Nimejaribu kukaanga Chips sijafanikiwa sana, msaada jamani

Nimejaribu kukaanga Chips sijafanikiwa sana, msaada jamani

Heshima kweny wakuu,

Nimejitahidi kukaanga chips zikaungua kidogo. Sijajua nimekosea wapi, nlitaka nitoe Chips zilizokauka laini na tamu kama zile za pale kwa mdebwedo.

Naomba msaada;

Ni hatua gani zinapaswa kufuatwa ili itoke chips amizing? Naomba utaratibu wa kufuata ili wkend ijayo niitengeneze vizuri. Halafu wkend hii nina mgeni.

Msaada wakuu.
View attachment 389813
Hii nliyotengeneza imeungua kidogo.
ayaah,,,umenikumbusha dame fulani nilikuta anakaanga chips kwa mafuta machache kama anakaanga chapati,hadi saa tisa toka saa nne chips nasubiri bado hazijaiva,,ha ha ha,

nenda you tube search,"how to cook MacDonald french fries"
 
Asante, kilichonichelewesha ni kumenya viazi na kuosha sahani. nlikuwa mbali kidogo. Asante kwa ushauri. Mwisho wa siku ntaomba mtu wa kujitolea aje kunifundisha hili pishi.
Yaani huoshi sahani hadi uwe unataka kuitumia?... Ama kweli wanawake tuna kazi hapa duniani. Mkeo akiumwa siku tatu tunakuja kutoa Funza ndani
 
ngoja nikufundishe, njia ya 1
chemsha maji yapate moto kisha yaepue. ukishaandaa viazi vyako viweke kwenye maji hayo ya moto kiasi kwa dakika 10 hivi, kisha vitoe uchuje maji uweke kwenye mafuta.
kwenye hayo maji uweke na chumvi kabisa.

njia ya 2
andaa viazi vyako viweke kwenye freezer vikishaganda vitoe kisha viache vichujuke ubarafu na uvikaange.
baada ya hapo hakikisha hauvigeuzi geuzi,
halafu jaribu kupikia kwenye sufuria manake hiyo dish inaunguza ukiwa mzembe.
acha kuchat.
Asante sana mkuu, ila mimi nataka vya kukaanga sio kuchemsha. halafu nataka vikauke. Asante, siku nyingine ntakuwa sichati.

Hiyo ya kuweka viazi kwenye freezer inasaidia nini au hiyo ya kusubiri dakika 10? Manake mimi hadi napika, maanake njaa inakuwa inauma. Sasa hapo si ntakuwa napoteza muda?
 
Duu mimi naingia mwaka wa kumi sasa tena kwa kuchelewa saana. ..jitahidi nakuombea
Kila ninaye mpata simuelewielewi, upendo unaisha. Au nmerogwa mkuu? Hongera sana kwa Miaka 10 hiyo, umejitahidi sana
 
Yaani huoshi sahani hadi uwe unataka kuitumia?... Ama kweli wanawake tuna kazi hapa duniani. Mkeo akiumwa siku tatu tunakuja kutoa Funza ndani
Hapana mkuu, hii imetokea bahati mbaya tu, hata nishindwa kuelewa imekuwaje hivi. Ndo maana nikaja kuomba msaada. Mimi huwa ni mtaalam wa kupika Makange na kusonga ugali wa muhogo ulochanganywa na dona. Yaani unakula hadi kujiramba vidole.
 
ayaah,,,umenikumbusha dame fulani nilikuta anakaanga chips kwa mafuta machache kama anakaanga chapati,hadi saa tisa toka saa nne chips nasubiri bado hazijaiva,,ha ha ha,

nenda you tube search,"how to cook MacDonald french fries"
Asante kwa ushauri mkuu. Ila uzuri wa hapa JF unaipata ile ya kinyimbani nyumbani.
 
Hapo umetengeneza chips za kuchoma.

Hivi kuna tofauti gani kati ya chips na viazi vya kukaanga
 
Asante sana mkuu, ila mimi nataka vya kukaanga sio kuchemsha. halafu nataka vikauke. Asante, siku nyingine ntakuwa sichati.

Hiyo ya kuweka viazi kwenye freezer inasaidia nini au hiyo ya kusubiri dakika 10? Manake mimi hadi napika, maanake njaa inakuwa inauma. Sasa hapo si ntakuwa napoteza muda?
hebu nisome vizuri.

hiyo ni option kwa anayehitaji kitu kizuri...
 
Mkuu, acha kunikatisha tamaa ya kujifunza kupika. Nmeomba ushauri, kama unaweza nifundishe. Hata hivyo haijaungua hiyo bali imebadiika rangi, nahisi ni kwa sababu ya mafuta yatakuwa yameungua.

Ukichanganya mafuta ya transformer kidogo tu haziungui tena [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]
 
pamoja nakuwa mwanaume mie sijawahi kufeli kupika aisee japo sina mke
 
figuost: 17396937 said:
Nielekeze mkuu. Inasaidia nini? Hazitepeti?
zitatepeta ukizigeuzageuza mara kwa mara.
ila kama ukizitoa kwenye maji ukazichuja na kuzitia kwenye mafuta, zinakua na ladha flani amazing.
 
Bro.
Umetengeza kaukau za viazi, wallahi sio chipsi hizo...
 
Hapo umetengeneza chips za kuchoma.

Hivi kuna tofauti gani kati ya chips na viazi vya kukaanga
Wewe hujui kupika wala huwezi nicheka[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom