Nimejaa hofu kwa nilichokishuhudia kwa mpenzi wangu

Nimejaa hofu kwa nilichokishuhudia kwa mpenzi wangu

Huyu jamaa amenifanya nikumbuke enzi za primary kuna jamaa aliibiwa pen sasa alipoona uwezekano wa kuipata haupo akachukua karatasi akaazima pen akaanza kuandika maandishi ya kiarabu huku akitoa onyo kwa yeyote alie iba kwamba ange dhurika. Kuja kuuliza wajuzi wa hayo mandishi kumbe hamna kitu alikuwa anaandika zile alifu be te se...kwa kiarabu.
 
Hayana maana,sema huyo mwanamke wako naye kaingizwa mjini kwa ujinga wake...fanya maisha yako na wewe usiingie kwenye ujinga wake

by emma mjasiriamali
 
Uchawi unakwenda kwa mshirikina. Kama we sio mshirikina wa mambo hayo huwezi patwa na kitu.ishi ukiwa ndani ya Mungu.
 
Hamna kitu hapo utapeli mtupu, hata kama ingaliandikwa Kiarabu kweli basi hivi vitu havifanyi kazi kama vile smartphones.
Kama hicho kitu ni cha uhakika usingaliweza hata kukianika hapa. Ungalifungwa macho hata usikione kabisa
 
Wana jukwaa naomba nisipoteze muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Nimepitia misuko suko mingi sana katika mahusiano,ilifika mahali nikaomba wadau mnishauri kwa baadhi ya mambo yaliyonikumba,nawashukuru wengi mlinishauri na maisha yakaendelea.

Nilipata binti,mpole na mtaratibu sana,nimekuwa naye katika vipindi vigumu na hakuwahi kuonyesha hali yoyote yenye mashaka.

Nimeshitushwa sana leo baada ya kuona vitu vya ajabu kwenye mkoba wake,(ambao sikuwahi kuuona tangu nimefahamiana naye,).

Naviweka hapa,wataalamu wa lugha ya kiarabu naomba mnisaidie kutafsiri maana ya maneno haya,nimekuta karatasi ikiwa na picha yangu,imeandikwa kwa maandishi mekundu kwa lugha ya kiarabu,halafu imefungwa na karatasi nyeusi!!!

View attachment 532069View attachment 532071View attachment 532072
Hizo herufi hazipatikani kwenye lugha ya kiarabu, huenda katapeliwa na huyo mganga akiamini kuwa ndio amekuroga.

Zipo sababu nyingi zinazowapelekea wanawake kufanya hivyo kwa waume zao ambazo ni :-
-Mwanamke kutoka familia duni na kukosa fursa ya kutafuta kipato, akimtegemea mwanaume tu kuwa ndio kila kitu.
-Mwanaume kuwa bahili mno kiasi cha kutomtimizia mahitaji ya mkewe wakati ana kipato cha kutosha laikini matumizi yake hayaeleweki yanafanyika wapi.
-Mwanamke kumpenda sana mumewe na kujijengea dhana au kuhisi kuwa anachepuka.
-Mwanamke kurithi katika familia yake, na ndio maana tunashauriwa kuoa wanawake wenye kushika dini na sio washirikina.


Ukiona mpaka umepata uwezo wa kuviona ujue kitu kimedunda hiko.

Kaza buti bro, kama unampenda mwambie aachane na hayo mambo na ikiwezekana ale yamini msikitini kwamba akirudia tena chamoto kimkute yeye.

Ila huyo mwanamke ni mbaya sana, mshirikina wa kutupwa, hafai kufanya nae maisha. Anaweza akakutilia hata sumu akiona ndumba zimedunda
 
Mimi nafahamu kiarabu. Hakuna kitu chochote kilichoandikwa hapo. Huyo mganga tapeli. Amachora chora herufi zinazofanana la lugha ya kiarabu. Lakini hazina maana yoyote. Ni utapeli wa mjini na kuganga njaa.
 
Back
Top Bottom