Nimeishi na mwanamke miaka mitatu bila kupata mtoto, nifanyaje

Nimekuja hapa JamiiForums kuomba ushauri na msaada Kwa namna moja au nyingine, hapa nimekuwa nikisoma tu nyuzi za watu nilikuwa sina account na mimi nimeona nijiunge nitoe yanayonisibu labda nitapata msaada, hapa naamini ni sehemu sahihi japo kuna ambao sometimes wanaleta masikhara.

Ishu inayonisumbua ni kwamba nimekaa na mwanamke kwasasa takriban Miaka mi3 hatujafanikiwa kupata mtoto.

Tulishakwenda hospitali kupima wote tukaonekana tupo sawa hatuna shida (hospitali special za uzazi) pia mimi kwenye pita pita zangu maisha ya nyuma huko nishawahi kutia sana wanawake mimba.

Harakati zetu za kutafuta mtoto zilianza baada ya kukaa Kwa mwaka mzima bila mwanamke kupata ujauzito, ndio akaanza na dawa za kupevusha mayai na za hormone imbalance (hii ni baada ya kupima hospitali kuambiwa hatuna shida akashauriwa atumie hizo), baada ya kuona mwaka wa pili unaingia bilabila ikabidi tuhamie kwenye dawa za kienyeji za chango, kanywa Sana Lakini hatukupata matokeo.

Tukahamia Kwenye kuombewa, manabii, wachungaji wa madhehebu karibia YOTE ya kikristo ashaombewa, ilifika kipindi maji ya kunywa na mafuta ya kupikia tulikua tunachukulia Kwa mwamposa.

ikabidi sasa nitafute mtaalamu japokuwa hayo sio mambo yangu, nijaribu kuchekiwa(ramli) ili nijue Kwa upande wa pili kama kuna shida yoyote.

Hapa sasa ndio nikaja kuamini kuwa uchawi upo, niliwasiliana na mtaalamu wa kwanza (namba zake nilipewa na mshkaji wangu), nikamtumia majina yetu wote watatu ili aangalie nani ana shida, nilipomtumia baada ya nusu saa akanipigia akaniambia kaangalia kwa upande wangu hakuna shida ila tatizo lipo Kwa mwanamke amefungwa, akanielezea kama kuna ndoto anaota usiku nikamwambia ndio, akaniambia ana kitu cha kichawi kimefunga uzazi.

Kwakweli sikuamini, nikahisi labda huyo Mtu ananichezea akili, huyo anakaa mikoa ya kaskazini ikabidi nitafute mwingine wa mkoa tofauti kabisa (Mimi nakaa Dar).

Nilipotafuta mwingine wa mkoa tofauti, maajabu ni kwamba ALINIAMBIA KITU KILEKILE KAMA HUYO WA KWANZA😳, nilishangaa Sana nikahisi hawa watu wanajuana wanaambiana au?! Lakini mbona ni watu hawajuani kabisa??! Na wanakaa mikoa ya tofauti kabisa??

Sikuridhika na majibu ya hao wawili japo yanafanana, NIKATAFUTA MWINGINE WA TATU kutoka mkoa mwingine (wote hawa ni wale wanatibu kiarabu, masheikh)

Huyu wa tatu nae alinipa majibu yaleyale kama ya wale wawili wa mwanzo, hapo ndio nikaamini, nikachukue hatua ya kwenda kwa yule wa kwanza ili huyu mwanamke atibiwe.

Kufupisha story, baada ya kwenda kutibiwa Kwa huyo wa kwanza, akapata nafuu Kwa kutokuota ndoto mbaya Kwa miezi mitatu tuu lakini mimba haikushika, baada ya miezi mitatu ndio ikawa kama tumechokoza kwani alikuwa akiota ndoto za kutisha mara nyingine anaota anaingiliwa.

Nilienda Kwa wote hao lakini HATUKUFANIKIWA, na pia nilienda Kwa wataalamu wengine nao wakaniambia amefungwa, tukajaribu na huko lakini hatujafanikiwa mpaka sasa.

Nikiwaza nimuache roho inakua nzito kwani ni Mwanamke alietulia Hana mambo mengi ya kimjinimjini (nilitoka nae mkoani), nawaza kurudi tena kutafuta alietulia kama huyu inaweza kuwa kazi ngumu sana kwa maisha ya sasa hivi.

Naombeni msaada wenu, najua hii kitu wapo waliopitia ambao wapo hapa JF, kwa ambao mlishawahi kupitia hili mkatoboa nakaribisha ushauri.

Tokea nimeanza kuhangaikia hii ishu nimecalculate nimetumia zaidi ya millioni 5 Kwa nauli za kwenda mikoani na kulipa wataalamu.

Kwa upande wa Imani Sisi ni wakristo na yeye anazingatia maombi hata Mimi kumpeleka Kwa wataalamu ilikuwa mbinde kwani alikua haamini hayo mambo, ikumbukwe ashaombewa sana, kwa manabii na wachungaji pia tulishaenda sana tulipooona hamna suluhisho ndio tukaanza kwenda upande wa pili.

Kama kuna Mtu atanipatia suluhisho la kunipa connection ya mtaalamu wa uhakika ambae atamtibia akishapona ndio tunalipa nitashukuru Sana, atakaenipa hiyo connection kama akitibika kweli nitampatia hata 500K ya maji.

Mambo haya yanaumiza, hapa nilipo Niko makazi mapya, tulipokua tunakaa mwanzo tuliondoka kwasababu ya maneno ya watu.

Haya mambo yanaumiza vibaya mno, kunajirani yangu alishawahi Kukaa Miaka 10 ndio wakafanikiwa, kuzaa nnje ya ndoa ndio kitu sijakifiria kabisa.

NATAMANI WAJITOKEZE WATU AMBAO WASHAPITIA HUU MSOTO TUPEANE EXPERIENCE NA NAMNA WALIVYOJINASUA.
Pole sana aisee ni kawaida sana na wewe siyo wa.kwanza kwa changamoto.hii
 
Pole Sana mkuu..
Mdogo wangu Mimi(KE) alikumbwa na kadhia hiyo na mume wake wamezunguka kama wewe Tu ..
Walisota Tangu 2020 nikaingilia Kati nikampeleka dogo sehemu .. Mungu NI mwema mwaka Jana kapata mtoto wa Kwanza . Navoongea hapa tena anaweek moja kapata tena mtoto wa pili . ..
Nicheki PM mkuu. .
 
Hao matapeli wanaojiita manabii watakupiga tu hela, na hao waganga huwa hawaondoi tatizo ila wanatengeneza tatizo jipya ili uwe mteja wao wa kudumu.

Tafuta imani sahihi uishikilie acha kuchanganya mambo , Hospital umeambiwa hamna tatizo tulia muombe Mungu ataondoa mitihani.
 
Sawa kaka shukrani sana
 
Pole Sana mkuu..
Mdogo wangu Mimi(KE) alikumbwa na kadhia hiyo na mume wake wamezunguka kama wewe Tu ..
Walisota Tangu 2020 nikaingilia Kati nikampeleka dogo sehemu .. Mungu NI mwema mwaka Jana kapata mtoto wa Kwanza . Navoongea hapa tena anaweek moja kapata tena mtoto wa pili . ..
Nicheki PM mkuu. .
Sawa kaka
 
Achana na hizo issues za majirani wanasema Nini
Kaa chini na mkeo na mkubaliane kuenjoy maisha kwa style yenu
Kaa mbali na watu wenye negativity kama hao majirani wanaowasema vibaya
Mambo yatajipa tu
Duh asante Sana kaka Mungu akubariki Kwa ushauri huu
 
Nenda kapime na wewe
Ukijikuta wewe hauna shida tafuta mwanamke pembeni zaa nae na funga domo lako ila tafuta mwanamke muelewa sana na asiye na makuu na umtolee ile mahari ya kuanzia ili usipate shida
Watoto hawapatikani kwa ushirikina
 
Nenda kapime na wewe
Ukijikuta wewe hauna shida tafuta mwanamke pembeni zaa nae na funga domo lako ila tafuta mwanamke muelewa sana na asiye na makuu na umtolee ile magari ya kuanzia ili usipate shida
Watoto hawapatikani kwa ushirikina
Sawa mkuu shukrani
 
Nimekuja hapa JamiiForums kuomba ushauri na msaada Kwa namna moja au nyingine, hapa nimekuwa nikisoma tu nyuzi za watu nilikuwa sina account na mimi nimeona nijiunge nitoe yanayonisibu labda nitapata msaada, hapa naamini ni sehemu sahihi japo kuna ambao sometimes wanaleta masikhara.

Ishu inayonisumbua ni kwamba nimekaa na mwanamke kwasasa takriban Miaka mi3 hatujafanikiwa kupata mtoto.

Tulishakwenda hospitali kupima wote tukaonekana tupo sawa hatuna shida (hospitali special za uzazi) pia mimi kwenye pita pita zangu maisha ya nyuma huko nishawahi kutia sana wanawake mimba.

Harakati zetu za kutafuta mtoto zilianza baada ya kukaa Kwa mwaka mzima bila mwanamke kupata ujauzito, ndio akaanza na dawa za kupevusha mayai na za hormone imbalance (hii ni baada ya kupima hospitali kuambiwa hatuna shida akashauriwa atumie hizo), baada ya kuona mwaka wa pili unaingia bilabila ikabidi tuhamie kwenye dawa za kienyeji za chango, kanywa Sana Lakini hatukupata matokeo.

Tukahamia Kwenye kuombewa, manabii, wachungaji wa madhehebu karibia YOTE ya kikristo ashaombewa, ilifika kipindi maji ya kunywa na mafuta ya kupikia tulikua tunachukulia Kwa mwamposa.

ikabidi sasa nitafute mtaalamu japokuwa hayo sio mambo yangu, nijaribu kuchekiwa(ramli) ili nijue Kwa upande wa pili kama kuna shida yoyote.

Hapa sasa ndio nikaja kuamini kuwa uchawi upo, niliwasiliana na mtaalamu wa kwanza (namba zake nilipewa na mshkaji wangu), nikamtumia majina yetu wote watatu ili aangalie nani ana shida, nilipomtumia baada ya nusu saa akanipigia akaniambia kaangalia kwa upande wangu hakuna shida ila tatizo lipo Kwa mwanamke amefungwa, akanielezea kama kuna ndoto anaota usiku nikamwambia ndio, akaniambia ana kitu cha kichawi kimefunga uzazi.

Kwakweli sikuamini, nikahisi labda huyo Mtu ananichezea akili, huyo anakaa mikoa ya kaskazini ikabidi nitafute mwingine wa mkoa tofauti kabisa (Mimi nakaa Dar).

Nilipotafuta mwingine wa mkoa tofauti, maajabu ni kwamba ALINIAMBIA KITU KILEKILE KAMA HUYO WA KWANZA😳, nilishangaa Sana nikahisi hawa watu wanajuana wanaambiana au?! Lakini mbona ni watu hawajuani kabisa??! Na wanakaa mikoa ya tofauti kabisa??

Sikuridhika na majibu ya hao wawili japo yanafanana, NIKATAFUTA MWINGINE WA TATU kutoka mkoa mwingine (wote hawa ni wale wanatibu kiarabu, masheikh)

Huyu wa tatu nae alinipa majibu yaleyale kama ya wale wawili wa mwanzo, hapo ndio nikaamini, nikachukue hatua ya kwenda kwa yule wa kwanza ili huyu mwanamke atibiwe.

Kufupisha story, baada ya kwenda kutibiwa Kwa huyo wa kwanza, akapata nafuu Kwa kutokuota ndoto mbaya Kwa miezi mitatu tuu lakini mimba haikushika, baada ya miezi mitatu ndio ikawa kama tumechokoza kwani alikuwa akiota ndoto za kutisha mara nyingine anaota anaingiliwa.

Nilienda Kwa wote hao lakini HATUKUFANIKIWA, na pia nilienda Kwa wataalamu wengine nao wakaniambia amefungwa, tukajaribu na huko lakini hatujafanikiwa mpaka sasa.

Nikiwaza nimuache roho inakua nzito kwani ni Mwanamke alietulia Hana mambo mengi ya kimjinimjini (nilitoka nae mkoani), nawaza kurudi tena kutafuta alietulia kama huyu inaweza kuwa kazi ngumu sana kwa maisha ya sasa hivi.

Naombeni msaada wenu, najua hii kitu wapo waliopitia ambao wapo hapa JF, kwa ambao mlishawahi kupitia hili mkatoboa nakaribisha ushauri.

Tokea nimeanza kuhangaikia hii ishu nimecalculate nimetumia zaidi ya millioni 5 Kwa nauli za kwenda mikoani na kulipa wataalamu.

Kwa upande wa Imani Sisi ni wakristo na yeye anazingatia maombi hata Mimi kumpeleka Kwa wataalamu ilikuwa mbinde kwani alikua haamini hayo mambo, ikumbukwe ashaombewa sana, kwa manabii na wachungaji pia tulishaenda sana tulipooona hamna suluhisho ndio tukaanza kwenda upande wa pili.

Kama kuna Mtu atanipatia suluhisho la kunipa connection ya mtaalamu wa uhakika ambae atamtibia akishapona ndio tunalipa nitashukuru Sana, atakaenipa hiyo connection kama akitibika kweli nitampatia hata 500K ya maji.

Mambo haya yanaumiza, hapa nilipo Niko makazi mapya, tulipokua tunakaa mwanzo tuliondoka kwasababu ya maneno ya watu.

Haya mambo yanaumiza vibaya mno, kunajirani yangu alishawahi Kukaa Miaka 10 ndio wakafanikiwa, kuzaa nnje ya ndoa ndio kitu sijakifiria kabisa.

NATAMANI WAJITOKEZE WATU AMBAO WASHAPITIA HUU MSOTO TUPEANE EXPERIENCE NA NAMNA WALIVYOJINASUA.
Jaribu Kwampalange kamanda.
 
Pole Sana mkuu..
Mdogo wangu Mimi(KE) alikumbwa na kadhia hiyo na mume wake wamezunguka kama wewe Tu ..
Walisota Tangu 2020 nikaingilia Kati nikampeleka dogo sehemu .. Mungu NI mwema mwaka Jana kapata mtoto wa Kwanza . Navoongea hapa tena anaweek moja kapata tena mtoto wa pili . ..
Nicheki PM mkuu. .
Kwahiyo mdogo wako ameamua kubemenda mtoto. Ndani ya miaka 2 watoto wawili.
 
Back
Top Bottom