimes wanaleta masikhara.

Ishu inayonisumbua ni kwamba nimekaa na mwanamke kwasasa takriban Miaka mi3 hatujafanikiwa kupata mtoto.

Tulishakwenda hospitali kupima wote tukaonekana tupo sawa hatuna shida (hospitali special za uzazi) pia mimi kwenye pita pita zangu maisha ya nyuma huko nishawahi kutia sana wanawake mimba.

Harakati zetu za kutafuta mtoto zilianza baada ya kukaa Kwa mwaka mzima bila mwanamke kupata ujauzito, ndio akaanza na dawa za kupevusha mayai na za hormone imbalance (hii ni baada ya kupima hospitali kuambiwa hatuna shida akashauriwa atumie hizo), baada ya kuona mwaka wa pili unaingia bilabila ikabidi tuhamie kwenye dawa za kienyeji za chango, kanywa Sana Lakini hatukupata matokeo.

Tukahamia Kwenye kuombewa, manabii, wachungaji wa madhehebu karibia YOTE ya kikristo ashaombewa, ilifika kipindi maji ya kunywa na mafuta ya kupikia tulikua tunachukulia Kwa mwamposa.

ikabidi sasa nitafute mtaalamu japokuwa hayo sio mambo yangu, nijaribu kuchekiwa(ramli) ili nijue Kwa upande wa pili kama kuna shida yoyote.

Hapa sasa ndio nikaja kuamini kuwa uchawi upo, niliwasiliana na mtaalamu wa kwanza (namba zake nilipewa na mshkaji wangu), nikamtumia majina yetu wote watatu ili aangalie nani ana shida, nilipomtumia baada ya nusu saa akanipigia akaniambia kaangalia kwa upande wangu hakuna shida ila tatizo lipo Kwa mwanamke amefungwa, akanielezea kama kuna ndoto anaota usiku nikamwambia ndio, akaniambia ana kitu cha kichawi kimefunga uzazi.

Kwakweli sikuamini, nikahisi labda huyo Mtu ananichezea akili, huyo anakaa mikoa ya kaskazini ikabidi nitafute mwingine wa mkoa tofauti kabisa (Mimi nakaa Dar).

Nilipotafuta mwingine wa mkoa tofauti, maajabu ni kwamba ALINIAMBIA KITU KILEKILE KAMA HUYO WA KWANZA😳, nilishangaa Sana nikahisi hawa watu wanajuana wanaambiana au?! Lakini mbona ni watu hawajuani kabisa??! Na wanakaa mikoa ya tofauti kabisa??

Sikuridhika na majibu ya hao wawili japo yanafanana, NIKATAFUTA MWINGINE WA TATU kutoka mkoa mwingine (wote hawa ni wale wanatibu kiarabu, masheikh)

Huyu wa tatu nae alinipa majibu yaleyale kama ya wale wawili wa mwanzo, hapo ndio nikaamini, nikachukue hatua ya kwenda kwa yule wa kwanza ili huyu mwanamke atibiwe.

Kufupisha story, baada ya kwenda kutibiwa Kwa huyo wa kwanza, akapata nafuu Kwa kutokuota ndoto mbaya Kwa miezi mitatu tuu lakini mimba haikushika, baada ya miezi mitatu ndio ikawa kama tumechokoza kwani alikuwa akiota ndoto za kutisha mara nyingine anaota anaingiliwa.

Nilienda Kwa wote hao lakini HATUKUFANIKIWA, na pia nilienda Kwa wataalamu wengine nao wakaniambia amefungwa, tukajaribu na huko lakini hatujafanikiwa mpaka sasa.

Nikiwaza nimuache roho inakua nzito kwani ni Mwanamke alietulia Hana mambo mengi ya kimjinimjini (nilitoka nae mkoani), nawaza kurudi tena kutafuta alietulia kama huyu inaweza kuwa kazi ngumu sana kwa maisha ya sasa hivi.

Naombeni msaada wenu, najua hii kitu wapo waliopitia ambao wapo hapa JF, kwa ambao mlishawahi kupitia hili mkatoboa nakaribisha ushauri.

Tokea nimeanza kuhangaikia hii ishu nimecalculate nimetumia zaidi ya millioni 5 Kwa nauli za kwenda mikoani na kulipa wataalamu.

Kwa upande wa Imani Sisi ni wakristo na yeye anazingatia maombi hata Mimi kumpeleka Kwa wataalamu ilikuwa mbinde kwani alikua haamini hayo mambo, ikumbukwe ashaombewa sana, kwa manabii na wachungaji pia tulishaenda sana tulipooona hamna suluhisho ndio tukaanza kwenda upande wa pili.

Kama kuna Mtu atanipatia suluhisho la kunipa connection ya mtaalamu wa uhakika ambae atamtibia akishapona ndio tunalipa nitashukuru Sana, atakaenipa hiyo connection kama akitibika kweli nitampatia hata 500K ya maji.

Mambo haya yanaumiza, hapa nilipo Niko makazi mapya, tulipokua tunakaa mwanzo tuliondoka kwasababu ya maneno ya watu.

Haya mambo yanaumiza vibaya mno, kunajirani yangu alishawahi Kukaa Miaka 10 ndio wakafanikiwa, kuzaa nnje ya ndoa ndio kitu sijakifiria kabisa.

NATAMANI WAJITOKEZE WATU AMBAO WASHAPITIA HUU MSOTO TUPEANE EXPERIENCE NA NAMNA WALIVYOJINASUA.
 
Najibia kichwa ya uzi

Mkiacha kuweka mawazo yenu yoteee kwenye hili mtashangaa mtoto anakuja fasta.. Hii usemwa ni muhimu sanaaaaaaaaaa.. Hivyo kila mmoja wenu atulie.. Nawe mwanaume muonyeshe mwenzako kwamba hauna hofu na hasira yoyote.. unampenda na hauta anza kuchepuka au kumuaga kisa kuto pata mtoto.. Lazima awe na Furaha na Amani sanaaaa moyoni na tie Moyo kuwa Muda wa Mola unakuja.
 
pole sana mtoa mada,

lakini hao waganga ulikua unawapa taarifa za tatizo ndo wanakueleza hayo au unawapa taarifa ya jumla tu kwamba hilo tatizo wanaligundua wenyewe bila ya nyinyi kuwaamboia mnatatizo gani?


pia nakutakia kila la kheri
 
Pole sana.
 
Umeshaenda hospital wataalam wamesema hamna shida mnaenda Kwa waganga kufanya nini? Miaka mi3 tu ushazunguka kiasi hicho?
Mitatu mingi Sana mkuu, na Kama nilivyoandika hapa shida imeshaonekana ipo upande gani
 
pole sana mtoa mada,

lakini hao waganga ulikua unawapa taarifa za tatizo ndo wanakueleza hayo au unawapa taarifa ya jumla tu kwamba hilo tatizo wanaligundua wenyewe bila ya nyinyi kuwaamboia mnatatizo gani?


pia nakutakia kila la kheri
Swali zuri, NILIKUA NAWAAMBIA KUA TUNATAKA KUANGALIWA RAMLI MAANA MWANAMKE ANAOTA NDOTO MBAYA USIKU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…