Nimeitwa Shetani baada ya kutoa ushauri ambao nimeombwa. Nikirudishia haya matusi najua tu itakuwa issue kwa ndugu

Nimeitwa Shetani baada ya kutoa ushauri ambao nimeombwa. Nikirudishia haya matusi najua tu itakuwa issue kwa ndugu

Ni kweli kwa ugonjwa alionao uwezekano wa kupona kibinadamu ni mdogo! Isipokuwa kama wataalamu wameshauri apelekwe India kwa matumaini ya kupona,hilo ni jambo jingine.
Lakini hata hivyo hekima ya kutoa ushauri ni muhimu sana sana.Hata kama ushauri ulionao ni mzuri katika mazingira ya mgonjwa kutapatapa huwezi kutoa ushauri kama huo.
Nadhani ungejua kwanza kama wataalamu wameshauri apelekwe India,ikiwezekana wao wenyewe wasaidie kum-council aweze kukubaliana na hali aliyo nayo.
Hapa bongo washasema mzee asubirie tu kudanja. Yupo stage ya mwisho sana. Hamna cha kufanya. Sema ndugu wanataka nao waonekane na wengine wawili nahisi ni safari ya kwenda India ndo wanaitaka si matibabu. Uwezekano wa kupona kwa kansa hamna. Ila Mungu anaweza mponya kwa miujiza so abaki hapa aombewe. Hawataki.wanataka aende india. Mzee mwenyewe kachoka sana....ana kansa ana BP yupo hoi anakula kwa mirija.
 
Kuna mtu alipata mtoto kiwete, hajiwezi, hata kama atakuja kukua hatopata nafuu yoyote ile kutokana na hali yake... wakati tunapiga mitungi na baba mttoto nikatoa maoni yangu kwamba ingekua ni wangu ningefanya maamuzi ya kumpumzisha coz anapata tabu sana kuanzia yeye mwenyewe(mtoto) na wanaomtunza.

Asee nlishambuliwa kwa maneno mengi.

Juzi jamaa kaja ananiuliza afanyaje kuhusu yale maoni yangu... maana imekua tabu... hali ya uchumi mbovu, mke kachoka ye mwenyewe hana muda wa kukaa home....

Nikamwambia afanye anavyoona inafaa kwa kiwa tatizo ni lake.

Sometimes lazma tuangalie faida ya uwepo wetu duniani , km uwepo wako ni tatizo kwa wengine maana yake wewe unatakiwa uwe eliminated kwenye equation, au km sio watu wasiumize kichwa kwa kuwa hakuna faida za kuwekeza nguvu na akili ktk maisha yako.
Te ee!! teee!!teeee!! dogo umenifurahisha sana!!! yaani mawazo yako ni sawa na yaleee ya Rais wa zamani wa Uganda Idd Amini Dada! Yaani huyu Rais ilikuwa hivi ''aliwaita viwete wote Uganda ili awape Misaada!! si wakaja kwa wingi!!

kilichotokea hee!!ee!! wooote humu na Dunia mnajua!! ikawa hivi .....

aliwajaza kwenye zile ISUZU binua mchanga mpyaa!! kma mia hivi, toleo la kwanza lile!! ma-tone kwa ma- tone bana!! kadri zile gari zilivo weza beba, akasema twendeni huku wapendwa mkapate zawadi zenu!!

si Id amini akawapeleka Mto Nile?? Binua zile isuzu binua na wewe, akawa mwaga Mto Nile bana! matani kwa matani!! wale walio ng'ang'ania walikula shaba faster Mchine gun serious!! some wakaliwa na Mamba live!! clip zimo humu!

Alipo ulizwa na Dunia Kwa nini?? akajibu ''eti watu wa hivi hawahitajiki Uganda sababu hawana faida Uganda'' Dunia ilimtafasiri km Rais kichaa!! kuumbe mpaka leo bado mpo watu wenye mawazo km ya huyu jamaa. sasa km ukiendelea kuwazaa wa ivo itakuwaje??

Eliminations of other people in de World lilikuwa ni wazo la Hitre pia!! kuondoa viwete wote ujermani, Jews wote, Germany- Black Africans wote!! akawaweka kwa concetrations Camp, Gas chamber, wakapigwa kiberiti faster! kilichomkuta hee!!

Jiulize nyie Waafrica km wewe! mnamchango gani, humu Duniani ya leo?? si ni kama huyo mtoto tu?? kwani mna nini!! angalia hapo ulipo ni kitu gani is Made from one of African country??

kwa akili zako km ungekuwa mzungu ungeua waafrica wote? maana hawana Faida, kwani wana mchango gani Duniani humu? zaidi ya kupigana miti tu, km ni ivo basi kufa wewe kwanza make huna faida Duniani kwanini hujafa??....

Piga ua galagaza Mataahila, viwete, wenye mtindio wa ubongo hawatakaa waishe humu Duniani, so utakacho kula weye na yeye huyo kiwete atakula hicho hicho !! tena kiipokuwepo mie nikae na njaa ila yeye ale first hicho bora kilicho patikana Daima dumu hafi, yeye kwanza mie wa mwisho!!

tena km ninge weza mngeniletea Mimi! akae kwangu! Naomba Mungu sana km ananisikia nisiwe na roho km hii yako na wengine km wewe!!! ki- Idd Amini! najua mie siwezi ila Mungu ataniwezesha! Kuumbe watu km nyie hamjaisha!!
 
Yeye nyumba hakuirithi. Hivyo hata akifanayo watoto watajenga zao. Tatizo ni pale nyumba inauzwa anaenda India na anapona. Sijui anakuja kuishi vipi. Maana nguvu hana na Mali ishauzwa
Ata panga kupitia watoto hao hao!! si ajabu akajenga Bonge la Bunga low!! kuliko lile alouza!! hata km atapanga ni matumizi pia!! kwani alizaliwa na Nyumba? Mbali na kupanga, mbona Bongo hapo tulianza maisha kwa kukaa kwa watu? tena kwa masimango
Unavurugwa hasa! eti mara una jidai sababu Baba yako ana pesa!! unajisikia,

Mara tumesema kwa watu hao siyo ndug zetu, mara tutelekezwe!! hayo yoote ni ili wapate uhalali wa kutufukuza majumbani mwao!! kisingizio tuna nyodo!

weye unasafiri waenda kuishi Bongo unaacha nyumba safi nzuri full matumizi umeme, maji safi ya ziwani, self container, unaenda anza moja au kupanga Bongo! USA, South africa na kule unaonekana maskini tu! kwani huko unaenda na nyumba yako ya Mkoani kwenu??

Anae kufanyia hivi alikaa kwenu full matumizi wkt babako bado ana nguvu yaani anazo!!! utasingiziwa mambbo kibao mara umemtongoza mke wake na mambo yanayo fanana na hayo!! ili tu uondoke! na kweli unaondoka kwingine!

Dogo mawazo Mgando sana haya! kwa mawazo haya hutakaa utoke kwenu! ukiangalia kajumba aliko weka baba yako unaumia hutakaa utoke hapo!! kuumbe kuna watu wana mijengo hatari!!
 
Mijitu mingine sijui ikoje....hovyo sana. Mtu anakuomba ushauri halafu kumbe tayari ana maamuzi yake kichwani. Unataabika kufikiri unampa ushauri anaanza kuongea shit tena.
Late 70's ana watoto wawili wadogo chini ya miaka 20.....hakika mtihani.....

Poleni kwa kuuguliwa......
 
Ushauri wa kupuuzwa huu, na huyo alikuja kuomba ushauri kwako sio kua utachosema wewe ndo sheria wala usikarike ana haki ya kuukubali au kuukataa.

Na muache kutoa macho kwa mali alizochuma huyo mzee, kama ni kuuza kumtibia yeye ziuzwe tu si zake mwenyewe. Kwa imani yake mzee anaona akipelekwa India atapona, kwa imani yenu mnaona akiombewa ndo ataopona, nyie sio yeye acheni ubinafsi nyie watu fanyeni kile mgonjwa anaona ni sahihi kwa mustakabali wa afya yake.

Na kuna wadau hapo wanasema eti kwa waafrika hawataelewa, aisee nyie watu ni wa ajabu sana kwamba wazungu watu wakizeeka huwa hawatibiwi badala yake wanaachwa wafe?? Na huko kwa wenzetu wazee ndio wengi kwakua wanatibiwa maradhi yao kwa wakati.
 
Mijitu mingine sijui ikoje....hovyo sana. Mtu anakuomba ushauri halafu kumbe tayari ana maamuzi yake kichwani. Unataabika kufikiri unampa ushauri anaanza kuongea shit tena.

Mijitu kama hii ngekuwa na uwezo ngekuwa naiponda tu na nyundo ya kupondea kokoto kichwani.

Mjomba wangu ana kansa inamsumbua muda sasa. Na ukimcheki umri wake nao ushakuwa usiku sana tu miaka ya late 70. Si umri mdogo. Kansa inamsumbua sana na kiukweli ashaambiwa kwa hatua yake utokee muujiza tu.

Kimeitishwa kikao leo tumeongea ndugu n.k kuwa tuchangishane kila mtu pesa isiyopungua Mil moja.sawa mi nimekubali. But pia watoto wake wanataka uza nyumba na some stuff (mali) kaja mama mdogo ananiuliza sasa hili suala la ugonjwa litakuaje.

Mimi nlishawahi sema ugonjwa mwingine watu msilazimishe mtu aishi. Mnamchosha tu mtu mwenyewe ashakula chumvi sana tu.mwacheni ende. Mnamlazimisha kuishi mtu ana kansa, ana BP mnataka aishi kufanya nini?

Sasa nikasema tunaweza changa hizo pesa akaenda India akadanja na hapo nyumba pia imeuzwa n.k hamuoni ni hasara? Wakati tu tungemwacha hapa na kumpeleka kwenye maombi? Sasa naye hataki maombi. Anataka aendelee kunywa mkojo wa shetani(pombe) so anapinga kabisa hbr za maombi.

Basi angekuwa anapinga maombi na kuendelea kupata kinywaji chake huku anasubiri kudanja. Unakuta mbishi. Hataki. Anataka apelekwe India. Sasa nawaza huyu India akafanye nini? Why anang'ang'ania kuishi wakati hana issue yoyote ya maana hapa duniani?

Mtu anatolewa ndani sometimes anaanikwa nje, halafu ana anuliwa kurudishwa ndani. Meno mengi keshapoteza age imeenda. Imekuwa usiku ila mbishi. Sasa nawaza hata akipona lengo lake la kuishi ni nini? Huyu mzee ni kama mchawi tu.

Mimi nimeshauri afanyiwe tu maombi hapa hapa bongo. Mali zisiuzwe ana watoto watano. Wabakize mali ziwasaidie. Hao wawili wa mwishoni wadogo kabisa hawajafika hata miaka 20 wapewe mali kuliko kumtibia mzee ambaye bado anaweza danja wakapoteza mali na mzee mwenyewe. Si bora wabaki na mali?

Mama mdogo anasema nina roho ya kishetani. Sasa nashangaa why alitaka ushauri kwangu? Lakini kibaya nilichosema hapo ni kipi?

Kuharibiana siku tu kwa mambo ya hovyo hovyo. Nirudi zangu tu home nikalale.
 
Miaka 70 anaogopa kufa huyo huenda anaogopa aliyoyatanguliza; Kama ana nyumba moja ikiuzwa baadaye watoto wataishi wapi? Ushauri uliyotoa uko sawa sawa sema watakuchukia waliopanga kupata chajuu mali ikiuzwa.....!
 
Back
Top Bottom