Nimeishi Urusi najua Tamaduni zake, pamoja na Ukubwa wa Jeshi lake Rushwa ndiyo inawafanya wasikamilishe malengo kwa muda

Nimeishi Urusi najua Tamaduni zake, pamoja na Ukubwa wa Jeshi lake Rushwa ndiyo inawafanya wasikamilishe malengo kwa muda

Nchini Russia kuna sabotage inaendelea ya kuungua Kwa majengo muhimu ya serikali hii ni siku ya 5 mfululizo baadhi ya majengo yanaungua Moto..... Putin Akili yake na nguvu zake amezielekeza Ukraine lkn ndani ya nchi yake kuna watu wanamsumbua Sana hasa kwenye ishu za usaliti.

Alafu western countries hawajafunga balozi zao ingawa wanagombana kuhusu mafuta na gesi hii inapelekea kufanya njama za kijasusi ili wapate Siri na mbinu anazotumia vitani.
Acha tusubiri tuone mbele ya safari itakuaje
 
Nimekuwa Russia tokea mwaka 2008 hadi 2011 alafu nikaenda Peru Na baadae kurejea Russia 2013

Russia ina rasilimali nyingi sana, ardhi hakika imebarikiwa. Russia ina historia, Russia ina utamaduni. Russia ina watu washindani wenye kuichangamsha dunia kwa kuipa ladha.

Tatizo kubwa linaloiumiza Russia ni Rushwa. Tatizo hili ndiyo chanzo cha hata huu utendaji wa hovyo ulioonyeshwa na Jeshi lake.
Russia imejitahidi sana kuwekeza kwenye huduma za kijamii.

Ukiungalia mtandao wa huduma za afya nchini Russia upo vizuri kuliko Marekani, Russia wamejenga health facilities na kuweka vitanda n.k, lakini huduma ni mbovu.

Wafanyakazi wanafanya kazi kimazoea, serikali kuu yenyewe hakuna transperency. Labda ndiyo ya mwisho barani ulaya kwa kutokuwa na transperency.

Uimarishaji wa Jeshi lake mao unaathiriwa na Rushwa, mafunzo na vitendea kazi ni Rushwa tupu, matokeo yake mafunzo yanakuwa ni yale yasiyo na ubora.

Uundwaji wa mifumi na silaha za kujeshi unawekewa magharama makubwa makubwa, lakini ubora wake unatia mashska sana. Huko kwenye silaha na mifumo ya ulinzi ndiyo watu wanapopigia hela kiulaini sana.

Military research ni njia nyingine ya kupigia hela.

Rushwa ndani Russia ni kama salaam tu. Kati ya nchi 180 duniani Russia ina rank namba 136 kwa kiwango kidogo cha Rushwa.

Kwa nafasi hiyo anayoshika Russia usitarajie lolote at all, ni taifa ambalo lina malizia zama zake

Leo hii tunaona tunaambiwa Kwamba ni jeshi kubwa Sana Duniani kama inavyojipambanua , lakin kuna harufu Ya rushwa Na sabotage kwenye Mäli Na mipango Ya jeshi.

Kuna kusaliti kambi Sana kwa kupewa ahadi Na Mali kwa Wanajeshi Na wapiganaji wanaounga mkono Urusi.

UNPROGRESS OF RUSSIA
Hii ngoma inapokwenda si mchezo. Russia wanafanikiwa kutangaza kuteka eneo, lakin hawamalizi siku mbili hapo, kwani uKrainians wanaenda kulichukua tena.

Kherson ilianguka juzi ma Russia wakawa wame take full control na kuanzisha mchakato wa kuwalazimisha watu wa Kherson wapige kura ya kujitenga na Ukraine.

Sasa hivi imeshabadilika tena, Ukraine wameshaanza kurudisha baadhi ya maeneo huko kherson, wakielekea upande wa Mariupol ili kuunganisha maeneo wanayoyateka kutokea Kherson.

Wakati Ukranians wakiielekea Mariupol kutokea Khersons, kumbuka ndani ya Mariupol kuna askari takriban 2,000 wa Russia, akari hao watalazimika kupambana na vikosi hivyo vya Ukraine, kumbuka ndani ya Mariupol kuna takriban akari 700 wa Ukraine ndani ya kile kiwanda, hapo Russian atajikuta analazimika kupambana na Ukranians wanaotokea Kherson kuja Mariupol halafu wale wa kuwandani nao watalianzisha kitu kitakachopelekea Russia wagawanyike ili kuweza kuwakabili.

Russia hapa anazidiwa akili, ili kuweza kupigana na kuendelea kuikamata Mariupol, atalazimika kuligawanya Jeshi lake, ili kuongeza askari zaidi Mariupol, kitendo cha kupunguza askari maenro mengine itakuwa ni sawa na kuyaachia maeneo hayo au kukunali kuuawa kwa askari wake watskaobaki maeneo hayo.

Ukranians wameshajua, maeneo mengi ambayo Russia wameyateka huwa hawana uwezo wala amani ya kuwepo hapo sababu huwa hawakai sana kabla hayajarudishwa, hivyo kuna kipindi huyaacha maeneo hayo ili baadaye waje kuwazunguka. Mbinu hii ya kuzungukwa, Russia wameipenda na wao wameanza kuitumia lakini kila wakijaribu kuzunguka, miduara haikamiliki huishia kukatwa au upungufu wa askari kwa wakati huo hupelekea waishie kuuawa tu.

Wakati Russia anaenda kuivamia Ukraine, alituma askari 150,000, ngoma ikabadilika, askari wa Russia 15,000 wameuawa, sasa hivi jumla ya askari waliopelekwa na Russia nchini Ukraine ni 300,000

Ntaeleweka hapo December December hapo 2022

Britanicca
Uliishi Urusi ya Tandahimba
 
Sawa mkuu tumeshajua umefika Russia.
Hofu yangu itakuwa Russia ya Gongolamboto. Na yale makombora yakutungulia ndege yalipolipuka yalikuathiri kiasi chakudhani umefika Russia ya kweli

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
Gongolamboto Kote huko
Tandahimba Kwenye Korosho kule
 
Ni mimi Yule Yule ila twitter panataka utumie sentence fupi kisamarize kilicho kichwani
Hakuna uwanja wa kujieleza Kama hapa! Pia twitter vijana wana pewa attention sana wale wa hovyo kisa kaongea upuuzi wanapata likes za kijinga na followers!

Nami nauliza swali we ndo Dr Lwaitama wa UDSM?
Hahaha! Kwa jinsi ulivyoandika tu hapa napata kujua kuwa huko kichwani mwako ni hewa! Ikiwa kama mtu utashindwa kuandika summary ili kufikisha ujumbe kama ulivyokusudia basi sina shaka kabisaa ww huna uwezo kabisa wa kuandika na kufanya tafiti! Kama hujui hata kuandika inclusive abstract! Wewe ni hewa kabisaa!
 
Leo umezungumza ukweli mkuu majamaa inaonekana yanapenda sana rushwa kama makenya akina MK254 yalifikia hatua ya kuwauzia adui zao alshabab siraha
Kifaru cha Urus sasa kinauzwa dola elfu 5 wapiganaji wa Russia wanakuachia na yale magari yenye makombora masafa marefu kila gari dola elfu 10 wanachukua na kujifanya wametekwa hawataki kurudi Russia ukiwapa watauawa!!!

Ndege za kivita dola laki moja mrusi anatua bila kuachia mabomu anakabidhi ndege na mibomu yote intact anakwambia mishahara midogo jeshini wakubwa wanakula kwa urefu wa kamba zao .Putin na magenerali wa Jeshi Sisi huku chini choka mbaya nipe ila usinirudishe Urusi

Ila Urusi sirudi hata ukitaka heri uniue wewe
 
Kifaru cha Urus sasa kinauzwa dola elfu 5 wapiganaji wa Russia wanakuachia na yale magari yenye makombora masafa marefu kila gari dola elfu 10 wanachukua na kujifanya wametekwa hawataki kurudi Russia ukiwapa watauawa!!!

Ndege za kivita dola laki moja mrusi anatua bila kuachia mabomu anakabidhi ndege na mibomu yote intact anakwambia mishahara midogo jeshini wakubwa wanakula kwa urefu wa kamba zao .Putin na magenerali wa Jeshi Sisi huku chini choka mbaya nipe ila usinirudishe Urusi

Ila Urusi sirudi hata ukitaka heri uniue wewe
Leta sosi
 
Britanicca napenda sana Kukusoma hapa Lakin nauliza kwanza Hivi ndo wewe Britanicca wa twitter? Wa twitter Mbona anaonekana kupwaya sana ?

Ulivyosema kuna ukweli fulani ndani yake mara zote Urusi , UKRAINE na nchi zilizokuwa chini ya USSR Rushwa iko juu sana na Kwa mambo ya Msingi

Na hii tulikuwa kwenye Kongamano chuoni St. Petersburg mwaka 2006 tulilugusia


Endelea na Uchambuzi wako wa mambo


Mwalimu Lwaitama
Mwl wewe ndye yulemuhadhir msaafu AZAVAEL LWAITAMA ?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Leo umezungumza ukweli mkuu majamaa inaonekana yanapenda sana rushwa kama makenya akina MK254 yalifikia hatua ya kuwauzia adui zao alshabab siraha

Ha ha ha!!! Usipende sana kuelekeza kidole bila kujikagua, Tanzania isingekua kwa rushwa leo hii ingekua mbali sana kiuchumi kwenye level ya akina Afrika Kusini, maana ina raslimali nyingi sana madini ya kumwaga, ila leo hii mara unanskia sijui jiwe la rubi lipo Ulaya limetokea Tanzania kwa kupitia figisufigisu.
 
Back
Top Bottom