Nimejaa hofu kwa nilichokishuhudia kwa mpenzi wangu

Nimejaa hofu kwa nilichokishuhudia kwa mpenzi wangu

Wana jukwaa naomba nisipoteze muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Nimepitia misuko suko mingi sana katika mahusiano,ilifika mahali nikaomba wadau mnishauri kwa baadhi ya mambo yaliyonikumba,nawashukuru wengi mlinishauri na maisha yakaendelea.

Nilipata binti,mpole na mtaratibu sana,nimekuwa naye katika vipindi vigumu na hakuwahi kuonyesha hali yoyote yenye mashaka.

Nimeshitushwa sana leo baada ya kuona vitu vya ajabu kwenye mkoba wake,(ambao sikuwahi kuuona tangu nimefahamiana naye,).

Naviweka hapa,wataalamu wa lugha ya kiarabu naomba mnisaidie kutafsiri maana ya maneno haya,nimekuta karatasi ikiwa na picha yangu,imeandikwa kwa maandishi mekundu kwa lugha ya kiarabu,halafu imefungwa na karatasi nyeusi!!!

View attachment 532069View attachment 532071View attachment 532072
Hiyo ni kombe na huandikwa kwa wino wa zafarani, hutumiwa sana kwenye shughuli za ramli
 
Naamini humu kuna watu wa imani tofauti tofauti,na wenye kujua lugha mbali mbali,nisaidieni tafsiri kwanza,kabla ya maoni binafsi mengine,nina wakati mgumu kweli,sio kwa sababu naogopa kufa kama baadhi ya watu wanavyonitisha hapa,(kila mmoja atakufa tu,kama sio leo,kesho)isipo kuwa wakati mgumu ni kwanini anifanyie hili,(kama ni kwa ubaya)
Acha uoga hupatwi chochote, mimi naona herufi za kiarabu tu zisizo na maana labda awe amechora makosi
 
Hiyo ni kombe na huandikwa kwa wino wa zafarani, hutumiwa sana kwenye shughuli za ramli
So kila kinachoandikwa kwa zafarani nikombe... Kombe linasomeka maana huwa niaya zakurani ..nakombe so shirk... Ila hilo so kombe niuchawi.
 
Inaonekana binti alikwenda kwa fundi labda kukutengeneza ila amekutana na findi tapeli kwa sie tunaejua lugha hii hapo hakuna neno la maana linaloweza kusomeka kwa ufupi naweza kusema fundi kajua huyo binti hajui hyo lugha so ndo maana kaamua kumdanganya

Hapo kaandika herufi tu za kiarabu ni sawa na wewe uandike z,x,c,v,t,y,w,a yaan ilimradi tu umuhadae mtu ila niamini mimi kuwa hakuna maana yeyote hapo na wala hakuna neno lolote la maana lililoandikwa hapo.

Hapa huwa ndo naamini maneno ya dada faiza foxy kuwa "wajinga ndo waliwao" hapo mwanamke wako kadanganywa

NOTE.
Huyo binti anaonekana ni mshirikina leo kapata fundi tapeli kesho aweza pata mkweli na akakutengeneza vizuri tu so kuwa makini sana.
Muombe Mola hakuna linalomshinda sisi waislam tunafundishwa kuwa uchawi upo ila usiuamini sana maana hutomuamini mola.
Muamini mola hakuna linalomshinda na tunafundishwa katika uislam kukaa mbali na shirki (ushirikina) na watu wake.
Nimependa ulivyo mjibu
 
mkuu usiwe na hofu hiko wala si kiarabu mganga wa mjini huyo maana kaunga unga tu
 
Mkuu huyo manzi ni mshirikina hakufai...ukibishia atakutuzusha Simbakaratasi
 
Hayo maandishi yanasema anakupenda na hataki kukupoteza
 
Mkuu huo uchawi kweli unadhani waganga wakitabu huwa wanaandika kiarabu fasaha??? Kombe nitafouti nauchawi wakitabu.. Kombe ndo wanaandika kiarabu maana huwa wanaandika aya za kurani.. Lakini uchawi huwezi kusoma uko hivo.
we nae yaonekana humo Ila huvumi looh
 
Hapo mtafute Alhaji Mohamed Said. Naamini atakwambia what do those words mean!

Kilichoandikwa hapo sio kiarabu per see ila ni lugha ya kuita majini! Kwahiyo huyo dada ni mshirikina tu basi.
 
Hata mimi nilishawahi kuwa na mtu wa mambo hayo lkn labda watakuwa tu walimu wa shule fulani huko Dubai,Afghanistan,Iraq
[emoji125] [emoji125]
 
Dont judge a book by its cover!!!
Yaani ni bora msichana anaekuonesha makucha yake kabisa kuliko sisi wapole!!! Tunaficha mengi
 
Ahsante sana Mkuu,walau umejibu kiu yangu,maana vitisho vimekuwa vingi sana!!!
Akirudi mkalishe chini kwa upole na mpe uchafu wake, mwambie akupeleke kwa huyo fundi na wewe kuna mtu unataka umlimbwate [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom