Nimeishi na mwanamke miaka mitatu bila kupata mtoto, nifanyaje

Nimeishi na mwanamke miaka mitatu bila kupata mtoto, nifanyaje

1.mruhusu kuchepuka ipo siku utaamini hajafungwa ila kuna factor hukizi,
2.Kama anaweza aje nimbebeshe mimba ya kwanza mimi,ila gharama za nauli na kulala juu yenu,
 
Nimekuja hapa JamiiForums kuomba ushauri na msaada Kwa namna moja au nyingine, hapa nimekuwa nikisoma tu nyuzi za watu nilikuwa sina account na mimi nimeona nijiunge nitoe yanayonisibu labda nitapata msaada, hapa naamini ni sehemu sahihi japo kuna ambao sometimes wanaleta masikhara.

Ishu inayonisumbua ni kwamba nimekaa na mwanamke kwasasa takriban Miaka mi3 hatujafanikiwa kupata mtoto.

Tulishakwenda hospitali kupima wote tukaonekana tupo sawa hatuna shida (hospitali special za uzazi) pia mimi kwenye pita pita zangu maisha ya nyuma huko nishawahi kutia sana wanawake mimba.

Harakati zetu za kutafuta mtoto zilianza baada ya kukaa Kwa mwaka mzima bila mwanamke kupata ujauzito, ndio akaanza na dawa za kupevusha mayai na za hormone imbalance (hii ni baada ya kupima hospitali kuambiwa hatuna shida akashauriwa atumie hizo), baada ya kuona mwaka wa pili unaingia bilabila ikabidi tuhamie kwenye dawa za kienyeji za chango, kanywa Sana Lakini hatukupata matokeo.

Tukahamia Kwenye kuombewa, manabii, wachungaji wa madhehebu karibia YOTE ya kikristo ashaombewa, ilifika kipindi maji ya kunywa na mafuta ya kupikia tulikua tunachukulia Kwa mwamposa.

ikabidi sasa nitafute mtaalamu japokuwa hayo sio mambo yangu, nijaribu kuchekiwa(ramli) ili nijue Kwa upande wa pili kama kuna shida yoyote.

Hapa sasa ndio nikaja kuamini kuwa uchawi upo, niliwasiliana na mtaalamu wa kwanza (namba zake nilipewa na mshkaji wangu), nikamtumia majina yetu wote watatu ili aangalie nani ana shida, nilipomtumia baada ya nusu saa akanipigia akaniambia kaangalia kwa upande wangu hakuna shida ila tatizo lipo Kwa mwanamke amefungwa, akanielezea kama kuna ndoto anaota usiku nikamwambia ndio, akaniambia ana kitu cha kichawi kimefunga uzazi.

Kwakweli sikuamini, nikahisi labda huyo Mtu ananichezea akili, huyo anakaa mikoa ya kaskazini ikabidi nitafute mwingine wa mkoa tofauti kabisa (Mimi nakaa Dar).

Nilipotafuta mwingine wa mkoa tofauti, maajabu ni kwamba ALINIAMBIA KITU KILEKILE KAMA HUYO WA KWANZA😳, nilishangaa Sana nikahisi hawa watu wanajuana wanaambiana au?! Lakini mbona ni watu hawajuani kabisa??! Na wanakaa mikoa ya tofauti kabisa??

Sikuridhika na majibu ya hao wawili japo yanafanana, NIKATAFUTA MWINGINE WA TATU kutoka mkoa mwingine (wote hawa ni wale wanatibu kiarabu, masheikh)

Huyu wa tatu nae alinipa majibu yaleyale kama ya wale wawili wa mwanzo, hapo ndio nikaamini, nikachukue hatua ya kwenda kwa yule wa kwanza ili huyu mwanamke atibiwe.

Kufupisha story, baada ya kwenda kutibiwa Kwa huyo wa kwanza, akapata nafuu Kwa kutokuota ndoto mbaya Kwa miezi mitatu tuu lakini mimba haikushika, baada ya miezi mitatu ndio ikawa kama tumechokoza kwani alikuwa akiota ndoto za kutisha mara nyingine anaota anaingiliwa.

Nilienda Kwa wote hao lakini HATUKUFANIKIWA, na pia nilienda Kwa wataalamu wengine nao wakaniambia amefungwa, tukajaribu na huko lakini hatujafanikiwa mpaka sasa.

Nikiwaza nimuache roho inakua nzito kwani ni Mwanamke alietulia Hana mambo mengi ya kimjinimjini (nilitoka nae mkoani), nawaza kurudi tena kutafuta alietulia kama huyu inaweza kuwa kazi ngumu sana kwa maisha ya sasa hivi.

Naombeni msaada wenu, najua hii kitu wapo waliopitia ambao wapo hapa JF, kwa ambao mlishawahi kupitia hili mkatoboa nakaribisha ushauri.

Tokea nimeanza kuhangaikia hii ishu nimecalculate nimetumia zaidi ya millioni 5 Kwa nauli za kwenda mikoani na kulipa wataalamu.

Kwa upande wa Imani Sisi ni wakristo na yeye anazingatia maombi hata Mimi kumpeleka Kwa wataalamu ilikuwa mbinde kwani alikua haamini hayo mambo, ikumbukwe ashaombewa sana, kwa manabii na wachungaji pia tulishaenda sana tulipooona hamna suluhisho ndio tukaanza kwenda upande wa pili.

Kama kuna Mtu atanipatia suluhisho la kunipa connection ya mtaalamu wa uhakika ambae atamtibia akishapona ndio tunalipa nitashukuru Sana, atakaenipa hiyo connection kama akitibika kweli nitampatia hata 500K ya maji.

Mambo haya yanaumiza, hapa nilipo Niko makazi mapya, tulipokua tunakaa mwanzo tuliondoka kwasababu ya maneno ya watu.

Haya mambo yanaumiza vibaya mno, kunajirani yangu alishawahi Kukaa Miaka 10 ndio wakafanikiwa, kuzaa nnje ya ndoa ndio kitu sijakifiria kabisa.

NATAMANI WAJITOKEZE WATU AMBAO WASHAPITIA HUU MSOTO TUPEANE EXPERIENCE NA NAMNA WALIVYOJINASUA.
Pole sana. Mlishajaribu kwenda kwa Kuhani Musa KImara Temboni?? Kama bado jaribuni kwenda huko
 
Duuh! Hizi akili nyingine bhana. 😀😀 sasa ndio ushauri gani huu?!😆😆
Suala si anataka mtoto na watoto, ninauhakika yeye ndo anakasoro ambayo tiba yake mke wake abebeshwe mtoto wa kwanza na mwamba mwenye nguvu,group O+ blood, damu kaliiii na awe fundi akamie haswaaa,siku ya hatari kati ya 13 na 14 tuuu
 
Mjaribu mbinu ya kupandikiza, ytoa mbegu harafu akawekewe ukeni hili hufanyika kitaalamu baada ya kufuatilia mzunguko wa mkeo, ongea na daktari wa uzazi
 
1.mruhusu kuchepuka ipo siku utaamini hajafungwa ila kuna factor hukizi,
2.Kama anaweza aje nimbebeshe mimba ya kwanza mimi,ila gharama za nauli na kulala juu yenu,
Nadhani haujaelewa au ni uandishi wangu Mbovu , lakini nlishaandika hapo kua tulishapata vipimo vyote kutoka Kwa specialist wa uzazi tukaambiwa wote tupo vizuri
 
Kuliko kuhangaika kote kwanini usiende muhimbili pale wapandikize mbegu milioni kumi mpaka ishirini.IVF KIJUX.
 
Potezeeni hizo ishu mtoto atakuja tu na kuweni positive,ukitaka sana kitu huwa hakiji kabisa lakin ukirelax tu huna hili wala lile unapata unachotaka
 
Potezeeni hizo ishu mtoto atakuja tu na kuweni positive,ukitaka sana kitu huwa hakiji kabisa lakin ukirelax tu huna hili wala lile unapata unachotaka
 
Wewe kama kweli unashida nitafute nikuunganishe na mtaalam( sio mganga) ni tabibu anaefanya tiba kwa miti shamba baadhi wa shida kama yako wamefanikiwa lakini pia usiache kuomba Allah
PM yangu IPO wazi kaka, nakudm
 
Fuatilia kiundani mahusiano ya wazazi wa mke wako yalikuaje/yakoje?
Mama yake alimtoa kwa baba yake kiujanja janja?
Je,anaye baba ama anasikaga story tu?

Kama njoo kikashani ikiwa hayo niliyouliza yanalandana na background ya mkeo.
 
Usiamini waganga,mtu anayeenda kwa waganga ajiandae kuwa mwanga pia
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Huwajui waganga wewe.
Mna uhakika damu zenu zinaendana?
Damu zikikataana hampati mtoto ng'o
 
Una option 2:

1. Mpe kianzio cha Maisha na mahali pa kukaa muache, ungekuwa usimamishi asingekuvumilia hata kidogo.

2. Tafuta Nyumba ndogo kazae huko uwe na wake wawili, Kuna familia Zina Siri nyingi sana huna haja ya kuteseka.

3. Rejea option mbili hapo Juu kama hutaki kuendelea kupata hasara!
 
Una option 2:

1. Mpe kianzio cha Maisha na mahali pa kukaa muache, ungekuwa usimamishi asingekuvumilia hata kidogo.

2. Tafuta Nyumba ndogo kazae huko uwe na wake wawili, Kuna familia Zina Siri nyingi sana huna haja ya kuteseka.
Asante Kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
Back
Top Bottom