Nimejaa hofu kwa nilichokishuhudia kwa mpenzi wangu

Ndio maana mm sipendi kukagua pochi ya mwanamke...mzee umekuta mpk pu.mbu ya paka iliyokaushwa....subiri mshana aje kwny fani yake
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Eti pum.bu ya paka ...!!!
 
Nenda kwenye ule uzi wao wa uchawi uulize huenda wakakupa jibu
 
Naamini hakuna atakayeleta tafsiri ya kweli kabisa hata kama kilichoandikwa hapo ni fekero,.wengi wataishia kusema hamna kitu, katapeliwa n.k...
 
kakutana na fundi wa kidigital mtoto wa Muji wakala mpunga.Yawezekana hata kumla wamemla .Usicheze na Jeshi la shetani
 
Naamini hakuna atakayeleta tafsiri ya kweli kabisa hata kama kilichoandikwa hapo ni fekero,.wengi wataishia kusema hamna kitu, katapeliwa n.k...
wewe tupe tafsiri sahihi mkuu,hata kwa macho ya nyama kiarabu hakiandikwi hivo.
 
Mkuu kwanza Pole sana. Ila Ukweli hayo maandishi yana Maana kubwa sana katika Lugha ya Majini na Uganga. Hata kama Mtu anajua kiaruabu kama hana Jini au Uganga hawezi kuelewa maana na ndiyo maana siyo Kila anayejua Kiarabu ni Mganga au anaweza ita Jini.

Ila kama akajitokeza Mganga humu ndani ataelewa hiyo Lugha na Maana yake. Japo tunaambiwa tusiamini Uchawi ila Uchawi wa Mapenzi upo asikudanganye Mtu. Ishara ya Kukuta Picha yako na Hicho Kinyama kilichoko kwenye huo Mfuko mara Nyingi wanatumia nyama ya Bundi ili uwe zezeta na kumsikiliza yeye tu.

Kwanza Mshukuru Mungu Kukufunulia hilo. Kama ni Mcha Mungu Omba sana na Kama huyo ni Mke wako Mbane atakwambia ukweli.

Mimi Nayafahamu haya na siku zote hayo Mambo yakigeuka Mwanamke ndiyo ambaye hukimbia Nyumba kwa kukiuka Masharti.

Hiyo ni Lugha ya Kiganga na Huwezi itafsiri kwa kuwa Unajua Kiarabu.

Pole
 

Labda alitaka kukuloga lakini icho sio kiarab.
 
Naamini hakuna atakayeleta tafsiri ya kweli kabisa hata kama kilichoandikwa hapo ni fekero,.wengi wataishia kusema hamna kitu, katapeliwa n.k...
Mkuu hakuna tafsiri yoyote hapo kwa kuwa hakuna maneno ya maana yaliyoandikwa hapo

Hivi unaweza kutafsiri neno hili xsjtky???
Kwa hakika huwezi.
Basi kama huwezi tafsiri neno hapo juu ndo vile vile huwezi tafsiri hayo maneno ya mshirikina tapeli kwenye hiyo karatasi.
 
wewe tupe tafsiri sahihi mkuu,hata kwa macho ya nyama kiarabu hakiandikwi hivo.
Ningekuwa nakijua na kama kilichoandikwa ni kiarab bas nongetoa...hata kama ni mapalanganyata au herufi/ namba ningetafsiri kama ilivyo...
Naamin umeelewa nlichomaanisha...
 
Alisema. Kuanzia Leo utoe ubahili umpe chochote atakacho. Umpende yeye pekee na ukichepuka ka dudu kako kalegee kama mlenda .fungua waleti toa ubahili.
 
Duh.. mlikutana nae wapi huyo mwanamke kwenye mitandao nini???? Hatari sana ingawa siaminigi hayo mambo kama yana nguvu kweli.... Imani tuuuuuu ukiweka hofu ndio itakusumbua sanaaaaaaa
 
Lugha ya Kichawwi siyo Lugha sawa na Kibinandamu.. Ndiyo Mana unakuta Mtu wako Uchi Mahospitalini lakini hakuna anayejua kama kuna watu waliopo Uchi mahopitalini wanatembea mpaka uwe na macho ambayo yapo kati Dunia yao. Hakuna Lugha ya Kiganga ambayo inaweza tafsiriwa na kila Mtu kama ingekuwa hivyo basi wote wangekuwa ni waganga.
 
Nina imani aliwahi kukuuliza jina la mama yako na ukamtajia, manuizi hayo ni hatari but utashinda. Fanya maamzi magumu hizo ni dawa za mapenzi.
 
Mkuu msaada wangu hapo ni kujikausha.. Then unakurupuka kama umepanda mashetani vile..! Unasema sema maneno ya ajabu ajabu yasioeleweka.. Then unamgeukia huyo demu! Unampiga mikwara ya kutisha ukijifanya mashetani yako yamestukia uchawi wake..! Then shetani anasema atoe vitu vyote kwenye mkoba..![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Akitoa na madude yake unamkazia kuwa leo umemsamehe ila akirudia tena kutaka kumchezea kiti ATAKIONA CHA MTEMA KUNI!
Nakwambia harudii tena huyo!
 
Ningekuwa nakijua na kama kilichoandikwa ni kiarab bas nongetoa...hata kama ni mapalanganyata au herufi/ namba ningetafsiri kama ilivyo...
Naamin umeelewa nlichomaanisha...
hicho kiarabu alichoandika hata mie Mgalatia naandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…